Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

IMG-20170622-WA0006.jpg
 
Kuna wengine wametuletea mambo ya kubakana, sijui wanaume kwa wanaume, hivi ushawahi kuona Mbuzi anakosea ile sehemu - JPM [HASHTAG]#MagufuliPwani[/HASHTAG].
tmp_14747-IMG-20170622-WA0044245787482.jpg
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa. Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu. Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Wewe ndiyo umekosea. Ukisharuhusu huo ujinga bas ndo unahamasisha mapenzi shuleni na utapata matukio mengi sana ya watu kuzaa na kuomba kurudi shule. Mtu anayependa kuzaa azae na aendelee kuwa mama huko mtaani maana ndo alichochagua badala ya elimu.

Haya mambo ukwel tukiyakubali yatatuletea shida sana kwenye malezi hata wazazi. Ulaya binti analeta mwanaume ndani ya nyumba nyumbani kwao na analala naye eti ni haki yake, matokeo yake ni mimba na mwisho wa siku eti bahati mbaya aachwe arudi shule.

Ndo mchezo wanaoenda kutuletea. Kila kitu haki haki haki hata mijianaume kulalana eti haki. Hizi haki za kijinga zikizidi kuruhusiwa mwishowe itakuwa hapakaliki
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Yuko sahihi 100% ...hii itawafanya watoto wa kike wajitambue sio kugawagawa tu.....wazae...warudi shule mtoto kakua
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Hujamuelewa mkuu, hapa anamaanisha kuwa kama mtu anapesa yake aende private lakini siyo serikali ikusomeshe bure halafu ulete ujinga, nchi hii inawatoto wengi Wanaotaka kusoma.
 
Saf sana mkuu wa nchi,manake kuna watu wanahamasisha upuuz,..kwanin mwanafunz apate mimba? Hizo ishu za kubakwa sjui nin,ni special case,la sivyo hakuna shule ukipata mimba
 
Mheshimiwa rais hajafunga milango ya watoto wanaopata mimba kupata elimu,wanaweza kwenda private lakini hayupo tayari kutumia fedha za umma kugharimia elimu yao kwa kuwa fursa yakulipiwa watakuwa wameipoteza wenyewe kwa kupenda mapenzi kuliko shule
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Mtakatifu huwa hapotoki na unatakiwa kukubaliana naye katika kila jambo!
 
Ni bora wakatafute shughuli nyengine za kufanya, ni bora wakajifunze ufundi stadi VETA, au wakajifunze ufundi wa kushona nguo [emoji4]
 
Unafiki, hujaelewa nini? Jifunze kujua hulka za mkulu!
 
Back
Top Bottom