Rais Magufuli njoo vyuo vikuu ujionee. Manunuzi ya magari ni suala pana kuliko linavyotajwa mbele yako

Rais Magufuli njoo vyuo vikuu ujionee. Manunuzi ya magari ni suala pana kuliko linavyotajwa mbele yako

Huko Geita Mkurugenzi kasimamishwa kazi. Ni safi sana!! Sababu ziko wazi. Pesa za CSR haziwezi kuwa za gari la Mkurugenzi, wakati shule hospitali na madaraja ni hovyo. Mbaya zaidi ni gari la milioni 400! Tatizo hili liko kote! Hiyo ofisi ya waziri mkuu inayopitisha vibali kama hivyo ina udhaifu wa kudumu na ni sehemu ya rushwa za manunuzi.

Hata vyuo vikuu kila leo kuna magari ya kifahari yananunuliwa kwa ajili ya viongozi wakati vyuo hivi haviwezi hata kulipa pesa za likizo za wafanyakazi, hawawezi kuboresha mazingira ya kusomea, hawawezi kujenga nyumba za wanafunzi. Rais Magufuli, tembelea UD, tembelea SUA, nenda UDOM, Mzumbe, Muhimbili, kote kuna magari ya aina hii yamenunuliwa kwa kipindi hiki.

Kama vyuo vikuu wako hivyo, unategemea nini kwenye halmashauri kwa madiwani? Wakurugenzi hawa wamesoma vyuo hivi visivyojua nini muhimu kuliko kingine na rushwa zao. Ni vyuo hivi hivi vilivyokuwa vinaiba pesa za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo. Bahati mbaya sana, wanaachwa bila kuchukuliwa hatua. Hawa ndo wnaojenga tabia ya waajiliwa wa baadaye.
Kuna haja ya kutoa sera ya ununuzi wa magari kwa viongozi wa serikali ili tuachane na hizi V 8 turudi kwenye Landcruiser standard au prado za kawaida na wengine Suzuki. Iwekwe kwenye procurement regulations.
 
Hiyo CCM kabla ya Magufuli ilikuwa imeoza kwa tabia ya kubebana na matumizi mabaya.

Tena usituambie tena habari za CCM.
CCM kama CCM yenyewe bila mtu sahihi pale juu ni janga kwa taifa.
Ccm yote ni sawa tu.
Viongozi wake ndo walewale.
 
Tatizo Mh Rais huwa anashughulikia tatizo kwa kuangalia mtu au kikundi.

Alitakiwa ashughulikie tatizo hili kimfumo na siyo ki mtu au kisehemu.

Office iliyotumiwa ni office ya waziri mkuu, ambae ni msaidizi wake mkuu. Hatujasikia maelekezo ya hadharani kutoka kwake kama alivyotoa ya wafanyakazi wa TMAA na Mkurugenzi wa Geita.

Mi nadhani kuna double standard katika kushughulikia matatizo ya nchi hii.
No tatizo tunataka afanye yote mwenyewe.
Yeye ameshaonesha hajaridhishwa na ujinga huo. Ni lazima kuwe na trickling effect ya hasira za Rais sio lazima yeye mwenyewe aingie kila ofisi na kuanza kushughulikia watu.
 
Wakuu,
vipi yule katibu mwenezi wa CCM aliyekuwa anajisifia kwa viongozi wao wa chama kutumia V8 ametumbuliwa

CCM si kila kiongozi anatumia v8, kwanini wamsimamishe mkurugenzi?!
 
Ulipoanza na swali eti, 'sheria inasemaje?' nimekumbuka mila yetu ya mkubwa kula firigisi! Yaani wewe uone mtoto pembeni yako hana mboga bado useme mila yetu ni mkubwa kula firigisi! That will be rubbish!
Kwa ufupi ulichokumbushia ni kwamba watu ambao akili ni mbovu, ni hatari kwa maendeleo ya taasisi zetu. KIla wakati watasema Ofisi ya waziri mkuu ilitoa kibali!
Hahaaaa! Huu ndo mfano halisi, haswa!! Eti mtu anaangalia alichoruhusiwa kufanya kisheria au taratibu, halafu hakuna fikra ya ziada! Akiulizwa anasema tumefuata sheria na taratibu za serikali. Hapa ndo inafikia tuweke taratibu hata za jinsi ya kufikiria maana baadhi ya walio na madaraka ni watu wa kutupeleka shimoni tu!

