Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Jamani kuna dogo kakaa kulia kabisa kwa JPM amevaa shati la drafti na miwani kanyoa denge...ni nani huyu maana namuona si wake wazee wa kaunda suti au ni mwanafamilia au mwanachuo?
Ingizo jipya
 
Huyu Mkandala naona anatema cheche hadharani.
 
Hapa nasubiri Dr Bashiru katibu mkuu wa CCM.
 
Jamani kuna dogo kakaa kulia kabisa kwa JPM amevaa shati la drafti na miwani kanyoa denge...ni nani huyu maana namuona si wake wazee wa kaunda suti au ni mwanafamilia au mwanachuo?
Mshiriki wa kawaida kama wewe unayefuatilia kwenye runinga.​
 
Yaani kama watoto wachekechea vile.Eti maprof duu.Full aibu.

Wameniangusha mno Mkuu yaani ni bora hata tu wasingekubali kwenda hapo Kongamanoni Nkurumah kwani ' wamejichoresha ' na ' wamedharaulika ' kwa kiasi fulani vile vile. Hebu angalia ' Confidence ' ya Kutukuka kabisa ya Profesa Mkandala hadi ' Presentation ' yake inavutia na inakufanya usichoke na usiboreke kumsikiliza. Huyu kweli ni ' Academician ' kabisa na alifanya vyema ' research ' yake pamoja na ' preparation ' ya anachokifanya leo tofauti na hao wenzie Wawili ambao Kipaumbele chao kilikuwa ni Kusifia na Kujikomba tu ama kuendelea kuaminiwa au kutafuta Cheo / Fursa / Madaraka.
 
Askari wote hawa na silaha hizi ni wa kazi gani? Nimekumbuka maadhimisho ya uhuru enzi za utawala wa marehemu Canal Muhamar Gaddafi.
a78305190a7bb174a91069e6dfad085f.jpg
 
Huyu Prof Rwekaza Mkandara yeye ndo anasifu moja kwa moja na bila aibu anamlinganisha Rais wa awamu hii na wa awamu ya kwanza (eti hao wengine hana muda wa kuwalinganisha na huyu). Yaani huyu amestaafu ila anataka uDC!
Mukandala kuwa DC ni dharau
 
Huku umeme wamekata tangu asubuhi.
Je,Hakuna Professor aliyefanya utafiti baada ya kujiuliza maswali yafuatayo?:-

Swali la Kwanza:-

Kila kitu kina faida na Hasara.
Je, Bwawa letu litakalojengwa la Stiglers litakua na ujazo wa Cubic Meter ngapi na Pressure kubwa kiasi gani ardhini na Madhara yanayoweza kutokana na mgandamizo huo hasa Tetemeko la ardhi kwa maeneo ya miji ya jirani ikiwemo jiji la DSM ukizingatia litakua ni bwawa kubwa lisilo la asili???

Swali la Pili:-

Kila kitu kina faida na hasara.
Tumekua tukisikia taarifa za kusifia tu ujenzi wa Bomba la mafuta kutaka Uganda Mpaka Tanga.
Je, Wataalam wetu wamewahi kujua ukubwa wa Ardhi yetu iliyomegwa kupitisha Bomba hilo ? Je, in Hekta ngapi za mraba zitakazokua ndani ya nchi yetu ambazo zitakua hazifai kwa matumizi endelevu ya wananchi kutokana na kupita kwa bomba hilo ?
Je, kupita kwa bomba hilo hakutakua na faida za muda tu kama vile vibarua wa kuchimba lakini baada ya hapo ni hasara ya milele kwa kuwa ardhi kubwa sana itakua haitumiki kwa maendeleo ya wananchi na hata serikali?
 
Tena wachina ni hatari kuliko wazungu angalia wawekezaji wa kichina sehemu zao uonevu na hata uharibifu wa mazingira. Kwa mikopo ya China ipo siku tutatawaliwa kinguvu
Hakuna nchi katilii kama China hasa kwa rais huyu wa sasa!! Africa tutaumia sana, matter of time
 
Ndo sasa hapo haaajiamini kama wasomi hapo angesema pande mbili nzuri za kiswahili pia umuhimu wa kingereza kidunia. Sio lazima ukosoea direct unasema tu ukweli kwa pande mbili
Nimemsikia akiongelea kuwa wasisome kiingereza tu.wasome pia kichina,kiarabu,kifaransa na kijapani.nadhani hakupangilia vema hoja zake tu.Ila so far mpaka sasa yeye ndiye mchangiaji bora mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom