Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Ukweli ndo huo kwa Mungu na malaika, hiyo ndo Hali halisi bila kuficha, mpendwa raisi wangu angalia matokeo ya uraisi ya KIUKWELI utaona picha halisi, wanasema uongezewe muda Ni kwa masilahi yao.
 
Mkuu wetu wa nchi hii nchi unayoiongoza ina wananchi takribani mil 60. Kati ya hao ni 5% ni wanasiasa. Lakini wengi wao amaboa ni 95% ni wakulima na wafanyakazi.

Wewe unayo mamlaka ya kupata maoni ya nini 95% ya raia wa Tanzania wanatoa maoni juu ya uongozi wako.

Ukweli usiopingika wafanyabiashara wengi hawataki uongezewe muda hata sekunde moja. Maana tangu umeingia madarakani umekuwa mwiba kwao. Biashara zimefungwa sababu ya kutaka walipe kodi hata kama mazingira ya kibiashara sio rafiki. Kila sekta ya kibiashara imeganda.

Wakulima wapo kimya wanaugulia moyoni. Maana tangu uingie madarakani hali yao kuuza mazao imekuwa mbaya.Mazao ya nafaka mengi yamekosa soko hasa la nje ambalo ndio chanzo kikubwa cha mapato yao.

Wafanyakazi wa umma ndio wanakilio kikubwa. Wao wanaomba Mungu ustaafu hata kabla hujamaliza muda wako. Maana hujaongeza mshahara kwa miaka mitano tangu uingie madarakani. Hali ya maisha ni ngumu kwao maana maisha ni ghali.

Je kwa mazingira kama haya nani ambae ni mwananchi wa kawaida atataka uongezewe muda wa kutawala?

Hao wanasiasa wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ambao ni 5% ya watanzania? Wewe ni mkuu wa nchi. Fanya utafiti juu ya hili. Wananchi wa kawaida wanaomba Mungu miaka minne iishe haraka aje rais mwingine mwenye huruma ili maisha yaendelee. Usidanganywe na akina Jah pipo wa Njombe.
Ongezea na ukosefu wa ajira,udikteta.
 
Makes a lot of sense. Ushauri mzuri sana, kama Raisi anao watu wazuri wa kumshauri, basi ukweli huu ataupata, na atabadilika.
 
Pale CCM ukisema jambo lisilotakiwa utakaripiwa na kuonywa vikali sana na wala hutarudia kamwe wanaweza kukuambia hata wakufutie uanachama refer kww akina sofia simba yaliyowapata....

NAJIULIZA Hawa wanaosema kila siku kuongeza Muda kinyume kabisa na Katiba hivi wao kwann wasiitwe wahojiwe na kuonywa vikali?? Happ ndipo huona jambo hili yawezekana lina kitu.
 
Mkuu wetu wa nchi hii nchi unayoiongoza ina wananchi takribani mil 60. Kati ya hao ni 5% ni wanasiasa. Lakini wengi wao amaboa ni 95% ni wakulima na wafanyakazi.

Wewe unayo mamlaka ya kupata maoni ya nini 95% ya raia wa Tanzania wanatoa maoni juu ya uongozi wako.

Ukweli usiopingika wafanyabiashara wengi hawataki uongezewe muda hata sekunde moja. Maana tangu umeingia madarakani umekuwa mwiba kwao. Biashara zimefungwa sababu ya kutaka walipe kodi hata kama mazingira ya kibiashara sio rafiki. Kila sekta ya kibiashara imeganda.

Wakulima wapo kimya wanaugulia moyoni. Maana tangu uingie madarakani hali yao kuuza mazao imekuwa mbaya.Mazao ya nafaka mengi yamekosa soko hasa la nje ambalo ndio chanzo kikubwa cha mapato yao.

Wafanyakazi wa umma ndio wanakilio kikubwa. Wao wanaomba Mungu ustaafu hata kabla hujamaliza muda wako. Maana hujaongeza mshahara kwa miaka mitano tangu uingie madarakani. Hali ya maisha ni ngumu kwao maana maisha ni ghali.

Je kwa mazingira kama haya nani ambae ni mwananchi wa kawaida atataka uongezewe muda wa kutawala?

Hao wanasiasa wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ambao ni 5% ya watanzania? Wewe ni mkuu wa nchi. Fanya utafiti juu ya hili. Wananchi wa kawaida wanaomba Mungu miaka minne iishe haraka aje rais mwingine mwenye huruma ili maisha yaendelee. Usidanganywe na akina Jah pipo wa Njombe.
Mitano Tena.Amri!
 
kwenye soko la mazao nje hapo kweli ni kilio

na hawa TRA tabia ya kufuatiliana nyuma nyuma kisa kuangalia kama una risiti au laah itakuja watokea kwa pua, walimfuatilia kijana wa baiskel alikuwa amebeba sukari kaagizwa dukan kabla hajaishusha wakamdaka aisee jamaa hajui kabisa kujitetea yeye akachomoa kisu tuu, wakaona waachane nae

sasa yote hayo ya nini
 
Toka Uhuru tulikuwa na uongozi wa Nyerere, watu hawakuhoji juu ya miaka yake ya kukaa madarakani.

