Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Huyu jamaa aandikiwe hotuba, kumnyima mtu elimu ni kumkatalia haki yake ya kibinadamu yale maazimio tuliyosaini yatawabana watakaotekeleza huu ujinga.

Juzi kawaponza trafiki wawili.
Kawaponzaje? Halafu sheria ya kuwafukuza wajaopata mimba shuleni kaanzisha yeye?
 
Atakayefanya kama alivyosema RAIS atakuwa MZAZI mpumbavu.Kuna shule za private,kama anauwezo ampeleke mtoto wake private.

Huu ujinga ati mtoto sababu amepata Mimba asisome aupeleke Lumumba na Chato
Hajakataza wasisome bali wasisome kwenye shule za umma. Kumbuka kuna private schools veta n.k
 
Kuna binti alipata ujauzito akiwa form 2 miaka ya nyuma kidogo.. akajifungua salama mtoto akawa mwaka moja kasoro wazazi wake wakapambana akarudi shule.. leo hii ni Mwalimu mshahara analipwa na anawasaidia watu wengine wakiwemo wazazi wake na serikali inakata kodi kama kawaida

Magu kwa upande wa vision hamna kabisa anajenga taifa la omba omba
Kabla ya magufuli taifa lilikuwaje? Kwa sab hii sheria ipo tokea Uhuru Tanzania bara haijawahi kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo waliofanya hivyo ni kwa ujanja ujanja tu.
 
Wewe ndo unavuruga mada mkuu.
Serikali inawajibu wa kuhakikisha watu wote wanapata frusa sawa Na za kutosha kuwawezesha kupata elimu.

Ndio mana inakusanya kodi inajenga bajeti,inajenga shule, inaajiri walimu,inatunga sera Na mitaala,inaandaa vitabu,inatunga mitihani ya kitaifa,inatoa vyeti,inatoa ajira n.k

Wenye uwezo siku zote huwa hawana ugomvi Na serikali mana watoto wao wanasoma IST,FEZA n.k

Haki inayodaiwa hapa Ni ya wanaotegemea elimu bure/elimu bila malipo watoto wa mtanzania maskini!!!
Mayatima,waliotelekezwa Na kuachwa bila uangalizi katika jamii!!!!
Naona hata mtoto wako wa kike akipata mimba shuleni utafurahi sana kwa kupata mjukuu shuleni
 
Angekuwa Ni binti yake angefanyaje, hiyo ni kumkomoa nani kumnyima huyu binti elimu? Sio kumwangamiza yeye na huyo Mwanaye na Kumfanya Mzigo wa Kudumu kwa Familia na Kwa Taifa?
Je ni waalimu, Madaktari wangapi, Viongozi wangapi wa kitaifa walipata mimba wakiwa wanafunzi na Bado wakaendelea na Masomo na sasa ni msaada kwao kwa familia na Taifa!

Mbaya zaidi hii kauli ya Kiburi na kijinga, ati sitasomesha "wazazi" ni kauli ya kiburi kanakwamba fedha za Serikali zitumikazo kwa ajili ya Elimu ni Ruzuku kutoka kwa Mama yake Magufuli au pesa zake za biashara ya sangara! Hana unyenyekevu wa kuona kuwa ni fedha za Walopa kodi wakiwemo wazazi wa hao mabinti, au kama sio kodi basi zinatokana na Raslimaliza taifa au mikopo ambayo jasho za kuilipa litatokana na Watanzania wakiwemo wazazi wa hawa mabinti.

Nilishasema Magufuli na Makonda akili zao zinafanana! Kama atabisha nitashangaa sana sio kidogo!
Mkuu kuna suala la maadili mema kwa wanafunzi wa kike. Ni kulea uhuni na umalaya shuleni ikiwa mwalimu ambaye ni mwanamama anafundisha ubaoni halafu huku kwenye madawati kuna wasichana watatu ambao wananyonyesha watoto nyumbani.

