Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Natamani hata hiyo 2020 ashindwe ila ndo hivyo tena tume yenyewe anaitue yeye na wakurugenzi wa wilaya anawateua na kuwapa mishahara yeye!
 
Hii siyo tabia nzuri, Rais wa Tanzania hana lolote la kuinga kutoka Uganda na Rwanda. Tanzania iko juu sana katika mambo mengi mazuri. Hana la kujifunza pale.
Tayari kesha jifunza kwa kagame namna ya kuwa treat wapinzani wake ktk siasa.
 
Wananunua wabunge halafu watabadilisha katiba ataiheshimu hiyo iliyobadilishwa
 
Rais Magufuli akiwa Korogwe Tanga amesema hayuko tayari kuendelea kuongoza baada ya miaka 10 iliyowekwa kikatiba. Ameyasema haya baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Prof. Maji Marefu) kusema Rais anastahili kuongezwa muda ilia afanye mambo mengi zaidi.

Its official kuwa Magufuli hataongeza muda wa kukaa kwenye kiti cha urais. Hii kauli imemaliza wasiwasi wa watu wote waliokuwa na speculation kuwa Rais anaweza kuongeza muda wa kukaa madarakani.

Shangilieni tu ila ikitokea katiba imebadilika na kuondoa ukomo wa miaka 10 msije hapa kupiga kelele maana akiendelea atakua ameiheshimu katiba pia. Kumbuka kubadili katiba kunahitajika 2/3 ya kura za wabunge wa bara na 2/3 ya wabunge wa Zanzibar. Baada ya hamahama hii nadhani CCM tuna 2/3 tayari kwa bara. Come 2020 sioni wabunge wa upinzani wakirudi bungeni labda wawili au watatu hivi. Na huko Zanzibar CUF inaelekea machoweo, kwa mweleleo huu 2/3 zinaweza patikana kwa bara na visiwani na inatosha kuondoa ukomo wa urais. Na hapo lazima tukubaliane kuiheshimu katiba kama tunavyoiheshimu ya sasa.
 
Hakujawahi tokea serikali yenye kujali manendeleo kama hii ya tano tukiachana na baba wa taifa

Rais wa sasa kaiwezea tanzania kila unapo safiri ndani ya tanzania lazima kuna mradi mkubwa wa maendeleo una tekelezwa

Na hiki ndicho watanzania tunataka sio kukaa kwenye mitandao huku umejifungia chumban unalalamika lalamika .

Tembea uone namna nchi inavyo shambuliwa na maendeleo pamoja na ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali.
 
Naona mnataka watu waanzishe vikundi vya waasi

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
endelea kujifurahisha, muda wake utaisha na ataondoka.... atakayekuja atakuja na vijana wake hivyo akina bashite andalieni familia zenu 'mazingira'
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakujawahi tokea serikali yenye kujali manendeleo kama hii ya tano tukiachana na baba wa taifa

Rais wa sasa kaiwezea tanzania kila unapo safiri ndani ya tanzania lazima kuna mradi mkubwa wa maendeleo una tekelezwa

Na hiki ndicho watanzania tunataka sio kukaa kwenye mitandao huku umejifungia chumban unalalamika lalamika .

Tembea uone namna nchi inavyo shambuliwa na maendeleo pamoja na ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali.
Hujui kuandika [emoji107] na ndiyo maana unasifu na kuabudu !!

Kila awamu imefanya yake. Naye afanye yake asingoje shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom