Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Mkuu jamaa alishasema kuwa hana huo mpango sasa mbona mnakuja tena na kauli hizo hizo, pia mnaanza kutoa mifano ya kumchafua Imani za wenzenu kwa faida yako kiimani.
Je wale antbaraka kule Africa ya kati kanisa au wakiristu walijitokeza na kukemea kuwa hawahusiki wao?
Acha chuki mkuu.
Anachoongeaga kwenye media yule jamaa huwa hakifanani na anachokiwaza na kukiratibu kichwani mwake ameshawahi kuwaita wafanya biashara ikulu ili wasaidiane kumtafuta mchawi anaepelekea sector ya biashara kufa matokeo yake kawatoa sadaka maofisa kadhaa wa TRA ili ajisafishe yeye mchawi mkuu.Nasema ni mchawi mkuu kwa sababu ikizimwa camera anawapa maagizo na lengo kubwa la makusanyo hao hao TRA na vitisho juu then hao hao TRA wanarudi kutafuta lengo kwa wafanyabiashara kwa namna yoyote ikiwemo kuumiza watu na biashara zao alafu anajitokeza tena kwenye media kushangaa kwa nini TRA wananyanyasa wafanyaBiashara nchini.
""UELEKEO NI ZIMBABWE FUNGENI MKANDA WATANZANIA"Utamsikia akisema "WATANZANIA MNIOMBEE"
 
Ameshaongea mara nyingi,mbona mnakua wagumu kuamini...haongezi hata dakika moja...
 
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, ninamwomba Mh. Rais Magufuli atoke hadharani na atoe kauli kuhusu hili suala la watu wachache wenye maslahi binafsi kutaka kucheza na katiba yetu. Wakitaka aidha kuondoa ukomo wa muda wa uraisi au wakitaka kumwongezea muda wa kusalia madarakani.

Ikiwa MH Rais hayuko nyuma ya hili Jambo la kiwendawazimu na ikiwa anaiheshimu katiba aliyoapa kuilinda basi kwa heshima namwomba atoke hadharani rasmi na awakemee wote wanaosuka mpango huu. Tena wakijinadi kwamba watamlazimisha Mh.Rais.

My.Rais ukiiheshimu katiba na kipindi cha miaka yako kumi kikiisha ukaondoka,basi utaondoka kwa heshima iliyotukuka.

MH.Rais endapo hutatoka hadharani ukalizungumzia hili basi sisi wananchi tutaamini aidha uko nyuma ya mpango huu na kama hauko nyuma ya hili na hujawatuma Hawa watu basi tutaamini unapenda hili lifanyike.

Nb: Jambo ambalo nilikuwa silijui Ni kwamba kuna watu,mtu au kikundi cha watu kwa Nia zao nzuri au ovu wana uwezo wa kumlazimisha Rais atekekeze matakwa fulani tena apende au asipende. Na mpaka sasa hivi sijui hili limekaaje kikatiba au kisheria.

Nini mtazamo wako.
Hebu acha ujinga! Mie hata huyo Magu sijawahi kusogeleana naye km 5! Na sijawahi ongea naye ana kwa ana! Na kimsingi hajui hata kama nipo hapa duniani! Lakini sasa mimi nipo mstari wa mbele kabisa kindakindaki Magu apewe 👊👊 tena! Ucha mchecheto, Magu si ameshakataa hadharani, na sisi wenye mtazamo wa 👊👊 tena tutahakikisha tunambeba mzomzobe mpaka tutoboe 👊👊 tena! Wenye wivu kitanzi cha kuji'mkwawa' kinawahusu! Ova!
 
kama uchafuzi wa serikali za mitaa na ule uchafuzi mkuu wa 2020 ulinajisiwa kwa kiwango cha SGR wadadisi tumeshabaini nini kiko nyuma ya haya matamko ya walazamishaji...
 
Haya yote tuliyatarajia kuja kutokea. Sema tu hatukuwahi kuwaza kama yatakuja yatokee mapema kiasi hiki.

Naamini na yeye anapenda aendelee. Role model wake Mu 7 ameshafuta miaka 35! Na bado ameanza ngwe nyingine. Madaraka ni matamu sana bila shaka! Halafu inaonekana yanalevya sana.
Kagame ameshamuonaga huyu jamaa sio hata wa kukaa nae karibu.Kaunda ushosti na huyo mseven
 
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, ninamwomba Mh. Rais Magufuli atoke hadharani na atoe kauli kuhusu hili suala la watu wachache wenye maslahi binafsi kutaka kucheza na katiba yetu. Wakitaka aidha kuondoa ukomo wa muda wa uraisi au wakitaka kumwongezea muda wa kusalia madarakani.