Inawezekana hatukuwa tunajua Nini maana ya uongozi bora kwakuwa hatukuwa na jerea.

Ilipokuja awamu ya Mwinyi watu wakaanza kuulinganisha na uongozi wa Nyerere,wakaanza kutoa kasoro.
Hali hiyo imeendelea mpk awamu hii.
Watu kaanza kuyaona hata makosa ya Nyerere kwa kulinganisha na awamu zilizofuata.

Tofauti ya awamu hii na zingine ni moja tu,WATU
KUHOJI SUALA LA KUMUONGEZEA MAGUFULI MIAKA YA KUTAWALA.
Jambo hili mpaka awamu ya Kikwete halikuwepo.
Hii inaonesha awamu hii haikubaliki kabisa na watanzani85%
Ila inakubalika na wachache wanaomzunguka mkuu, Kama kina Butiku, makamba Yusuf na ccm wachache wanaomega mkate pamoja na mkuu.

Hivyo ccm, msiwalazimishe watanzani kubadiri Katiba yao kwa kubadiri ukomo kwaajili ya magufuli.

Ccm mtambue kuwa watanzania wanazidi kuelimika, wanazidi kupata ujasiri, ipo siku mtatusababishia vurugu na umwagaji wa damu.

Watanzani watadai haki yao ya kikatiba Kama kwa mkoloni wa ndani.

Sasa tumetambua kuwa kumbe mbunge wa chemba mlimtuma kuchokoza mada ili kupima upepo.
ACHENI JAMBO HILI HARAKA
 
CCM bwana hawataki katiba waliyotengeneza wananchi kipindi cha Jaji warioba wanataka katiba waliyotengeneza wao!!!

Ndugu wanasema hayo ni kutest kina cha maji na upepo unaelekea wapi,
 
Ukweli ni kwamba, hizi kelele za baadhi ya watu kutaka Magufuli aongezewe muda, ni kelele tu za watu wachache ambao ama wanafaidika na huu utawala, au wanatumika na huu utawala kuendesha hiyo kampeni na si vinginevyo.

Ni imani yangu, watanzania wengi wanatamani muda wake uishe aondoke apishe wengine kuanzia wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, watu walioko katika sekta ya madini, vijana wanaotafuta ajira, n.k kiasi kwamba hata kura ya maoni ikipigwa leo hii kuhusu swala hili la kumuongezea Magufuli muda wa kukaa madarakani, hawezi pata uungwaji mkono hata wa asilimia 30 ya kura zote zitazopigwa.

Hata baadhi ya aliowapa vyeo nao wanaweza kupiga kura ya kukataa jambo hilo kwani hata wao hawana uhakika wa nafasi zao huku wako ambao na wao wanatamani hiyo- nafasi ya uraisi.

Siamini kabisa kama watu wanafurahia namna Magufuli anavyoendesha hii nchi wakiwemo wana-CCM wenyewe kwani ni wazi kauli za Magufuli na vitendo vyake haviwapendezi wengi na mfano mzuri ni kauli ya hivi karibuni kuhusu madakatri walioacha kazi serikalini na ile ya kuhusu kutoa chakula cha msaada wakati wa njaa kwa wananchi kauli hizi zikiwa ni muendelezo wa kauli zake zenye ukakasi tangu aingie madarakani mwaka 2015.

Ukiacha maswala kama ya kutoongeza wafanyakazi mishahara, wafanyabiashara kubambikiziwa kodi kubwa, mazao ya wakulima kukosa soko,kuminya uhuru wa maoni, kukandamiz demokrasia,vitendo vya utekaji, n.k ,jambo lingine linalommaliza vibaya kisiasa ni ili la kuutangazia umma kuwa hakuna Covid na kuonekana ni kosa kusema mtu fulani kafa kwa corona katika nchi hii wakati mitaani hali inaonekana kuwa ni tofauti.

Jambo lingine linalomuweka pabaya kisiasa ni tuhuma za kutumia fedha za umna kuendeleza sehemu anayotoka (Chato), jambo linaloonekana kuwakera watanzania wengi na hivyo kujiuliza iwapo ataongezewa muda hiyo Chato itakuwaje ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi na maswali mengine mengi.

Kwa kifupi, kulingana na mtazamo wangu na ambao naamini ni mtazamo wa watu wengi pia, Magufuli amefeli sana katika swala zima la uongozi na alichoweza ni kuendeleza tu sekta ya ujenzi na miundombinu mambo ambayo hayawezi kumfanya aonekane anastahili kuongezewa muda kwani mahitaji ya watanzania ni zaidi ya miundombinu.

Hivyo, kutokana na sababu hizo na zingine ambazo sikuzitaja(amabazo unaweza kuzitaja), Magufuli hawezi pata uungwaji mkono hata wa asilimia 30 litapokuja swala la kura ya maoni juu ya kumuongezea au kutumuongezea muda wa kukaa madarakani.
 
Back
Top Bottom