Rais Magufuli, namuombea msamaha Paul Makonda. Msamehe

Rais Magufuli, namuombea msamaha Paul Makonda. Msamehe

Watu sijui mkoje. Kwan Tanzania nzima yupo yeye tu mwenye vigezo, kwani lazima yeye ndio atumikie wananch?.
Unaona walio kaa ktk nafasi zingine hawastahili au anastahili yeye tu??

Mhubiri 9:11
[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
Hapo ndo wanamharibia kijana wa watu yye alishasema hapangiwi
 
Afu mkiwa madarakani mnadai vijana mjiajiri. Huyo tayar anamtaji lakini bado mnamuonea huruma. Wapo vijana wanataman hata mtaji wa milion tu watusue life nyie mnaanza kuangaika na wakulitaka mwenyewe
 
Makonda umekuwaje?
Huwezi kuishi kama sisi tunavyoishi hadi utagemee huruma za Rais?

Ulionywa kwa maneno haya "Toshekeni" wala hukusikia.Unajua kuna watanzania wangapi wenye uwezo mkubwa sana na wazalendo hawajapata nafasi uliyokuwa nayo?
Unajua kwa Mungu huyu anatufahamu mimi nikiwa mmoja wao,kuwa tunaeweza kufanya mambo makubwa sana ila tumekuwa wapole tu hadi Mungu aamue mwenyewe tu kutuinua?

Tafadhali usijiaminishe sana kuwa u peke yako na hivyo kuhitaji huruma kila wakati.Fanya kazi nyingine za ujasilia mali ikiwemo kilimo
 
Amsamehe kwani kamkosea nini? Muda wake umekwisha apige mishe nyingine, Haya mambo ya kulipana fadhila sio kabisa.
 
Lao moja hao ni kwamba kipindi hiki cha uchaguzi ameamua kujitenga nae ili asipoteze kura baada ya hapo ndoa yao itaendelea kama kawaida
 
Mhe Rais wetu, na viongozi wote wa serikali yako, sisi kama vijana tunayemtazama. Paul Makonda kama chachu ya uongozi katika mioyo ya vijana, tunakuja mbele yako kwa unyeyekevu mkubwa kuomba msamaha wa yale yote aliyoyafanya kinyume na matakwa yako na serikali yako kwa ujumla.

Tunaamini yapo mapungufu mengi aliyonayo na yapo makosa mengi aliyoyafanya hata ambayo sisi tunaweza tusijue, ila tunakujua wewe Mh. Rais kama Baba mwenye upendo, mwenye huruma, kipenzi cha vijana wa taifa hili, mwenye moyo wa kusamehesaba mara sabini maana tumekushuhudia ukitusamehe vijana wa taifa hili. Tunakuomba sana baba msamehe Makonda mpe nafasi nyingine itakayokupendeza ili aendelee kuwatumikia watanzania.

Tunaamini bado anayo akili, utashi, ujasiri na upendo kwa nchi yake. Bado ana vitu vingi sana vya kuwafanyia wanyonge wa nchi hii. Bado tunaamini anayo nguvu ya kuendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo kwa 2020-2025 imesheheni mipango mingi na mizuri sana kwa kijana wa nchi hii.

Baba msamehe Makonda mpe nafasi katika serikali yako.Tunakuahidi kukupigia kura nyingi za kishindo, zitakazoonyesha shukrani yetu kwa kazi uliyoifanya kwa nchi hii.Kwa yeyote anayeweza kumfikia Mh. Rais, tunakuomba umwambie tunampenda, tunamuomba amsamehe Makonda, yatima, wajane, maskini, wanyonge na vijana wanchi hii tunamkumbuka na kumuombea msamaha.

Lakini pia tunamuomba Askofu Gwajima amsamehe na kumuondolea laana aliyoitamka madhabahuni kwake ya kumfuta katika siasa za nchi hii juu yake. Bado ni kijana mdogo anayehitaji kusamehewa na kufundishwa. Taifa hili bado linahitaji mchango wake.Mungu awabariki sana.Kwa niaba ya tunaomkumbuka Makonda.


[email protected].View attachment 1556427View attachment 1556428


NOTE: MLETA MAADA HANA MASLAHI WALA HUUSIANO NA UJUMBE HUSIKA, HIVYO HASIUSISHWE MOJA KWA MOJA NA MADA, YEYE NI MLETA TAARIFA TUU.

Hivi huu ujinga tutaacha lini watanzania wenzagu!! Hivi unajua TZ ina watu wengi wasomi, wenye kila aina ya skills katika utawala wengine tena wamo CCM!! So why Makonda!! Ukiangalia zile clips za Polepole na Bashiru wakionya Mkuu wa Mkoa kugombea Kigamboni tena Pole pole akaenda mbele zaidi akionya kuwa hayo ni maelekezo ya Mwenyekiti kuwa Mkuu wa Mkoa Dar asijaribu kugombea Kigamboni!! Aridhike na U RC DSM!! Still Makonda akakaidi akaenda Kigamboni!! Na akapigwa!! Sasa huu msamaha ili iweje? Kuna waTZ wengi sana including CCM members ambao wanaiweza kazi hiyo na wanamheshimu sana JPM kuliko kijana huyu aliyejaa kibri huku akijinasibu eti katika Nchi hii hakuna anaekula raha kama yeye!! Kweli? [emoji15][emoji15]
Basi aachwe aendelee kula Raha!! Wachapa kazi wenye nidhamu na maadili ya uongozi watajaza hiyo nafasi!! Hatukuzaliwa na vyeo!! Bali huja na kuondoka!!
 
Mbona kaanza kulialia mapema sana.hakujiwekea akiba na malengo ikitokea hana hiyo kazi ya RC?
 
Si kila siku mnaimba vijana wajiajiri sasa wewe unashindwa kujiajiri bwana makonda?
 
Kafanya kosa gani kwani? Kuna adhabu gani aliyopewa kwani kwa hilo kosa?
Aliamua kuacha kazi abet ubunge mhindi kachana mkeka wa ubunge na alistake ukuu wa mkoa kaamka wajumbe wamemchania mkeka na ukuu wa mkoa umeota mbawa sasa anasaka mtaji tena ili abet maisha mengine.
 
Aliamua kuacha kazi abet ubunge mhindi kachana mkeka wa ubunge na alistake ukuu wa mkoa kaamka wajumbe wamemchania mkeka na ukuu wa mkoa umeota mbawa sasa anasaka mtaji tena ili abet maisha mengine.
Kuacha ukuu wa mkoa ili kugombea ubunge ni kosa? Tangu lini? Mbona jiwe aliacha uwaziri wa barabara akakimbikia form za urais? Na yeye aadhibiwe?
 
Huyu atakuwa makonda mwenyewe ameonja joto ya jiwe ya kukaa bila Kazi
 
Bashite ana jina jipya siku hizi DOMITIAN...

Siku hizi hata kampeni za chama, wanambagua!
Dunia ipo kasi, ukizubaa inakuacha aisee!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Back
Top Bottom