Nimegundua Rais kukosa “consistency” kwenye maneno yake ni kitu kinachokosolewa na watu wachache sana, wengine ni kama hawaoni na hata kama wanaona hawaelewi kama ni tatizo, Nadhani sababu kuu ni “kufanana naye”, Watanzania wengi ni waongo, vigeu geu na hawawezi kusimamia maneno yao. Huu umegeuka kuwa ni utamaduni wa mtanzania. ( M-bongo)
Consistency ni moja kati ya interpersonal skill ambayo mtu anaweza kufundishwa, kwanini wasilifanyie kazi hili suala? Ni jambo la kufedhehesha Rais kila mara ananukuliwa akitoa kauli zinazokinzana, kila mara anakula matapishi yake, aibu kubwa.