Ikiwa MH Rais hayuko nyuma ya hili Jambo la kiwendawazimu na ikiwa anaiheshimu katiba aliyoapa kuilinda basi kwa heshima namwomba atoke hadharani rasmi na awakemee wote wanaosuka mpango huu. Tena wakijinadi kwamba watamlazimisha Mh.Rais.

My.Rais ukiiheshimu katiba na kipindi cha miaka yako kumi kikiisha ukaondoka,basi utaondoka kwa heshima iliyotukuka.

MH.Rais endapo hutatoka hadharani ukalizungumzia hili basi sisi wananchi tutaamini aidha uko nyuma ya mpango huu na kama hauko nyuma ya hili na hujawatuma Hawa watu basi tutaamini unapenda hili lifanyike.

Nb: Jambo ambalo nilikuwa silijui Ni kwamba kuna watu,mtu au kikundi cha watu kwa Nia zao nzuri au ovu wana uwezo wa kumlazimisha Rais atekekeze matakwa fulani tena apende au asipende. Na mpaka sasa hivi sijui hili limekaaje kikatiba au kisheria.

Nini mtazamo wako.
Anapima upepo. Narudia tena anapima upepo. Ndiyo maana kila akijitokeza hazungumzi kwa msisitizo na wala hajawahi kukemea hao washenzi wenye haya mawazo. Anapima upepo akiona upinzani umekuwa mkubwa na hawezi kutimiza ndoto yake basi aonekane kama hakuwa na hiyo nia. Marais wote wanaotaka kubaki madarakani huwa wanatumia hiyo njia.
 
This time NO.
Atatakiwa akabidhi nchi kwa mtu mwingine endapo atataka kufia madarakani, tambueni mrithi ajaye nae atataka kufia madarakani.
This time NO.
 
Watoto wengi mtaani kwetu wanajua huyo ndiye Rais hadi Mungu atakapoamua vinginevyo.
Sijui huu ujasiri wameutoa wapi
Huo mtaa lazima uwe Lumumba wa wajinga ingawa si wajinga, maana mtoto ni mtoto tu hata mtaa husika uwe London watoto hawatajua jina la huyo kiongozi wala Mungu ni nani ingawa wanakwenda kanisani kila Jumapili wao wanajua mwalimu tu kama wameanza shule. Mwulize mtoto mama yake anaitwa nani atajibu "mama" au mwalimu wake anaitwaje jibu ni "mwalimu", huyu kilaza anayetafuta uteuzi anatwambia watoto wa mtaa wake ni majasiri sana wanamjua Rais John Pombe Joseph Magufuli wanamwombea kwa Mungu atawale milele. MaCCM hayo, kesho tutasikia ameteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Geita!
 