Hao wasichana watatu hawawezi kumpa heshima yule mwalimu mwanamama kwa sababu ya zile akili za kusema "huyu si ni mwanamke mzazi kama sisi?". Hakuna heshima katika mazingira ya aina hiyo, na pia hakuna utii wa mkubwa kwa mdogo.

Bila ya uwepo wa utii kutoka kwa hao watatu sidhani kama hao wasichana wengine watamheshimu huyo mwalimu mwanamama.

Waende wakasome VETA, waende shule za private, waende kokote kule, lengo ni lile lile, la kurudisha heshima ya elimu.
 
Hahahahha duhh huu mnyoosho sio wa nchi hii,mummanyire Maguu ehh...kwa kiasi fulani ana point ni muhimu kujenga character za watu km taifa,freedom ya kuzaa ikizidi ina side effects zake...kujitunza kusubiria ndoa kutakosa thamani kabisaa...hivyo kuathiri utengenezaji wa familia bora,freedom mfano mambo ya ushoga hivi ni jema hilo hata tulishabikie??

Japo waangalie namna gani mabinti ambao ni victims wa ubakaji watapona ktk hili na marufuku hii itaongeza abortions kwa hio tuangalie pia hiko
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Alafu hii.sio adhabu,mkuu badilisha mtazamo kidigo

Kumbuka pia mtoa mimba anachezea mvua 30 akibainika.

Labda hapa tuombe hiyo 30 nayo ifutwe

Niende kijijini nikafungue KA tuition kangu na mimi
 
Ni muhimu pia mabinti kwa kua ndo wahanga wa mimba zisizotarajiwa wakajengewa mazingira ya kuwasaidia ktk hilo...
1.mfano shule za boarding na hostels zinasaidia sanaaa kuwa mbali na wanaume... Mfano mi mambo ya mapenzi nimeyajulia ukubwani chuo,nlikua busy na shule boarding
2.mafunzo ya life skills yatolewe zaidi kwa wanafunzi wa kike na kiume waone thamani ya kupostpone mapenzi kpnd wapo shule wayafanye ukubwani huko
3.abstinence ihubiriwe zaidi km njia salama kwny hii ishu ya mapenzi
4.ikishindikana basi condoms zitumike

Otherwise Magu ana point... Tulivokua shule wadogo we were afraid of men mana mkiwa shule mara mnapimwa mimba nk.. Hamuoni siku hz watu kujizalia bila ndoa inakua kawaida tu,sio sawa...we can't have perfection but we need to preach and live what is RIGHT...exceptions lazma zitakuwepo and such is life...
 
Ilani ya ccm 2015-2020 inasema mtoto akipata mimba akiwa shule, atarudi kuendelea na masomo yake. Leo generali dikteta anaikana ilani hiyo.
 
Hivi Professor Lumumba ana maoni gani kuhusu kauli hii ya Magufuli?
Bado Anadhani Magufuli ni mtu sahihi?
Real deal au raw deal?
 
Mkuu kuna suala la maadili mema kwa wanafunzi wa kike. Ni kulea uhuni na umalaya shuleni ikiwa mwalimu ambaye ni mwanamama anafundisha ubaoni halafu huku kwenye madawati kuna wasichana watatu ambao wananyonyesha watoto nyumbani.

Hao wasichana watatu hawawezi kumpa heshima yule mwalimu mwanamama kwa sababu ya zile akili za kusema "huyu si ni mwanamke mzazi kama sisi?". Hakuna heshima katika mazingira ya aina hiyo, na pia hakuna utii wa mkubwa kwa mdogo.

Bila ya uwepo wa utii kutoka kwa hao watatu sidhani kama hao wasichana wengine watamheshimu huyo mwalimu mwanamama.

Waende wakasome VETA, waende shule za private, waende kokote kule, lengo ni lile lile, la kurudisha heshima ya elimu.

..lakini hata huko unakopendekeza wapelekwe kuna waalimu wa kike vilevile.

..au veta nako hakuna wanafunzi ambao hawajapata ujauzito wanaoweza kuwa influenced na hao waliozaa?

..tumejielekeza zaidi kwenye kuadhibu kuliko kuzuia tatizo la mimba mashuleni.

