Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Hili ni Kongamano la Hali ya uchumi na siasa au Kongamano la "kusifu" na "kuabudu"??
Naona la kusifu na kuabudu!! Maana naona mkandala amejisahau anadhani yeye ni Msemaji wa serikali maana kwa hizi pambio lazima aukwae uwaziri. Mpaka anamfananisha jiwe na Mchonga
 
Prof. Mukandara is a genious.
Nimeukubali uwasilishaji wake kuliko walio mtangulia.
Mwenyewe nimemuelewa yuko vzuri hata ushauri wake mzuri sana na kueleweka wengine sijui walikula maharage ya wapi
 
Tatizo hawa maprof wetu wajitoa akili ili tu,wapate ulaji.maana wanajua kuwa ukijitoa ufahamu lazima ulambe dume.Ukweli ni kuwa wanauza utaalamu wao.pathetic.
 
Mkandara ndo nimemuelewa vzuri kaongea kulingana na hoja ya mjadala katisha sana yani

Wameniangusha mno Mkuu yaani ni bora hata tu wasingekubali kwenda hapo Kongamanoni Nkurumah kwani ' wamejichoresha ' na ' wamedharaulika ' kwa kiasi fulani vile vile. Hebu angalia ' Confidence ' ya Kutukuka kabisa ya Profesa Mkandala hadi ' Presentation ' yake inavutia na inakufanya usichoke na usiboreke kumsikiliza. Huyu kweli ni ' Academician ' kabisa na alifanya vyema ' research ' yake pamoja na ' preparation ' ya anachokifanya leo tofauti na hao wenzie Wawili Profesa Moshi na Profesa Qorro ambao Kipaumbele chao kilikuwa ni Kusifia na Kujikomba tu ama kuendelea kuaminiwa au kutafuta Cheo / Fursa / Madaraka.
 
Mnachokifanya hapo UDSM siku hizi ni kukiua chuo kwa kasi kubwa. Hiyo hadhi mliyoikuta hapo UDSM ilijengwa na waliowatangulia, akina Dr. Lwaitama, Dr. Mvungi, Prof. Mpangala, Prof. Luhanga, Prof. Othman, Prof. Ngwale, Prof. Rugumamu, Prof. Chachage, n.k. Badala ya kuiendeleza hadhi ya chuo ninyi mmekuwa mstari wa mbele kufifisha chuo. Ona sasa hivi waziri anakuwa hata na ujasiri wa kuwapangia cha kufanya kwenye udahili wa wanafunzi. Kitakachofuata ni kupangiwa cha kufundisha. Ovyo kabisa UDSM kwa sasa. Ile chemchemi ya fikra mmeipoteza kwa kukumbatia kujipendekeza kwa watawala ili mpate vyeo.

Hakuna cha maana kitajadiliwa hapo. Kongamano lenyewe limeandaliwa kwa kusudi fulani kwa ajenda ya siri ya kutaka kutuaminisha kuwa jamaa anafanya kazi nzuri. Shame on you.
 
Hakika profesor. Mkandala kaongea kisomi kabisa, uwasilishaji wake ni kama ukosoaji kwa serikali lakini kulibaini lazima uwe makini, la sivyo unaweza ona anasifia tu.
 
Ni kwelii kabisa, jamaa hawa ubinadamu kabisa na watu tofauti na wachina wenzao ukitaka kujua ukatili wa wachina fatilia maisha wanayoishi watu wa Tibet na Taiwan pia honkong'o huko ni balaa tupu, ukija huku Africa ndo kabisaaa
 
Kongamano lenyewe ni mwendelezo wa juhudi za kusifu na kuabudu mbele ya mfalme.
 
naona wameamua kuongea upande wa siasa tu badala ya siasa na uchumi
Ilitakiwa kuwa na kongamano la uchumi pekee na la siasa liwe lenyewe
 
Kila mtu lazima asifie leo.Maana hiyo inatambulika.Lakin usifiaji huu prof.Mushi ametisha kwa mapambio.
Wenzake wanapewa mashavu manene huko kwny ma board etc kwanini na yeye asisifu barabara.
 
Mumemtega ZITTO,ndo maana mukamuita polisi kuepuka aibu eeee
 
Kuna yule Mama na Prof Mukandala naona wamepiga vizur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…