Rais anaweza kuwa amefanya Kazi kubwa, lakini hata waliomtangulia walifanya Kazi kubwa kama yake au zaidi kutegemea mtazamo Wa MTU binafsi. Hivi J K aliyejenga barabara kilomita zaidi ya elfu saba za lami , akajenga shule za kata zaidi ya 3000. Akapandisha mishahara ya wafanyakazi kila mwaka, akakuza diplomasia ya nchi yetu hata Tz ikawa nyota duniani, kweli alifanya Kazi ndogo? . mbona hatukusikia aongezewe aongezwe? . Raid ameishatamka wazi hapendi kuongezewa. Ila wnaofaidi sana awamu hii ndiyo wameshika Bango aongezewe . kama sio kwamba wanatumwa sielewi. Of all the people Butiku nilimuheshimu sana , lakini Jana nimemtoa kwenye hesabu za kwenye busara. Eti hili jambo linaongeleka, I beg to differ with Butiku. Amenunuliwa na yeye eti Jana kavaa nguo ya kijani bluu afanane na wapiga debe Wa jpm. Tumaini limebaki kwa Warioba aliyesema , "ukiona katiba inabadilishwa ili kiongozi Fulani aongezewe muda basi ujue hiyo kiongozi ANAPENDA kuongeza muda wake". Neno tutamlazimisha ni nonsense huwezi kumlazimisha MTU mwenye madaraka yote nchini . Kikwete ameshakuwa RAIA Wa kawaida, mpira umebaki mikononi mwa JPM, akipenda ataongeza, akipenda ataachia kila kuna viashiria vya watu kutumwa naye wadai aongezewe. ila ajue kuwa wakulima na wafanyakazi wote huku chini wanaomba 2025 ifike aondoke. Hana jipya wala hata kuwa nalo maana na anayoyafanya ni sasa na MTU mwenye mshahara mdogo awalishe watoto dona na mchicha miaka 10 ili ajenge nyumba nzuri sawa na mwenye kipato kikubwa. Hatuwezi kumsifu kwa kujenga nyumba Bali tutamlaumu kwa kuidhki familia yake hadi wanapata utapia mlo. Kuna wajinga wanatoa mifano ya China na Russia eti viongozi wanaendelea kwa mapenzi ya watu, ni uongo. Russia Putin anaua wapinzani hadi kwa sumu ugenini. Na China aliua vijana 1990 pale Tian men ndio maana watu walinywea.hadi Leo . mbona hawatoi mfano wa India the largest democracy nao wametushinda kimaendeleo. Korea kusini kuna democracy, na hong Kong, na singapore zote zina democracy na bado zinapeta kimaendeleo. Imefika mahali mzee Butiku anatoa mfano Wa Merkel kuongoza miaka 16, this was joke. Merkel anaongoza serikali ya Muungano miaka yote kama katiba yai inavyoeleza, wale hawana winner take all. Msitumie uchovu Wa Tz kutojua international affairs kutudanganya wote haiwezekani ndio maana nimesema kuna viashiria vya kutumwa. Tumeishatambua mnatumwa. Mimi nasema JPM katimiza wajibu wake, come 2025 baba Wa watu apumzike kwa heshima kama waliomtangulia, tutamuenzi, kinyume cha hapo kunajisi katiba aliyoapa kuilinda ni ubatili kwake binafsi.
Hatuwezi kupoteza bahati ya kuwa na kiongozi mwadilifu na mcha Mungu eti kwa kuwa katiba itakiukwa wakati sisi ndio wenye mamlaka na katiba hiyo. Viongozi aina ya Magufuli si wa kuwaachia kirahisi, hawapatikani kwa urahisi!! Ukiona watu kama mzee Butiku wanaunga mkono hoja ujue kuna maslahi ya kitaifa hapo!
Mafisadi kama mlikuwa mnasubiri miaka kumi iishe, imekula kwenu!!
 
Tafadhali rais Magufuli usituangushe!! Usitukatalie, lazima tukuongezee muda Hadi nguvu zitakapokuishia!! Kwa Sasa wewe bado kijana sana!!
 
Huo mtaa lazima uwe Lumumba wa wajinga ingawa si wajinga, maana mtoto ni mtoto tu hata mtaa husika uwe London watoto hawatajua jina la huyo kiongozi wala Mungu ni nani ingawa wanakwenda kanisani kila Jumapili wao wanajua mwalimu tu kama wameanza shule. Mwulize mtoto mama yake anaitwa nani atajibu "mama" au mwalimu wake anaitwaje jibu ni "mwalimu", huyu kilaza anayetafuta uteuzi anatwambia watoto wa mtaa wake ni majasiri sana wanamjua Rais John Pombe Joseph Magufuli wanamwombea kwa Mungu atawale milele. MaCCM hayo, kesho tutasikia ameteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Geita!
Asante sana janja la mtaa. Inaonekana huko kwenu ndiye pekee mwenye maamuzi ya mwisho na hakuna anayekupinga.

Jambo dogo kama hilo (post yangu) umeshindwa kuelewa kweli?

Unatia huruma sana
 
Hatuwezi kupoteza bahati ya kuwa na kiongozi mwadilifu na mcha Mungu eti kwa kuwa katiba itakiukwa wakati sisi ndio wenye mamlaka na katiba hiyo. Viongozi aina ya Magufuli si wa kuwaachia kirahisi, hawapatikani kwa urahisi!! Ukiona watu kama mzee Butiku wanaunga mkono hoja ujue kuna maslahi ya kitaifa hapo!
Mafisadi kama mlikuwa mnasubiri miaka kumi iishe, imekula kwenu!!
Hakuna kiongozi muadilifu ananajisi box la kura, na kuendesha kundi la watu wasiojulikana.
 
