Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

HABARI: Rais John Magufuli amesema hawezi kukaa kwenye urais miaka 20 kama alivyoombwa na Mbunge, Steven Ngonyani kwa kuwa ni kinyume na katiba.

Mh Rais anahutubia muda huu hapa Korogwe Stand,Tanga.
Labda kwa mbinu za kamati za Ufundi kama uganda, Zimbabwe na Rwanda lakini kwa njia za kawaida ni vigumu sana tambua watanzania wanataka maendeleo sio visasi kukomoana kubambikiana kesi na kuchukua pesa za Umma kuwanunua madiwani wa chadema na kumpatia Lipumba adhoofishe Ukawa, hakuna viwanda tena pesa yote inatumika kukandamiza Demokrasia.
 
Ili asionekane mlevi wa madaraka,dikteta!!! Huku wanaosema atawale milele wanavunja ratiba na yeye anajua ni kinyume cha katiba,aamuru wakamatwe kwa uchochezi basi kama habariki hizo hadaa!!!
 
HABARI: Rais John Magufuli amesema hawezi kukaa kwenye urais miaka 20 kama alivyoombwa na Mbunge, Steven Ngonyani kwa kuwa ni kinyume na katiba.

Mh Rais anahutubia muda huu hapa Korogwe Stand,Tanga.
Kama anaikumbuka katiba na aliapa kuiteteana kuilinda mbona anafanya mengine ambayo anaikiuka hiyo katiba [ mfn KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA KWA WAPINZANI ]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aibu ya Mzee Mwinyi,Maji Marefu na taka taka zote zilizokuwa zinapigia upatu nyongeza ya muda wa muhula by 2025!
Halafu yule ndezi wa OP ya BAKI MAGUFULI aweke tako lake chini...
2025 tunawaletea jembe lingine!
Inaonyesha jinsi ulivyo shallow au haukumuelewa mzee Mwinyi, alisisitiza kabisa KAMA KATIBA ingeruhusu!!
 
JAMANI WAFANYAKAZI WASERIKALI NA WAFANYABIASHARA NAOMBA TUVUMILIE KWANI IMEBAKI MIAKA 8 TU.BAADA YA HAPO TUNARUDI KULA NA KUPIGA DILL KAMA ENZI ZA KIKWETE. SAFI SANA MAGUFURI


 
Watanzania tutaandana kuibadilisha katiba, watanzania ndo wenye katiba hivyo tutaibadili. Kama ataendelea na spidi hii au ataiongeza zaidi, tutaibadilisha katiba kwa ajili yake tu kisha tutairejesha atakapotaka kupumzika.
 
Mpinzani gani amemteua?
 
Wajua akitaka kuongezewa anawatuma wapambe wake wanaanzisha vugu vugu.....la kutaka aongezewe muda....baada hapo anapelekwa hoja bungeni.....!!! Ikipita amebadilisha katiba na yeye atasema wabunge na wananchi wamebadilisha katiba!!!!! Bado hajajibuhoja bado.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…