Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Haya maneno kayatoa kwenye kuruani. Yani huyo anafundisha kuruani sijui kwanini kamuonyesha hayo maneno.
 
Sawa sawa....
.
.nakupingaga sana mzee ila katika hili tupo pamoja ,
.
.wazaz watengeneze mazngra mazur kwa watoto kusoma...
.
.ufatiliaj uongezeke ,
.
.sio kuwaachia walimu tu...
.
.hv ni ushawah kujiulza ni kwann wanaopata mimba wakiwa shulen wengu huwa ni wa shule za serikari?? Kwann sio private ????
Mkuu hilo ni swali au ushajijibu mwenyewe?Mazingira yasiyo rafiki ya kusomea haswa shule za kata za kutwa.
 
Mimi namsapoti katika hii issue...watoto wa siku ukiwachekea utapata tabu sana.
 
Mwenyewe siafiki mwanafunzi wa kike kuzaa na arejee shule, labda ajisomeshe private, kuruhusu haya ni kuwaambia zaeni, fanyeni ngono muwezavyo maana mkipata ujauzito mtarejea shule, hapo ndio na maradhi yatazidi kushamiri...hapana na kidume atakaempa mwanafunzi ujauzito asibaki salama
 
Kama ndiyo hiyo ya Mama Kikwete. Yeye Mama Kikwete alisema wasirudi shule yaani hata leo Mama Kikwete amekumbusha kuwa hata bungeni alikataa hiyo habari ya watoto wa kike kupata mimba, mara wajifungue kisha shule.
Huyo rohoni atakuwa anaumia tu
 
Mwalimu Nyerere na Elimu


Mwalimu Julius Nyerere alikuwa mwalimu. Naamini ni sahihi kusema kuwa silika ya ualimu iliathiri siasa na matendo ya Mwalimu Nyerere kama kiongozi wa Tanganyika na hatimaye Tanzania. Aliiona nchi yake kama darasa, na daima alikuwa anafundisha.

Ninachotaka kuongelea hapa ni mchango wa Mwalimu Nyerere katika uwanja wa elimu. Elimu ni suala mojawapo ambalo Mwalimu Nyerere alilishughulikia sana. Katika kuelezea suala la elimu, Mwalimu aliweka na kufuata misingi kadhaa muhimu.

Tanganyika ilipopata Uhuru, Mwalimu Nyerere alikuwa ameshajizatiti kubadilisha mfumo wa elimu uliokuwepo wakati wa ukoloni, ambao ulikuwa mfumo wa kibaguzi. Kulikuwa na shule za wazungu, za Wahindi, na za watu weusi. Mara tulipopata Uhuru, Nyerere alifuta ubaguzi na kuwachanganya wanafunzi mashuleni. Tangu mwanzo, Mwalimu Nyerere aliamini dhana ya usawa wa binadamu.

Mwalimu Nyerere aliamini kuwa elimu ni haki ya kila mtu. Alifanya kila juhudi kutoa elimu kwa watu wote, kuanzia watoto hadi watu wazima. Mwalimu alijitahidi kujenga mfumo wa elimu ambao ulitoa nafasi kwa yeyote kutokana na uwezo wa akili yake, bila kujali kama alikuwa maskini au tajiri. Kwa msingi huu, watu wengi ambao hawangeweza kulipia masomo walisoma hadi vyuo vikuu.

Mwalimu Nyerere alitaka elimu iwe inamjenga mwanafunzi kuwa mdadisi wa mambo na mwenye kiu ya kutafuta elimu. Yeye mwenyewe alikuwa mwanafalsafa, mtu wa kutafakari mambo. Na hivyo ndivyo alivyotaka elimu iwe. Mwalimu alitaka elimu iwe nyenzo ya kumkomboa mwanadamu, tofauti na elimu ya kikoloni, ambayo ilikuwa inaendeleza fikra tegemezi, fikra za kujidhalilisha, fikra za kitumwa. Alitaka elimu ijenge tabia ya kuheshimiana, sio kiburi cha usomi.