Alihaidi ato ongeza ata sekunde atamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya nchi.
 
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, ninamwomba Mh. Rais Magufuli atoke hadharani na atoe kauli kuhusu hili suala la watu wachache wenye maslahi binafsi kutaka kucheza na katiba yetu. Wakitaka aidha kuondoa ukomo wa muda wa uraisi au wakitaka kumwongezea muda wa kusalia madarakani.

Ikiwa MH Rais hayuko nyuma ya hili Jambo la kiwendawazimu na ikiwa anaiheshimu katiba aliyoapa kuilinda basi kwa heshima namwomba atoke hadharani rasmi na awakemee wote wanaosuka mpango huu. Tena wakijinadi kwamba watamlazimisha Mh.Rais.

My.Rais ukiiheshimu katiba na kipindi cha miaka yako kumi kikiisha ukaondoka,basi utaondoka kwa heshima iliyotukuka.

MH.Rais endapo hutatoka hadharani ukalizungumzia hili basi sisi wananchi tutaamini aidha uko nyuma ya mpango huu na kama hauko nyuma ya hili na hujawatuma Hawa watu basi tutaamini unapenda hili lifanyike.

Nb: Jambo ambalo nilikuwa silijui Ni kwamba kuna watu,mtu au kikundi cha watu kwa Nia zao nzuri au ovu wana uwezo wa kumlazimisha Rais atekekeze matakwa fulani tena apende au asipende. Na mpaka sasa hivi sijui hili limekaaje kikatiba au kisheria.

Nini mtazamo wako.
Hilo jambo sio kwamba tu Mzee Meko yuko nyuma yake, yuko mbele na kati. Yeye ndiye designer and engineer wa mpango mzima.

Jipe muda ndugu utaona mambo.
 
Hata yeye alishasema akitoka hana uhakika kama reli itajengwa au bwawa la stigilazi. Sasa kwa akili yako unafikiri hao wamekurupuka? Hapo wanatafuta uhalali ionekane sio yeye anayetaka kubadili katiba. Tuwe wavumilivu muda utasema. Aibu kubwa hii sijui tutaificha wapi
 
Nb: Jambo ambalo nilikuwa silijui Ni kwamba kuna watu,mtu au kikundi cha watu kwa Nia zao nzuri au ovu wana uwezo wa kumlazimisha Rais atekekeze matakwa fulani tena apende au asipende. Na mpaka sasa hivi sijui hili limekaaje kikatiba au kisheria.[/QUOTE]

Hapa neno ndipo lilipo!

They call it survival of the fittest!

The world is a Jungle! You either fight or run forever!
 
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, ninamwomba Mh. Rais Magufuli atoke hadharani na atoe kauli kuhusu hili suala la watu wachache wenye maslahi binafsi kutaka kucheza na katiba yetu. Wakitaka aidha kuondoa ukomo wa muda wa uraisi au wakitaka kumwongezea muda wa kusalia madarakani.

Ikiwa MH Rais hayuko nyuma ya hili Jambo la kiwendawazimu na ikiwa anaiheshimu katiba aliyoapa kuilinda basi kwa heshima namwomba atoke hadharani rasmi na awakemee wote wanaosuka mpango huu. Tena wakijinadi kwamba watamlazimisha Mh.Rais.

My.Rais ukiiheshimu katiba na kipindi cha miaka yako kumi kikiisha ukaondoka,basi utaondoka kwa heshima iliyotukuka.

MH.Rais endapo hutatoka hadharani ukalizungumzia hili basi sisi wananchi tutaamini aidha uko nyuma ya mpango huu na kama hauko nyuma ya hili na hujawatuma Hawa watu basi tutaamini unapenda hili lifanyike.

Nb: Jambo ambalo nilikuwa silijui Ni kwamba kuna watu,mtu au kikundi cha watu kwa Nia zao nzuri au ovu wana uwezo wa kumlazimisha Rais atekekeze matakwa fulani tena apende au asipende. Na mpaka sasa hivi sijui hili limekaaje kikatiba au kisheria.

Nini mtazamo wako.
Magu amenogewa hataki kj kuondoka madarakani kama walivyo ndugu zake kagame na m7
 
Back
Top Bottom