Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Nilifikiri atazungumzia jipya lolote katka nedani za jiolojia, akaishia kusifia tena kwa kupitiliza huku kwa makusudi akioneka 'kuomba' usikivu wa jiwe!
Angalau huyu Mama anazungumza fact.Sio kujikombakomba kama mabrazamen waliopita ma profesa uchwara.Ndio maana waandaaji walipunguza majina ya kina mama.
 
Nimefatilia wote kuanzia mzungumzaji wa kwanza wengi hawasimamii kweli mfano prof Moshi mara alisema tusitegemee mksaada ya western countries ndo imetufanya hatupigi hatua eti China wamepiga hatua ndo tu side nao tangia ujenzi wa Reli ya mwanzo kitu ambacho si ukweli umaskini watu ni uzembe wetu wenyewe. Sasa kongamano la kisomi prof hashauri kisomi hyo si matumizi mabaya ya elimu
Mkuu tuseme ukweli, hakuna prof. mwenye usubutu wa kuzungumza kwa kukosoa pale. Wote wako biase kutokana na mazingira ya kongamano lililo andaliwa na wakalibishwaji. Mfano wewe ungekaribishwa pale ungeweza kusema jambo lolote la kukosoa. Mfano huyu prof. anayewasilisha maada ya lugha, anadai eti watoto wetu wafundishwe kiswahili tu, waachane na kingereza. Jamani hivi dunia ya leo ni ya kujifunza lugha mmoja tu?.
 
Kongamano linaanza leo tarehe 01/11/2018 kuanzia saa 3:00 asubuhi hii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ni Mshiriki Maalum kwenye Kongamano hilo. Watoa Mada ni Wanazuoni wabobezi katika masuala ya Uchumi, Siasa ya Uchumi,Siasa ya Jamii, Sheria n.k

Nitawaletea kila linalojiri kupitia Mada hii. Unaweza pia kufuatilia moja kwa moja kupitia Runinga ya TBC1


======

UPDATES

Kongamano UDSM: Hali ya Uchumi na Siasa nchini Tanzania 2018

- Kanuni 3 zitazingatiwa ktk mjadala: Uwazi na Uhuru, heshima na staha, kuzingatia muda

- Rais Magufuli hatazuiliwa kuongea hata akizidisha muda

Prof. Humphrey Moshi: Nitazungumzia “Umuhimu wa Viwanda ktk Uchumi wa Nchi hii”

- Kwa miaka 15 Uchumi wa TZ ulikuwa ukikua kwa 6-7% lakini haukuwa Uchumi Shirikishi

Prof. Moshi: Sekta ya Madini haikuweza kupunguza kasi ya umasikini na ajira

- Bado mfumo wetu wa uchumi haukuwa umebadilika; hakukuwa na mfumo mbadala

Prof. Moshi: Ukitaka kupunguza umasikini kwa haraka na kufikia uchumi, viwanda ni lazima

> Viwanda ni sekta vuguvugu, ni kiwanda cha uvumbuzi. Hakuna sekta yoyote katika taifa lolote iliyo na mahusiano na uchumi kama viwanda

Prof. Moshi: Kwa nchi za Afrika hasa Tanzania viwanda ni sekta kombozi, kwahiyo kwa Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kitu sahihi kinachopaswa kufanyika

> Wakati wa Mwalimu, tulikuwa na viwanda vya kila aina na viwanda vinazalisha ajira zenye hadhi

Prof. Moshi: Kulikuwa na mpango wa SAPs lakini baadaye tukaja kuwa na ubinafsishaji ambao ulifyekelea mbali viwanda

> Wafadhili wanatoa mapendekezo yao ambayo hayaendani na mipango ya Taifa
> Wakati huo kulikuwa na viwanda vya umma lakini hakukuwa na wataalamu, sasa wapo

Prof. Moshi: Miaka ya nyuma hatukuwa na uwezo wa kununua katika masoko ya kimataifa

> Kulikuwa na uwekezaji katika tafiti za mipango na hakukuwa na utekelezaji, watu wa nje wanakuja kuchukua mipango Tanzania na kwenda kuitekeleza

Prof. Moshi: Serikali ni lazima ikae mbele wakati wa kuendeleza viwanda, tulikaa miaka 25 tukisubiri sekta binafsi ituletee umeme

> Tulikaa miaka mingi tukisubiri sekta binafsi ituletee kilimo cha miwa. Miradi mikubwa ya Marekani inamilikiwa na serikali

