Uchaguzi 2020 Rais Magufuli na Tundu Lissu wote ni Wakatoliki wazuri. Je, Kanisa halioni umuhimu wa kuwapatanisha?

Hakika haya ni mambo ya kaiser si ya Yesu mtoto wa Maria
 
Umeongea mambo ya hekima,Amani ya kweli huletwa na vitendo vya Haki vinavyozingatia Utu na Usawa kwa wote huku tukiepuka Ubaguzi wa aina yoyote.Vinginevyo tutakuwa wasindikizaji hapa Duniani.
 
Wakatoliki huwa tunamwabudu na kumsifu Mungu- kati ya hao kuna jamii hana akiandaa hotuba anapenda kujisifia kuliko Mungu--
 
Nadhani hujanielewa japo najua unaelewa kosa ambalo kanisa lilifanya katika mauji ya Kimbari huko Rwanda, kanisa katoliki kamwe haliwez kukwepa lawama , wahanga wa mauaji walikimbilia makanisani wakiamini ni sehemu salama, lakin viongozi wa makanisa wakawasaliti kwa wauwaji, kitendo hiki hakikupaswa kufanywa na viongozi wa kanisani Katoliki ambalo limekuwa likitufunza juu ya Usaliti wa akina Peter na Yuda walichokifanya kwa Bwana Yesu na kutuasa tuwe tayari kwa ajili ya wengine, kwa mfano hii ni sawa na majambazi wavamie kwako usiku wakwambie usipotuonesha watoto wako walipojificha tunakuua wewe, kwa kuogopa kufa unawaelekeza watoto wako walipo kisha wanauawa na wewe unabaki salama.

Kwa baba ambaye anasimama katika nafasi yake anapaswa kufa kwa ajili ya wototo wake. Maana yake viongozi wa Dini hawakuwa tayari kufa kwa ajili ya wengine. Hali hii bado inaendelea mpaka sekunde ya leo. Viongozi wa kanisa au kanisa kiujumla ikiwemo RC wamekuwa watu wa kufumbia macho uozo unaofanywa na viongozi wetu kisa tu wanaogopa kuwakemea ili wasisumbuliwe. Hii ni ishara kwamba wanacho wafundisha waumi hakina uhalisia na maisha.

Rejea mateso aliyoyapata Yohana kutoka kwa mfalme Herode, rejea mtumishinwa Mungu Ayubu alivyoteseka mpaka hatua ya mwisho. Leo viongozi wa Dini hii na wengine hawana uwezo wa kumwita Magufuli na kumwambia hapa umekosea mbali kwamba ni watumish wa Mungu ambao wanapaswa wasiogope mtu yeyote pale anapofanya maovu. Hivyo ndiyo maana suala la Rwanda hawawezi kwepa lawama si kwamba walikuwa wameshika mapanga wanaua watu la hasha!
 
Jibu la swali lako analo Lissu.

Anayoendelea kusema dhidi ya Mkatoliki mwenzake, katika ziara yake yakutafuta wadhamini, huku akifanya kampeni ya kumchafua mgombea mwenzake, yatajibiwa na wagombea wengine kampeni zitakapoanza.

La msingi anafanya makusudi ili Serikali imchukulie hatua, lengo ambalo halijatimia.
 
Kwani mtu akiongea jambo anatakiwa kuchukuliwa hatua??? Jibuni hoja acheni ubabe!!

Ni raisi gani aliwai kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwao????
 
Kupatanishwa na Lissu? Huyu mtu anayeuza nchi mchana kweupe? Labda kama kanisa halina kazi za kufanya.
Labda una uwezo mdogo wa kufikiri kiasi kwamba ukidanganywa kuwa watu wanaweza kuuza nchi ukakubali-
Wengine kwa uwezo wenu mdogo wa kufikiri mkiona wazungu nchini mnaweza kusema nchi imeuzwa-
 
Labda una uwezo mdogo wa kufikiri kiasi kwamba ukidanganywa kuwa watu wanaweza kuuza nchi ukakubali-
Wengine kwa uwezo wenu mdogo wa kufikiri mkiona wazungu nchini mnaweza kusema nchi imeuzwa-
Nahitaji kudanganywa wakati nayaona. Hakuna mtu mwenye akili timamu anyeweza kumpa urais Tundu Lissu. Mnapoteza muda tu
 
Kwani mtu akiongea jambo anatakiwa kuchukuliwa hatua??? Jibuni hoja acheni ubabe!!

Ni raisi gani aliwai kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwao???? Jibu hoja hiyo wewe Lumumba project???
Sheria ya Ucjaguzi, 2010, Ibara ya 51 inatoa utaratibu wa kufanya kampeni. Muda huu ni wa kutafuta wadhamini.

Kujenga uwanja wa ndege kwani ni dhambi kwa WaTz wa huko? Mbona huoji kurejeshwa kwa reli ya Moshi-Arusha au Meli ya Victoria?

"Charity begins at home” walinena huko majuu. Kama nyumbani kwako hahaweka kitu huaminiki kwa jamii. Huo ndio msingi wa kuonesha uwezo wa mtu.
 
Kanisa liwapatanishe kwani Magufuli kamkosea nini Lissu au Lissu kamkosea nini Magufuli?

Je Lissu kupinga aina ya utawala wa Magufuli ndo kanisa limtulize aunge mkono Juhudi au?

Au kanisa limuingilie Magufuli ili aache aina yake ya utawala au?
 
Kwa nini wapatanishwe? hawa watu 2 hawajakosana. Ni washindani tu wa kisiasa. Sisi wapiga kura ndo "tutawapatanisha" Octoba 28!
 
Kama nixuluhu mnataka na xixi jiwe aingie kwenye gari lake tumfetulie rixaxi 36 af akitoka xalama kama mwenzake bax tuwapatanixhe kwani kila mtu atakua na amani kwa hilo.lkn akibahatika kufa nixafi xan tutamfukia kiroh xaaaf
 
Kwani wamekosana?
 
Magufuli ni Mkatoliki. Lakini jee Lissu ni Mkatoliki pia? Hilo sina uhakika. Hata kama ni kweli wote ni Wakatoliki, litakuwa si jambo la busara kwa Kanisa kuingilia kati tofauti hizo za kisiasa. Ni sawasawa na kusema Kanisa liegemee kwa Magufuli dhidi ya Lipumba au Maalim Sefu ambao ni Waislamu. Kwa vitu vya kidini ni sahihi kwa Kanisa kuingilia kati, kama lifanyavyo kwa wanandoa wa Kikatoliki. Lakini kwa tofauti za kisiasa, kamwe Kanisa lisihusike.
 

Watakatifu huwa ni wazungu tu? We ni MTUMWA wa Karne ya 30
 
Magufuli inabidi amwombe msamaha lissu, alichonifanyia siyo ubinadamu,

Hasitahili hata kupokea Eucharist takatifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…