Ubaya ni hii hali kwamba hata mtu wa elimu inayoitwa ya juu kuona uamuzi huo unamuongenzea jambo la ziada ktk maisha yake. Yaani pamoja na Ph.D! No wonder Darasa la saba la Musukuma sasa linapambanua kuliko hawa ma-profesa wetu.
 
Tunapambana na watu na siyo mfumo hilo ni kosa kubwa sana kwa maendeleo ya nchi...... Nchi zote zilizoendelea zilifanikiwa kutengeneza mifumo thabiti. Tanzania dira ya nchi ni kiongozi mkuu wa nchi na siyo mifumo. Belive me atakuja Rais atasema vipaumbele vyake ni Gas asilia wala siyo stigler's gorge ama SGR...... Tufike Mahali tujenge mifumo ambayo itaishi miaka 100...
 
Hapana! Tusitamani mfumo kila wakati. Hata iweje, tabia ya mtu ni jambo muhimu sana. Leo hii US wamejikuta wanalizwa na Trump. Pamoja na mfumo, sasa anaondoka akiwa maetia kovu kwenye jamii. Ameibua hata wanayoyaonea aibu!
 
Huko Geita Mkurugenzi kasimamishwa kazi. Ni safi sana! Sababu ziko wazi. Pesa za CSR haziwezi kuwa za gari la Mkurugenzi, wakati Shule, Hospitali na Madaraja ni hovyo. Mbaya zaidi ni gari la milioni 400! Tatizo hili liko kote! Hiyo ofisi ya waziri mkuu inayopitisha vibali kama hivyo ina udhaifu wa kudumu na ni sehemu ya rushwa za manunuzi.

Hata vyuo vikuu kila leo kuna magari ya kifahari yananunuliwa kwa ajili ya viongozi wakati vyuo hivi haviwezi hata kulipa pesa za likizo za wafanyakazi, hawawezi kuboresha mazingira ya kusomea, hawawezi kujenga nyumba za wanafunzi. Rais Magufuli, tembelea UD, tembelea SUA, nenda UDOM, Mzumbe, Muhimbili, kote kuna magari ya aina hii yamenunuliwa kwa kipindi hiki.

Kama vyuo vikuu wako hivyo, unategemea nini kwenye Halmashauri kwa madiwani? Wakurugenzi hawa wamesoma vyuo hivi visivyojua nini muhimu kuliko kingine na rushwa zao. Ni vyuo hivi hivi vilivyokuwa vinaiba pesa za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo. Bahati mbaya sana, wanaachwa bila kuchukuliwa hatua. Hawa ndo wnaojenga tabia ya waajiliwa wa baadaye.

Pale chuo kikuu Ardhi kuna GXR-V8 Brand New imenunuliwa this week na inagharimu si chini ya Mil.400.Inatumiwa na makamu Mkuu wa Chuo Prof Evaristi Joseph Liwa.

Huu hapa uchafu unaotendeka Chuo kikuu Ardhi.

1.Chuo kikuu Ardhi kina matatizo mengi mno ikiwemo madai lukuki ya watumishi wanaodai stahiki zao, wengine tangu mwaka 2013 mpaka leo lakini hakuna lolote linalofanywa kuwapa mahitaji yao japo kwa wakati.

2.Chuo kimeanzisha kampuni kwaajili ya kufanya za Ushauri wa kitaalamu kwa niaba ya Chuo, lakini huu ni mwaka wa pili haina audited Financial statements na hela zinapigwa haijawahi tokea.

3. Makamu Mkuu wa chuo anatumia rungu la kuwa karibu na vigogo wa Ikulu ili kuwafukuza ama kuwahamisha vituo vya kazi watumishi anaowaona ni threat kwenye maauala yake.

Mengine nitaandika jioni.
 
PALE CHUO KIKUU ARDHI KUNA GXR-V8 BRAND NEW IMENUNULIWA THIS WEEK NA INAGARIMU SIO CHINI YA MIL 400.INATUMIWA NA MAKAMU MKUU WA CHUO PROF EVARISTO JOSEPH LIWA.

HUU HAPA UCHAFU UNAOTENDEKA CHUO KIKUU ARDHI

1.CHUO KIKUU ARDHI KINA MATATIZO MENGI MNO IKIWEMO MADAI LUKUKI YA WATUMISHI WANADAI STAHIKI ZAO WENGINE TOKEA MWAKA 2013 MPAKA LEO LAKINI HAKUNA LOLOTE LINALOFANYWA KUWAPA MAHITAJI YAO JAPO KWA WAKATI.