Prof. Moshi: Elimu, miundombinu na viwanda lazima viende pamoja. Tuboreshe uhusiano na nchi za Asia

> China wakati wanajenga SGR walikuwa wana kipato cha 1/3 ya Watanzania lkn sasa ni zaidi ya mara 10
> Tuimarishe mahusiano na nchi hizo, tupunguze utegemezi kwa nchi za Magharibi

Prof. Hudson Nkotagu anasema:

Pro. Nkotagu: Nitazungumzia Nishati na Miundombinu katika kuendeleza uchumi wa viwanda

> Vyanzo vya nishati ni vingi vikiwemo vanzo 'jadidifu na vile visivyo jadidifu'

#KongamanoUDSM

Pro. Nkotagu: Chanzo jadidifu kama Mto Rufiji kufikia 2020-2025 kitakuwa kinachangia asilimia 21 ya nishati ya umeme nchini

> Yako maeneo yenye dalili za kuwa na mtiririko wa mafuta. Serikali imejipanga kuzalisha Mewati 5,000 na kufikia 2020-2025 kupitia Stieglers Gorge itafikia Megawati 10,000
Ili Serikali imeweza kutekeleza miundo mbinu wezeshi ikiwemo Reli, barabara ya kuunganisha mikoa na nchi za jirani. Barabara za vijijini. Usafiri wa anga na Majini vimeboreshwa. Ndege zimenunuliwa karibu 9. Kuimalisha usafiri wa angIa. Meli zinatengenezwa na nyingine zinakarabatiwa. Hiyo ni miundombinu wezeshi ya kuinua uchumi

Kuna changamoto

Wataalamu ni wachahce sana. tunatakiwa tuwe na injinia 1 kwa mafundi watano na wafundi michundo 25. Tnatakiwa tuwe na Injinia 10 Mafundi 50 na fundi michundo 250,hiyo ni ya kitaifa.

Tuhakikishe nishati zetu hazipotei, mfano taazinawaka na jua linawaka

Stiegler's Gorge

Faida ya Huu Mradi wa Stiegler's Gorge

tutatumia asilimia 3 tu ya eneo lile.

Itapunguza ukataji miti

Hii nishati ni endelevu sababu haihitaji wabia.

Itavutia wawekezaji

Itaongeza ukuaji wa miji

Mapendekezo

Napendekeza Serikali iweze kuendekeza vyanzo mbalimbali vya nishati, Kuongeza Wataalam, Kuongeza Tafiti na kuwawezesha watafiti na kuelimisha raia.

Wakuu ! Je,tumefikiri kwa jicho la tatu kusudi la Kongamano hili ?
Sikiliza maoni ya hao wanaoitwa wasomi yana lengo lipi kama si kuthibitisha mawazo ya rais Magufuli kwa jamii na kumtetea katika mtazamo wake anaoleta kwa nchi ?
 
Kwa ambao hawawezi kuaccess tv ingia kwenye page ya facebook ya ITV wanaonyesha live!
 
Hata China ni mnyonyaji vile vile maana mikopo yake ina masharti usifikirie Kuna mataifa makubwa yanapenda umaskini uishe kwetu maana wanapenda tuwe tegemezi sio China wala western countries itatuondolea umaskini tusipoamua wenyewe
Kujitegemea ndio mpango mzima. Anachopinga prof Mushi ni ile tabia ya mzungu kukwambia usifanye hiki na kile halafu yeye akiwa kwao anafanya. Ndio maana ya mfano wa airbus na boeing kumilikiwa na serikali za Uingereza, Ujerumani na Ufaransa halafu tunaletewa dhana ya sisi kutokuwa na haki ya kumiliki mashirika yetu ya ndege.
 
Mkuu tuseme ukweli, hakuna prof. mwenye usubutu wa kuzungumza kwa kukosoa pale. Wote wako biase kutokana na mazingira ya kongamano lililo andaliwa na wakalibishwaji. Mfano wewe ungekaribishwa pale ungeweza kusema jambo lolote la kukosoa. Mfano huyu prof. anayewasilisha maada ya lugha, anadai eti watoto wetu wafundishwe kiswahili tu, waachane na kingereza. Jamani hivi dunia ya leo ni ya kujifunza lugha mmoja tu?.
Ndo sasa hapo haaajiamini kama wasomi hapo angesema pande mbili nzuri za kiswahili pia umuhimu wa kingereza kidunia. Sio lazima ukosoea direct unasema tu ukweli kwa pande mbili
 
Back
Top Bottom