Mwalimu Nyerere alitaka elimu ijumlishe nadharia na vitendo, na ijenge tabia ya kushirikiana, si kushindana na ubinafsi. Vijana mashuleni alitaka wawe pia wanajishughulisha na kazi za mikono, kama vile kulima au kufuga na useremala. Hii nayo ni elimu, na ni fursa ya kufahamu mengi ambayo hayapatikani darasani. Kazi za mikono aliziona ni njia moja ya shule kujenga msingi wa kujitegemea kwa mahitaji yake.

Mwalimu Nyerere alifundisha kuwa elimu haina mwisho. Aliwahimiza watu kujibidisha katika kutafuta elimu. Mbali ya kushughulikia elimu ya watoto na vijana mashuleni, alianzisha mpango wa elimu ya watu wazima. Vijijini na mijini watu walihimizwa na walipata fursa ya kujiongezea elimu, kuanzia kujifunza kusoma na kuandika hadi kujipatia ujuzi na maarifa katika fani na taaluma mbali mbali.

Kwa utaratibu ulioitwa kisomo chenye manufaa, wavuvi, wakulima, seremala, wafugaji, na wengine katika shughuli mbali mbali, walihimizwa kujiongezea ujuzi kwenye fani na shughuli zao. Vitabu vilichapishwa katika fani za aina aina, ambavyo viliwapa watu fursa ya kujifunza kusoma na pia kujiongezea maarifa na ujuzi.

Kama Watanzania tungefuata mawazo ya Mwalimu, leo tungekuwa mbali kimaendeleo, na tungekuwa na mategemeo ya kufanikiwa zaidi. Katika dunia ya leo ya utandawazi, elimu, ujuzi na maarifa ndio msingi wa mafanikio. Lakini, Tanzania tuna matatizo makubwa, kwani ari ya kujielimisha imepungua sana, na watu wanatafuta vyeti badala ya elimu. Wengi wanaamini kuwa njia ya mafanikio ni kutumia mambo ya ushirikina, badala ya kujiongezea maarifa katika fani na shughuli mbali mbali, iwe ni kilimo, uvuvi, au biashara.

Nimeona jinsi Wamarekani wanavyojali elimu. Wanatumia fedha kununua vitabu, kulipia semina, na fursa nyingine kadha wa kadha za kujiongezea elimu, ujuzi na maarifa, ili wapate mafanikio katika shughuli zao, kama vile biashara. Watanzania tungekuwa tumefuata nyayo za Mwalimu Nyerere tungefanya hivyo hivyo: tungeona umuhimu wa kutumia fedha kununulia vitabu na kulipia warsha za kujiongezea ujuzi na maarifa katika shughuli mbali mbali. Imani ya kuwa maendeleo na mafanikio yanatokana na mambo ya kishirikina ni dalili za kuanguka kwa ule msingi aliokuwa anaujenga Mwalimu Nyerere. Je, Watanzania tutaweza kushindana katika dunia ya leo na kufanikiwa bila elimu, ujuzi na maarifa? Hilo wimbi la ushindani wa kimataifa tutaliweza au litatuzamisha? Hilo ni suala la kulitafakari.

Kuufahamu mchango wa Mwalimu Nyerere katika elimu ni sherti kuyapitia maandishi yake na hotuba zake. Baadhi ya maandisho hayo na hotuba hizo zilihusu elimu moja kwa moja, na baadhi ya kazi zake hizo ni hazina ambayo inatuwezesha kukusanya dondoo mbali mbali za kutuwezesha kuielewa falsafa na sera ya Mwalimu Nyerere kuhusu elimu. Kwa bahati nzuri, kuna kitabu kimechapishwa, kinachokusanya maandishi muhimu ya Mwalimu Nyerere kuhusu elimu. KinaitwaNyerere on Education/ Nyerere Kuhusu Elimu.
 
Duuhhhh
Hii hatari.
Sitaki kuamini Magu anaakili finyu kiasi
Hiki. Kwa hili siungi mkono kabisa linatisha.

Badala ya kuwaza TZ miaka kumi ijiyo yeye anawaza sasa. Hili sio jambo dogo Lita gharimu taifa zaidi ya anavyowaza.
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Huyu bwanamkubwa anataka kutengeneza taifa la wajinga,kukosesha elimu akina dada wanaolea vijana wa taifa la kesho ni sawa na kutengeneza taifa la mazombi....Mungu ibariki Tanzania na watu wake
 
Ni vigumu sana kujua upendo na uchungu wa mzazi kwa watoto kama wewe mwenyewe si mzazi.

