Rais Magufuli na Rais Chakwera waweka jiwe la msingi Kituo Kikuu cha mabasi Mbezi, Rais Magufuli ataka Wakandarasi walipe fidia ya kuchelewesha mradi

Rais Magufuli na Rais Chakwera waweka jiwe la msingi Kituo Kikuu cha mabasi Mbezi, Rais Magufuli ataka Wakandarasi walipe fidia ya kuchelewesha mradi

Turudishe hapo kwa Bella kumpigia kampeni mgombea wa CCM! NEC wanasoma hapa na wanamuona raia wa kigeni asiyeruhusiwa kisheria lakini wamenyamaza Kama kwamba Sheria za uchaguzi zinaruhusu na wewe kwa uzwazwa unaofanania na huo wa nec unashangilia pasi na shaka!
 
Huyu ni msanii tunaweza hata kumleta hapa neyo au rihana wakapiga kamapeni jukwaani kutumbuiza
Turudishe hapo kwa Bella kumpigia kampeni mgombea wa ccm! Nec wanasoma hapa na wanamuona raia wa kigeni asiyeruhusiwa kisheria lakini wamenyamaza Kama kwamba Sheria za uchaguzi zinaruhusu na wewe kwa uzwazwa unaofanania na huo wa nec unashangilia pasi na shaka!
 
PAYE hii ambayo licha ya kushuka watu wamekuta sh. 5000 tu ndo imeongezeka!?

Hata JK alikuwa anashusha kodi na wakati huo huo anatoa "annual increment" na kupandisha watu vyeo.

Huu utopolo wenu mnaousifia hapa ndio unawafanya watanzania waishi kama wakimbizi kwenye nchi yao ya kuzaliwa.

Hawezi kushinda uchaguzi huyu dikteta, anapingwa kila kona ya nchi.
PAYE imeshuka tayari. Watumishi wengi wamefurahishwa na hili. Wewe siyo mtumishi wa umma inaelekea.
 
Kwa taarifa yako, mimi ni mtumishi wa umma na niko kwenye wizara moja nyeti sana. Lakini simpendi Meko kwa huu udhalimu anaotufanyia.
PAYE imeshuka tayari. Watumishi wengi wamefurahishwa na hili. Wewe siyo mtumishi wa umma inaelekea.
 
Fidia ya CCM watalipia 28/10/2020 kwa kutucheleweshea maendeleo kwa miaka 59!
 
Kwakweli ni kituo kikubwa na cha kisasa kabisa Afrika Mashariki na kati. Ni Lango kuu la kukuza Uchumi wa Tanzania, hongera sana Rais JPM.


Mkuu wakikusikia waluguru mtabishana mpaka kesho wao wanajua kile chao pale ndiyo baba lao kwa Africa Mashariki na Kati
 
Huu mradi wa serikali lakini tunaona kijani tu kama vile ni kampeni. NEC mnasemaje au mnaogopa kutumbuliwa. Si vizuri wakati wa kampeni kufanya haya maana yanaonekana kufanya kampeni kwa aina nyingine.

Anyway tunawatakia wagombe wote afya njema na huyo atakayechaguliwa tutamunga mkono kama uchaguzi utakuwa wa haki.
 
Hata mimi nilidhani kituo cha bus ni kitu kidogo sana kwa rais wa nchi ya jirani kuja kuweka jiwe la msingi.

Anyway pengine ni u-layman wangu wa kutokujua hizi mambo.
Ulitaka azindue kwa Zoom?
 
Back
Top Bottom