Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Namkubali sana Magufuli, yaani hawa ndio viongozi tuliomsubiri kwa mda mrefu. anapokosea ni sehemu ndogo tu naimani nayo itakaa poa mda si mrefu... na watz tutakuwa tunachekelea tu..
 
Wengi wanaounga mkono hii kauli bila shaka hawajaoa na kuwa na watoto.
tumeoa na tuna watoto , wengi mnaopinga hii kauli inaonesha ni wazinzi sana na mnampango wenu ni kuchochea uzinzi mashuleni.

huku wanafunzi watakaa wakijua wakipata tu bahati mbaya wanaleta mtoto kwa bibi afu anarudi shule kama kawa.
tumuunge mheshimiwa watoto waogope kuvuliavulia chpi wanaume waangalie masomo.
 
Katika hili naunga mkono mtazamo wa Mkuu kwani ametoa pia alternative solution kuwa kuna elimu mbadala ambayo anaweza kufuata kama kuelekea VETA, QT nk. kimsingi hataki kuhalalisha hilo ili na wengine waone ni kawaida. kwa wanaobakwa ni muhimu watendaji na jamii kuangalia namna ya kuliondoa tatizo la ubakaji na tayari adhabu yake ni miaka 30 inajulikana....Wengine wanahoji wale wanaowapa mimba hawajaguswa ...la hasha amesema wanaowapa mimba wawe ndani ya shule au nje ya shule adhabu yao ni miaka 30 iko wazi. Tatizo umma unataka kulifanya suala la mimba kwa wanafunzi liwe la kawaida...hapana litamomonyoa maadili na kuchangia kuongeza vifo vya wazazi nk.
 
Umri sahihi wa mwanamke kuzaa ni anapokuwa na ukomavu wa kimwili na kiakili. Rais hajatunga sheria au kanuni mpya, zilikuwepo. Kakumbushia tu. Tuwahimize watoto kusoma, sio kuzaa. Wanafunzi waliozaa wakalee watoto wao. Wasiwanyime haki ya kunyonya miaka 2 na kupelekwa clinic miaka 5.
 
Angekuwa Ni binti yake angefanyaje, hiyo ni kumkomoa nani kumnyima huyu binti elimu? Sio kumwangamiza yeye na huyo Mwanaye na Kumfanya Mzigo wa Kudumu kwa Familia na Kwa Taifa?
Je ni waalimu, Madaktari wangapi, Viongozi wangapi wa kitaifa walipata mimba wakiwa wanafunzi na Bado wakaendelea na Masomo na sasa ni msaada kwao kwa familia na Taifa!

Mbaya zaidi hii kauli ya Kiburi na kijinga, ati sitasomesha "wazazi" ni kauli ya kiburi kanakwamba fedha za Serikali zitumikazo kwa ajili ya Elimu ni Ruzuku kutoka kwa Mama yake Magufuli au pesa zake za biashara ya sangara! Hana unyenyekevu wa kuona kuwa ni fedha za Walopa kodi wakiwemo wazazi wa hao mabinti, au kama sio kodi basi zinatokana na Raslimaliza taifa au mikopo ambayo jasho za kuilipa litatokana na Watanzania wakiwemo wazazi wa hawa mabinti.

Nilishasema Magufuli na Makonda akili zao zinafanana! Kama atabisha nitashangaa sana sio kidogo!
 
Katika hili naunga mkono mtazamo wa Mkuu kwani ametoa pia alternative solution kuwa kuna elimu mbadala ambayo anaweza kufuata kama kuelekea VETA, QT nk. kimsingi hataki kuhalalisha hilo ili na wengine waone ni kawaida. kwa wanaobakwa ni muhimu watendaji na jamii kuangalia namna ya kuliondoa tatizo la ubakaji na tayari adhabu yake ni miaka 30 inajulikana....Wengine wanahoji wale wanaowapa mimba hawajaguswa ...la hasha amesema wanaowapa mimba wawe ndani ya shule au nje ya shule adhabu yao ni miaka 30 iko wazi. Tatizo umma unataka kulifanya suala la mimba kwa wanafunzi liwe la kawaida...hapana litamomonyoa maadili na kuchangia kuongeza vifo vya wazazi nk.

Kama nani Apangie Watoto wa wengine wasome wapi?
 
Binafsi nafikiri kumpinga JPM kwenye hili ni kumwonea. Hili analosema liko kwenye Sheria ya Elimu ya 1978 na marekebisho yake mbalimbali 1995 na 2002.
Tatizo ni namna alivyolisemea lakini kisheria yuko sawa.
Kwa kawaida mtoto wa kike kupata mimba ni ushahidi kuwa amefanya ngono ambayo ni utovu mkubwa wa nidhamu katika kanuni za shule.
Kitu kinachopaswa kwa wanaharakati na wabunge ni kushinikiza sheria ibadilishwe badala ya kumlaumu JPM..
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Hivi raisi anajua the term "second chance"? Unataka kuniambia katika maisha yake hajawahi kupewa second chance? Hii mimi nadhani busara itumike. Ujauzito sio kwamba ni mwisho wa ndoto za wasichana walio wengi wanaotaka kujiendeleza ki maisha. Wengi unakuta wanapewa mimba na walimu na watu wengine ambao wao hawapewi adhabu. Hii kwa kweli sio sawa. Kama sote tusingepewa second chance no one will be here.
 
tumeoa na tuna watoto , wengi mnaopinga hii kauli inaonesha ni wazinzi sana na mnampango wenu ni kuchochea uzinzi mashuleni.