..matatizo haya kuna uwezekano yakatuzidi nguvu na maarifa.
 
Mkuu bila adhabu tulizopewa utotoni pengine tusingekuwa ni watu tuliokuja kuwa na heshima utu uzimani.

Ukiondoa zile cases za binti kubakwa ambazo ni chache, nyingine zote ni zile za msichana au mvulana kwa utashi wao wenyewe kuingia kwenye mapenzi wakiwa mashuleni.

Hawa ni lazima watishwe kwa kuambiwa kwamba wanafanya starehe na wapenzi wao kwa gharama ya kuwa tayari kupoteza nafasi ya elimu bure.

Huwezi kuwa na elimu bure halafu yule anayepewa bure aamue kutoiheshimu kwa kuendekeza umalaya shuleni.
 
Naona hata mtoto wako wa kike akipata mimba shuleni utafurahi sana kwa kupata mjukuu shuleni
Uelewa wako umeishia hapo ili uelewe ninachomaanisha mpaka uvue hiyo hirizi ama uzaliwe upya uje Na akili mpya hizo za kushikiwa hutonielewa kabisa!!!
 
tumeoa na tuna watoto , wengi mnaopinga hii kauli inaonesha ni wazinzi sana na mnampango wenu ni kuchochea uzinzi mashuleni.

huku wanafunzi watakaa wakijua wakipata tu bahati mbaya wanaleta mtoto kwa bibi afu anarudi shule kama kawa.
tumuunge mheshimiwa watoto waogope kuvuliavulia chpi wanaume waangalie masomo.
Siungi mtoto kupata mimba akiwa sio shuleni tu bali hata kabla ya ndoa, kuna vitu vingine vinaweza mtokea kutokana na mazingira akajipata katika hali asiyotarajia acha ulimbukeni, We huna mtoto, ungekua na mtoto usingeongea upuuzi wa namna hii, kuzaa hakumuondolei msichana akili darasani.
 
Hii ni kuwaamsha wazazi kuwa, ukiwa na mtoto mtunze na mlee kwenye maadili na kujitambua.
 
Kwa hili Rais yuko sahihi, unajua hatupendi kusikia ukweli maana unauma. Sema tu labda lugha imekua kali kidogo.
Tulipokuwa shuleni tulikuwa tunapimwa mimba kila mwaka, sikuwa hi kuona mwanafunzi mwenye mimba kuanzia form 1 hadi 6; na ilikuwa day school tena Dar; Maadili ni muhimu jamani, tuseme na vijana wetu wasiwe na mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni.
 
Mkuu bila adhabu tulizopewa utotoni pengine tusingekuwa ni watu tuliokuja kuwa na heshima utu uzimani.

Ukiondoa zile cases za binti kubakwa ambazo ni chache, nyingine zote ni zile za msichana au mvulana kwa utashi wao wenyewe kuingia kwenye mapenzi wakiwa mashuleni.

Hawa ni lazima watishwe kwa kuambiwa kwamba wanafanya starehe na wapenzi wao kwa gharama ya kuwa tayari kupoteza nafasi ya elimu bure.

Huwezi kuwa na elimu bure halafu yule anayepewa bure aamue kutoiheshimu kwa kuendekeza umalaya shuleni.

Una heshima gani? Heshima ni nini? Unaweza kukuta wewe ni Waziri na bonge la fisadi. Hapa unajaifanya una heshima. Kwani hao wanaoibia nchi ni kina nani kama sio nyinyi mnaofurahia victims (msichana kupata mimba akiwa shuleni ni victim)? Haki ya msichana wa nchi hii kupata elimu ni haki ya kuzaliwa - haipaswi kutegemea utashi wa Rais. JF imeshuka viwango sana jamani. Eti kuruhusu wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo ni kuhamasisha wasichana wapate mimba. Seriously? Na watu wenye mawazo ya hovyo kiasi hiki ndio wanazungumza mambo ya viwanda etc. Kweli tuna bahati mbaya nchi hii.
 
Back
Top Bottom