Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Haijalishi sheria ipo kwa mbakaji ni miaka 30 jela.!
Mbakaji anafungwa, na mwanafunzi kama akipata ujauzito katika saga hilo la kubakwa anaadhibiwa kwa kutokurudishwa shule.!!!

Acha tucheke tu iko siku atatoa amri kuwa wanaopata ujauzito kwa kubakwa watolewe mimba hizo ili waendelee na shule!!
 
"Hata wanyama hawafanyi hivyo mbuzi Ng'ombe huwezi kuwaona wakikosea ile sehemu...Wachungaji si mpo hapa mmewahi kuwaona mbuzi wakikosea au ng'ombe wakikosea"..
Naona mzee leo kajiachia
 
Mashoga na wanaobaka vibinti vya shule ndiyo wanachukia hatua zote hizi anazozichukua rais Dr. Magufuli.

Ila mwanaume, aliyetimamu na anakula "K" ya mwanamke aliyetimiza umri wa kuolewa na asiye mwanafunzi wa shule za sekondari na za msingi hana tatizo kabisa na kauli kama hiyo.
 
Mashoga na wanaobaka vibinti vya shule ndiyo wanachukia hatua zote hizi anazozichukua rais Dr. Magufuli.

Ila mwanaume, aliyetimamu na anakula "K" ya mwanamke aliyetimiza umri wa kuolewa na asiye mwanafunzi wa shule za sekondari na za msingi hana tatizo kabisa na kauli kama hiyo.
Kwa hiyo wanaopinga kauli ya Mkuu ni wahusika wa uvunjaji wa sheria.?
 
Huyu jamaa aandikiwe hotuba, kumnyima mtu elimu ni kumkatalia haki yake ya kibinadamu yale maazimio tuliyosaini yatawabana watakaotekeleza huu ujinga.

Juzi kawaponza trafiki wawili.
Tangu zamani mwanafunzi akipata ujauzito alikuwa akikatisha masomo. Sasa leo kusemwa na JPM ndiyo inakuwa isdue? Au wewe una mimba tayari?
 
Kuna binti alipata ujauzito akiwa form 2 miaka ya nyuma kidogo.. akajifungua salama mtoto akawa mwaka moja kasoro wazazi wake wakapambana akarudi shule.. leo hii ni Mwalimu mshahara analipwa na anawasaidia watu wengine wakiwemo wazazi wake na serikali inakata kodi kama kawaida

Magu kwa upande wa vision hamna kabisa anajenga taifa la omba omba

One In a million huyo ukweli usemwe tu Nchi itoe Tangazo kuwa atakaepata mimba arudi shule wanafunzi watasoma kweli? ukijua saikolojia ya watu walio katika mobb maamuzi kama hayo ya kuwaruhusu ni sawa kumfunga mfugo katika shamba la mazao!! Naomba nikuulize ile ishu ya mbeya day iliishaje baada ya wale wanafunzi kutetewa sana na ukweli ulipojulikana ni hatua zipi zilichukuliwa??

Tanzania lazima ibaki katika misingi yake kulinda maadili yanayoporomoka kila siku leo mnapiga kelele kwa huyu inaonekana mmesahau kauli ya "viherehere vyao" ya mtangulizi wake yote ni katika kusaidia kizazi cha watanzania na si kuendekeza mambo yasiyo na maadili kama hayo.

Kesi za kubakwa naamini zinaripotiwa katika maeneo husika na mwanafunzi kama huyo sidhani kama kuna kosa la kuendelea na shule kama kweli atathibitika alibakwa. Lakini si kuruhusu watu wa do na wapate mimba then warudi shule Hilo HAPANA.
 
Mambo mengine bana.najiuliza hivi kwani kupata mimba ukiwa shule ndo mwisho wa maisha.au shule kwake ni nini.alafu anaongelea shule gani hizo,au hizi shule za watoto wanazoenda na mafagio na vidumu,au uko sekondari ambako mabint wanakosa ata taulo zakujisitiri wakisafiri safar ya mbali.Hizi ambazo wanafunzi wanatembea makilometa kwenda nakurud shule.Hiv hajui changamoto na vishawishi wanavyokutana nao hawa wanafunzi wa kike.Maswali ni mengi kuliko majibu,ila labda tuseme ametania tu kama ambavyo tuliambiwa kipindi kile cha kufyatua watoto.
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.

" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.
Since time in memorial wanafunzi wa kike wamekuwa wakipata mimba na baadhi yako kupata nafasi ya kuendelea na masomo. Wako ambao hupata mimba kutokana na maadili mabovu. Wako ambao hubakwa. Wako ambao hudanganywa na wanaume washenzi. Lakini pia wako wale viherehere. Kama kuna uwezekano wa kuwasomesha na wenyewe wako radhi kuendelea na masomo wasinyanyapaliwe.
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
100% nakubaliana na pombe joseph, swala la mimba mashuleni likiachwa kama hizi NGOs zinataka hakika wanafunzi watakua wanamaliza std 7 nusu wana vibendi
 
Nataka niwaambie hawa ngo's Na taasisi nyenginezo... Katika utawala wangu mwanafunzi atakaye pata ujauzito akiwa shuleni ( kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ) Hakuna ruhusa kwa mwanafunzi huyo kuendelea na masomo baada ya kujifungua..

"NATAKA NISEME, KATIKA UTAWALA WANGU HAKUTAKUWA NA KITU KAMA HICHO "
 
Watoto wetu wana bahati mbaya na marais wetu. Mmoja alisema wana 'kiherehere', mwingine anasema hasomeshi 'wazazi'.
 
Back
Top Bottom