Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Hata mbowe alisema anaheshim Katiba na hato ongeza muda ila vijana tukamchukulia form so acha magufuli na yeye vijana wachange hela ili wamjazie fom
Mbowe anahusianaje na Urais wa Tanzania
 
Ni sawa lkn ikiwa kuna viashiria vya wizi basi tusizuie huo wizi kufanyika bali tusubiri wizi ufanyike halafu tulaumiane.Au tuanze kumtafuta mwizi ambaye taarifa na mipango yake ya wizi tulishaijua mapema.

Pili, nilicholeta si kumhukumu bali ni kutokana na movement inayoendelea. Kuna ubaya gani kusikia msimamo wake rasmi. Au unataka tuamini kuwa analazimishwa, kumlazimisha maana yake hataki. Na km hataki atoke hadharani na aseme sitaki na mjadala uishe.

 
Habari za jioni wanajamvi?

Ili kuwaelewa hawa watu wanao sema Rais Magufuli aongezewe muda lazima na wewe uwe certified fool. Unajua kwanini? Maana yake ni moja tu kuwa wamesha ona kuwa Maguli ameshinda uchaguzi 2025 na ameshinda tena 2030!!

Maana yake ni kwamba aidha watafuta mfumo Wa vyama vingi au wataimarisha kitengo cha wizi wa kura. Kwa kupigiwa kura na watanzania hawezi kupata hata 15% ya kura zote. Wakiamua kuiba au kupora uchaguzi wanatutafuta ubaya. Yaani hatutakubali kuwa wajinga mara mbili. Wanacho jivunia nasisi tutanunua ulaya. ONCE BITTEN TWICE SHY. Wakifuta vyama vingi sijui kama patakalika.
 
Habari za jioni wanajamvi?

Ili kuwaelewa hawa watu wanao sema Rais Magufuli aongezewe muda lazima na wewe uwe certified fool. Unajua kwanini? Maana yake ni moja tu kuwa wamesha ona kuwa Maguli ameshinda uchaguzi 2025 na ameshinda tena 2030!! Maana yake ni kwamba aidha watafuta mfumo Wa vyama vingi au wataimarisha kitengo cha wizi wa kura. Kwa kupigiwa kura na watanzania hawezi kupata hata 15% ya kura zote. Wakiamua kuiba au kupora uchaguzi wanatutafuta ubaya. Yaani hatutakubali kuwa wajinga mara mbili. Wanacho jivunia nasisi tutanunua ulaya. ONCE BITTEN TWICE SHY. Wakifuta vyama vingi sijui kama patakalika.
Unasema ww usitunzungumzie wengine bhn na kauli za uwingi uwe. Unaangalia mkuuuu
 
Actually siwahusishi certified foo l Najua Tanzania imejaa watu watu wenye akili timamu kuliko slow learners au to precise bendera fuata upepo.
Sio wote fool mkuu usichukulie kila mtu fool na usion nasema hvy uwez kusema hatutakubal sasa hapo umeongea wa au na ukiona utajibu vibaya kam hv kukataa kmya busara pia
 
Mamlaka ya serikali iko mikononi mwetu wananchi
Na Kura ndio zitaamua kama inafaa au haifai
 
Mbona hujui kuandika?
Umeona mam D alichojibu ety maamuz ya kutak kubaki yako mikonon mwa mwanach na sio ww
---+> sasa kuja na kusema hatutakubal umeingia kote katika vichwa vya watanzania ukaona wanafikiri kam ww
 
View attachment 1696487

Rais Magufuli akiwa Korogwe Tanga amesema hayuko tayari kuendelea kuongoza baada ya miaka 10 iliyowekwa kikatiba. Ameyasema haya baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Prof. Maji Marefu) kusema Rais anastahili kuongezwa muda ilia afanye mambo mengi zaidi.

Hii kauli imemaliza wasiwasi wa watu wote waliokuwa na speculation kuwa Rais anaweza kuongeza muda wa kukaa madarakani.
Kumbe ni kuheshimu katiba na siyo lazima
 
Rais Magufuli katiba yetu ya jmt inasema urais ni miaka kumi mwisho atakaeongeza zaidi ya hapo atapaswa kuchukuliwa Kama mhaini

Kuna watu wanakupigia debe uendelee kutawala hata baada ya miaka kumi kwisha tunaomba uwakemee kwa maana wanataka kulitikisa taifa kuna mtu anaitwa mkulima huyu anataka kulitikisa taifa akemewe vinginevyo itatafsirika unavunga ila kimsingi unautaka muda wa nyongeza nje ya katiba kwa lazima.

Pia Rais tambua kwamba watanzania tuko milioni hamsini na tano hivi kweli haya sio matusi ya wazi kwamba hakuna mtu mwingine zaidi yako Kati yetu milioni hamsini na tano?

Mh Rais legasi aliyoiacha mwalimu ya kung'atuka kwa hiari ndiyo iliyoiletea Tanzania heshima

Mwinyi hakuivunja
Mkapa hakuivunja
Jakaya hakuivunja

Wewe ukiivunja kumbuka moja utaharibu na kuchafua historia ya taifa letu lakini pili ikitokea nchi ikaingia matatizoni kwa jaribio hili la kung'ang'ania madaraka wewe ndio utawajibika moja kwa moja

Mh Rais umezungukwa na wanafiki wanaokuogopa na wanaonufaika na uwepo wako Hawa wote wanakuambia unayoyapenda na kutaka kuyasikia hawakuambii ukweli

Mh Rais wakina mkulima wanajua wako salama wakijipendekeza kwako maana kinyume chake Ni maangamizo kwao watu wanaojiita mataga Ni wanafiki wa kutupwa usiwasikilize hata wanaccm wanaoimba nyonjera za wewe kubaki wanatetea mradi wao sio kweli kwamba wewe unapendwa hapana wanakuogopa na kimsingi hawakuogopi wewe wanaiogopa dola kutekwa kupigwa risasi na kubambikiwa kesi.

Ushauri wangu kwako

Muda wako ukifika ondoka kwa heshima vinginevyo mchuma janga hula na wakwao !!

Nakutakia baraka amani na upendo viendelee kutawala katika moyo wako na taifa letu kwa ujumla !!

Wasalaam!
Mungu akubariki ulieandika hapa
 
Back
Top Bottom