Hawana ugomvi ila wana tofauti za kimtizamo na kimkakati. Kama watu wana mitizamo tofauti huwezi kuwapatanisha, Kwa mfano inawezekana mmoja anaamini kuwa ana mamlaka ya kufanya lolote analoona ni jema (wewe unaweza usione kama ni jema) na kweli kikatiba anayo mamlaka, na mwingine anaona si sawa kutumia mamlaka hayo hivyo, na hivyo anafikiri katiba ifanyiwe marekebisho ili hayo mamlaka yapunguzwe au yawekewe utaratibu wa kuyatumia. Katika hali hiyo Kanisa linaweza kuingiliaje?
Kuna tofauti ambazo kanisa linaweza kuingilia na kusuluhisha kama vile ugomvi halisi, kuumizana, nk. Na ili kanisa liweze kufanya hivyo, lazima lisiwe na upande wowote iwe kwa kulaumu au kwa kusifia.
Lisu na Magufuli wakikutana kanisani watapeana mkono wa kutakiana amani ila wakipanda kwenye ulingo wa kisiasa - ni tofauti