huku wanafunzi watakaa wakijua wakipata tu bahati mbaya wanaleta mtoto kwa bibi afu anarudi shule kama kawa.
tumuunge mheshimiwa watoto waogope kuvuliavulia chpi wanaume waangalie masomo.
Hawa wanaompinga wao wanasema tu haki ya mwanafunzi kusoma bila kusema wajibu wake ni nini.
Pia hawasemi huyo mtoto atakae zaliwa yeye hawasemi atakuwa na haki zipi na atazipata vipi bila mama.
Hawa ndio baadae wanakuja na NGOS nyingine za kutaka serikali iwalishe
 
People will always have sex - religion or no religion, legal or illegal, underage, marital or extra marital - you name it. Girls/women will always get pregnant as adults or underage - we can't and shouldn't penalise them for that. When we deny girls education, they will not value it in the lives of their children too and we'll in turn create a generation that is illiterate and dependent. Having an illiterate generation has multiplier effects in areas such as poor health, malnutrition, high maternal and infant mortality, low accessibility to credit facilities etc. Jailing the men, or threatening them with 30 years jail term will not stop people from desiring to have sex, that's nature in control.
 
cjutegemea kama wengi wenu umu ndani mtasupport haya maneno aliyoongea uyu magu!!!kumbukeni c wte ni wazazi na kama sio mzazi utakuja pita tu kwenye uzazi!!tunayemzungumzia hapa mkae muelewe ni msichana wa kuanzia darasa la 5 na kuendelea hadi secondary!!wengi walio hapa ni chini ya miaka 18,kiujumla wengi wao bado hawajajitambua na vigumu sana kukwepa vishawishi kutokana na umri wao,wengi wao wanashawishiwa na kurubuniwa bila kujitambua!!!na ndio maana sheria inamkaba mwanaume sbb anakua kama amembaka!!sasa kma tunatambua hili ndio maana tukaeka adhabu kwa mwanaume!!why tuje tumuhukumu uyu aliyerubuniwa!!kumbuka ni mtoto au kasichana!!!tupambane na ujinga lakini si elimu!!
 
Wazazi waende kwenye QT na private wakirudi shule wataharibu wenzao
 
Mjadala uliokuwa unaendelea hapa juu ya Mimba za wanafunzi na kuzuiwa kuendelea na masomo, mimi ningeshauri tutumie tu majukwaa mbalimbali kuishauri serikali ifanye utafiti wa kutosha kujua tatizo liko wapi. Chanzo cha tatizo kikishajulikana tuanze kufanya njia mbalimbali za kumaliza tatizo hili. suluhisho sio kuzuia wasiendelee na masomo.

Kama mtu atarubuniwa kwa kukosa kujua umuhimu wa elimu yake ukisema wasiendelee shule utakuwa umewarahisishia wengine ambao wanachukia shule wabebe mimba ili wasiendelee na masomo. Suluhisho ni kuwafundisha watambue umuhimu wa elimu. Mtu akishajua anafanya nini shuleni ataweza kuepuka vishawishi vya aina nyingine vinavyoweza kumnyima masomo.

Kama tatizo ni njaa labda wanahongwa pesa, huwezi kulitatua kwa kuwatishia kwamba hawataendelea na masomo, suluhisho ni kuwapa elimu bora na huduma za muhimu wakiwa kwenye mazingira ya shule na nyumbani.

Tukijikita katika kutatua tatizo itasaidia Zaidi kuliko kuweka vitisho juu ya watoto. Tutakuwa tunarudi kule kule, kwasababu mtoto anagombezwa nyumbani, akifika shuleni waalimu ni wakali. Hata kama kuna vijana wanamsumbua anakosa wa kumweleza matatizo yake.

Kuna Maisha mengine yapo huko vijijini watu hawayajui wanaishia kutamka tu bila kuangalia kwa upana Zaidi. Unakuta mtoto baba yake ni mlevi kupindukia, mama na yeye anauza baa. Kaka zake ni wavuta bangi. Akirudi nyumbani ndio pabaya Zaidi kuliko hata shuleni. Sehemu pekee anayopata faraja ni kwa kijana wa bodaboda anaembeba bure. Unafikiri binti kama huyu ataachaje kubeba mimba?

Tuviangalie vyanzo vya watoto kupata mimba mashuleni tuanze kufanya mchakato wa kutatua matatizo haya. Taasisi zinazohusika na kutetea haki za mabinti ziongeze kasi kutembelea mashuleni na majumbani pia. Elimu inahitajika sio kwa mabinti peke yao kwasababu sio wenyewe wanajipachika mimba. Jamii nayo kwa ujumla inahitaji elimu.
Hii ni dunia yetu sote tupambane katika kuitengeneza kwa pamoja.
 
Hizo kauli za kiongozi....hivi angetamka wazi kwamba in ruhusa wao kurudi shuleni ingekuaje...no kama amehalalisha hizo mimba.HIYO NI KAULI YA MWONGOZO

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Kusema ukweli, zaidi ya kupambana na wezi (wale anaowachukia), kiongozi wetu ni mwepesi sana (intellectually). Uthibitisho ni vitu kama hivi anavyosema ambavyo havihusiani na kufukuza watu kazi. Mara NGO zimeleta ushoga ambao mbuzi na nguruwe hawana. What is that? Mara wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu walituibia. Mara kuigaiga. Kwani kutoa fursa kwa watoto wa kike ni kuiga? I am so disappointed.
 
Mimi sikubaliani na ile sheria ya mtoto wa kiume ambaye pia wanasoma wote darasa moja na huyo dada akimpa mimba mwanaume unaenda gerezani, Ni sheria ya ajabu kweli, inawezekana mwanamke kataka mwenyewe akalazimisha halafu kesi inapotokea mwanaume anaenda jela sio haki kabisa.
 
Back
Top Bottom