Rais anaweza kuwa amefanya Kazi kubwa, lakini hata waliomtangulia walifanya Kazi kubwa kama yake au zaidi kutegemea mtazamo Wa MTU binafsi. Hivi J K aliyejenga barabara kilomita zaidi ya elfu saba za lami , akajenga shule za kata zaidi ya 3000. Akapandisha mishahara ya wafanyakazi kila mwaka, akakuza diplomasia ya nchi yetu hata Tz ikawa nyota duniani, kweli alifanya Kazi ndogo? . mbona hatukusikia aongezewe aongezwe? . Raid ameishatamka wazi hapendi kuongezewa. Ila wnaofaidi sana awamu hii ndiyo wameshika Bango aongezewe . kama sio kwamba wanatumwa sielewi. Of all the people Butiku nilimuheshimu sana , lakini Jana nimemtoa kwenye hesabu za kwenye busara. Eti hili jambo linaongeleka, I beg to differ with Butiku. Amenunuliwa na yeye eti Jana kavaa nguo ya kijani bluu afanane na wapiga debe Wa jpm. Tumaini limebaki kwa Warioba aliyesema , "ukiona katiba inabadilishwa ili kiongozi Fulani aongezewe muda basi ujue hiyo kiongozi ANAPENDA kuongeza muda wake". Neno tutamlazimisha ni nonsense huwezi kumlazimisha MTU mwenye madaraka yote nchini . Kikwete ameshakuwa RAIA Wa kawaida, mpira umebaki mikononi mwa JPM, akipenda ataongeza, akipenda ataachia kila kuna viashiria vya watu kutumwa naye wadai aongezewe. ila ajue kuwa wakulima na wafanyakazi wote huku chini wanaomba 2025 ifike aondoke. Hana jipya wala hata kuwa nalo maana na anayoyafanya ni sasa na MTU mwenye mshahara mdogo awalishe watoto dona na mchicha miaka 10 ili ajenge nyumba nzuri sawa na mwenye kipato kikubwa. Hatuwezi kumsifu kwa kujenga nyumba Bali tutamlaumu kwa kuidhki familia yake hadi wanapata utapia mlo. Kuna wajinga wanatoa mifano ya China na Russia eti viongozi wanaendelea kwa mapenzi ya watu, ni uongo. Russia Putin anaua wapinzani hadi kwa sumu ugenini. Na China aliua vijana 1990 pale Tian men ndio maana watu walinywea.hadi Leo . mbona hawatoi mfano wa India the largest democracy nao wametushinda kimaendeleo. Korea kusini kuna democracy, na hong Kong, na singapore zote zina democracy na bado zinapeta kimaendeleo. Imefika mahali mzee Butiku anatoa mfano Wa Merkel kuongoza miaka 16, this was joke. Merkel anaongoza serikali ya Muungano miaka yote kama katiba yai inavyoeleza, wale hawana winner take all. Msitumie uchovu Wa Tz kutojua international affairs kutudanganya wote haiwezekani ndio maana nimesema kuna viashiria vya kutumwa. Tumeishatambua mnatumwa. Mimi nasema JPM katimiza wajibu wake, come 2025 baba Wa watu apumzike kwa heshima kama waliomtangulia, tutamuenzi, kinyume cha hapo kunajisi katiba aliyoapa kuilinda ni ubatili kwake binafsi.