2.CHUO KIMEANZISHA KAMPUNI KWA AJILI YA KUFANYA KAZI ZA USHAURI WA KITAALAMU KWA NIABA YA CHUO LAKINI HUU NI MWAKA WA PILI HAINA AUDITED FINANCIAL STATEMENTS NA HELA ZINAPIGWA HAIJAWAHI TOKEA.

3. MAKAMU MKUU WA CHUO ANATUMIA RUNGU LA KUWA KARIBU NA VIGOGO WA IKULU ILI KUWAFUKUZA AMA KUWAHAMISHA VITUO VYA KAZI WATUMISHI AMBAO ANAONA NI THREAT KWENYE MASUALA YAKE

MENGINE NTAYAANDIKA JIONI
Dah! Hiki ni kilio cha taasisi zote. Ktk majadiliano haya, binafsi nimeumia kusikia kwamba hata viongozi wa elimu ya juu wako hivyo hivyo sawa na wakurugenzi wa halmashauri. Viongozi wote wa vyuo ni maprofesa, nasema maprofesa, Watu ambao tungeweza kuamini wako kiwango cha juu cha uelewa kumbe hovyo tu!

Kuna mtindo wa kuhamisha watumishi wanaoonekana hawatakiwi taasisi fulani umekuwa ni kichaka cha uharifu. Ukiwauliza unaambiwa eti ni utaratibu wa kawaida lakini zipo taarifa nyingi za kiongozi akijisikia kupingwa maamuzi yake, anaamua kwenda utumishi kuomba uhamisho. Taarifa za ndani zinaonesha wanahonga viji-laki kadhaa na mtu anahamishwa.
 
Halafu cha ajabu wanazunguka nayo mijini tu. Wakipata kazi za kufanya utafiti wanatumia hayo hayo magari halafu wanajilipa mamilioni ya pesa.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Acheni Ndulane ashindwe kusoma kiapo, kuna mengi wanayoyakosa vyuoni.
 
Ipi ni sababu ya msingi ya DAS/RAS/DED/DC/RC kutumia magari yale ya kifahari?Kwani wakitumia 78 series hardtop kuna shida?

Serikali ingekua ina nia ya dhati ya kubana matumizi ingebadili sheria hizo za manunuzi lkn sababu tuna mapesa mengi acha tuendelee tu kutumia magari hayo ya kifahari.
Zipo sababu za msingi, na ndiyo maana si wote wanatumia magari ya aina hiyo. Vinginevyo magari hayo yasingekuwa yanatumika kabisa. Wahasibu kuna kitu wanaita opportunity cost. Nachelea kusema kuwa dhana hii ndiyo imewafanya wakaendelea kuyatumia mpaka leo, maana pengine waliona wakiyaondoa kabisa kwa kuogopa gharama ya fedha, wanaweza kuingia gharama nyingine tofauti ambayo si ya fedha, na ambayo ni kubwa mno kuzidi hata zile fedha ambazo waliogopa kuzitumia wakidhani kuwa wanabana matumizi. Swala nadhani liko zaidi kwenye usalama wa viongozi hasa pindi wanapokuwa wanasafiri hapa na pale kwa safari za masafa marefu. Hayo magari ambayo ni ghali, kwa upande mwingine yanaongoza kwa usalama kwa ruti za aina zote kuzidi magari mengine yoyote tuliyonayo hapa nchini, ambayo yanaweza kutumika kwenye ofisi zetu za umma
 
Kwa hiyo nawe umetumia akili kama yule Mkurugenzi, eti? Haya magari unaamini yana usalama zaidi? Yanatumia barabara zingine au hizi tunazopita na boda zetu? Yagigongana na Yutong yanawakumbatia wasife, eti?
 
Hakuna gari ambayo imetengenezwa perce kwa ajili ya kumkinga mtu asiumie kipindi inapotokea ajali, kwa sababu lengo la kutengeneza gari siyo ili zipate ajali. Gari zina uwezo fulani tu wa kumkinga abiria pindi inapotokea ajali, na uwezo huo unatofautiana kutoka gari moja hadi nyingine. Una umri gani?
 
Back
Top Bottom