Kwa hiyo, ukiwa mzazi ndiyo ufurahie hivyo vitoto vya chekechea kufunguwa duka lao la kitumbua kwenye wapita njia eeeeh.

Frankly speaking, for this decision, Iam standing with President, Dr. Magufuli.

Period.
 
Hahahahahah
Critical thinking is better than argumentation!!
No body is fighting with anybody ideologically.. What you have to do is to THINK be for you argue!!!

Tafsiri ya kisheria ni kwamba mwanafunzi akipata mimba amebakwa!!!
Na adhabu yake Ni kifungo kisichopungua miaka 30 jela.

Kama Ni hivyo unawezaje kumwita mtu aliebakwa immoral!!?

Nakama hoja Ni maadili Na yakwamba waschana woote wanaopata mimba Ni umalaya hivyo kurudi shule Ni kuendekeza utovu wa nidhamu Na uvunjifu wa maadili mema..

Kwanini tusianze Na kufuta Sheria ya SOSPA!!!
Na wafungwa woote waachiliwe huru mana hawakubaka isipokuwa walijipatia uroda kwa Malaya!!
Unatongozwa unakubali kwenda guest halafu eti umebakwa!Hivi unahitaji akili sana kweli kujua kwamba that is not correct.Halafu sheria unazozungumzia mkuu zimetungwa ili kuhalalisha upuuzi.In fact to me they are unacceptable. Naamini hizi hizi NGOs ndizo zimepelekea kutunga sheria hizi za hovyo.
 
Majira ni mbaya sana usizuie ujauzito wakati hujui kizazichako kipovip...anaeruhusiwa kutumia ni yule aliezaa tu.
Ma adolecents wa kizungu wanatumia ,na baadae wanakuja kuzaa tu,sema wao wanakuwa prescribed kabisa na Dr baada ya kupimwa damu na Dr kujua ni majira yapi yatamfaa.
 
..Rais anadai haezi fundisha student mwenye yuko na mimba,sasa naulizaJe..kwani hizo pesa ni zakwake ama ni zile Kodi za waraia..
 
Kwa hiyo, ukiwa mzazi ndiyo ufurahie hivyo vitoto vya chekechea kufunguwa duka lao la kitumbua kwenye wapita njia eeeeh.

Frankly speaking, for this decision, Iam standing with President, Dr. Magufuli.

Period.
Mkuu ni haki yako kuwa upande uupendao, ila suala hili linasababishwa na muingiliano wa sababu nyingi sana na linahitaji hekima na busara kulishughulikia kwa manufaa ya pande zote. Shule za kata zina matatizo lukuki yanayopelekea mimba kwa wanafunzi, elimu duni ya afya ya uzazi na sababu zinginezo ni lazima zitafutiwe ufumbuzi. Sisi walimu wa miaka mingi huku vijijini tunayaona na tunajua uhalisia wake, so mkuu atafakari na aache kauli za namna hiyo.
 
Duuhhhh
Hii hatari.
Sitaki kuamini Magu anaakili finyu kiasi
Hiki. Kwa hili siungi mkono kabisa linatisha.

Badala ya kuwaza TZ miaka kumi ijiyo yeye anawaza sasa. Hili sio jambo dogo Lita gharimu taifa zaidi ya anavyowaza.


Acha kutisha watu.

Kama hao, wasichana hawana vipaumbele kwenye maisha hapo mbeleni si ndiyo watatusababishia nchi kuingia gharama wakisha kuwa na nafasi, maamuzi yao yote yatakuwa ya kutokuwa na vipaumbele!!

Priorities in life, is a key to success and not a combination of assumptions!!
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Ulitaka aseme wanafunzi wa kike wakipata mimba waendelee kusoma alafu awe anachochea ngono? Hiyo speech ni total deterrence. Big up sana your Excellency Mr John
 
Huu ndio mtazamo wa rais wetu,ila sidhani kama amekaa chini na washauri wake na kuja na kitu au makubaliano kama haya.
 
Back
Top Bottom