Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Huku ni kunyimana Elimu, viongozi wasioweza kufikiria, Yeye Magufuli kama Mzazi mwenye mtoto wa kike atajionaje pindi binti yake atakapopata mimba na kuambiwa haruhusiwi kusoma tena? Hii Sheria ya kipuuzi zinawahusu walalahoi wasio na pesa za kuwasomesha watoto wao wakike, lakini ukiwa na pesa binti yako atasoma popote pale katika dunia hii.

Elimu yenyewe ipo chini halafu bado mnawanyima watoto wa kike elimu kwa kisingizio cha mimba. Badala ya kufikiri jinsi gani ya kuwasaidia wasipate ujauzito wanapokuwa masomoni nyie wapuuzi mnafikira jinsi gani ya kuwanyima haki zao za kupata elimu.

Mlaaniwe viongozi wenye maneno ya kipuuzi kama haya
 
Mwaka Huu Tutapiga Sana Kelele

Waiter Zungusha Tena[emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482]
 
Wananchi kumsifia sana kumempa kiburi siku hizi anatema ugoro.
Yaani kafananisha wadada wenye mimba na mashoga? Alafu anajua vizuri akishaleta neno ushoga kwenye jamii ya watanzania atapewa pongezi kubwa maana sijawahi ona watu homophobic kama wabongo.

NGOs anazionea tu, NGO haikufanyi shoga, labda angeongelea sababu nyingine. Kama mtu aliye juu namna hii kichwa kipo hivi basi njia bado ni ndefu zaidi ya tunavyofikiria.

I'm so done with this guy, ana mdomo mbaya sijawahi pata kuona.
Mwambie Lissu akutetee basi
 
Inakuwaje pale Binti mwanafunzi akapata mimba baada ya kubakwa!!

Changamoto hiyo.

Tatizo ukiruhusu waliobakwa warudi shule hata wale waliofanya kwa kuamua wenyewe watasingizia kubakwa ili nao warudi shule.
 
Kadiri anavyozidi kuombewa ndivyo anavyozidi kuchanganyikiwa na kuharibu..
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.

Amesema mtasomeshwa na NGOs
 
Iko sahihi kabisa iyo kauli,nyie mlitegemea awaambie mkipata mimba mjifungue mrudi shule heeee!!
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!


[HASHTAG]#Nilimsikiliza[/HASHTAG] hotuba yote nikafurahi sana. Magufuli seems to know the tools of analysis. Tena kawachamba hawa maNGO wanaopotosha maadili ya taifa hili kwa wimbo wa haki za binadamu.
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.
haki inamipaka na wajibu!
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
Kama maadili yenyewe ni hovyo kama kuzuia watoto w maskini wasipate elimu kwa faida yao hata baada ya kujifungua, hamna haja ya kuwa maadili "yetu"" maana wewe na rais wako hamtapata chochote iwapo hivyo visichana vitasoma au havitasoma
 
Inakuwaje pale Binti mwanafunzi akapata mimba baada ya kubakwa!!

kama umebakwa sheria za nchi zipo aliyebaka ataenda jela., aliyebakwa tutampeleka shule za wazazi ambaz zitaanzishwa ni NGOs.
 
Kwani kuna tafauti gani kumfundisha mwanafunzi mzazi na mwanafunzi wakawaida?
Kwani kuna tatizo gani mwanafunzi mzazi kumuomba mwalimu ruksa kwenda kumyonyesha mtoto wake? au serikali itapungukiwa nanini katika mpango wake wa elimu bure? Je hao wanafunzi wazazi ikiwa niwazuri kwa masomo ya sayansi nahesabu, watakapo fukuzwa lengo la taifa kufanikisha kupata mainjinyia, madokta na wahasibu ambae ni wachache litafanikiwa? Mbona ulaya na marekani mambo hayapo hivyo?
Kumbe akili yako huko ndipo inapowaza , kwamba uwezo wako wa kufikiri na kuchambua mada umeishia hapo?

Hujajiuliza madhara yatakayotokea mashuleni baada ya kuruhusu kurudi shule kwa mwanafunzi aliyepata mimba?
 
Back
Top Bottom