Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Serikali iwasaidie lakini si vizuri kuwapa ahadi hewa hasa kujenga nyumba zao. Labda serikali iwaondolee kodi kwenye vifaa vya ujenzi hasa cement, bati na nondo
Nia ya kusaidia wanayo tatizo hao wasimamizi, watakula pesa zote kabla kuzifikisha kwa wahusika. Msaada unachinjwa toka juu mpaka chini. Wahanga wanaishia kung'aa macho.
 

Mgonjwa anahitaji maneno ya matumaini hata kama ana Kansa anajua hatapona. Ukimwambia usimalize dawa maana hutapona, mgonjwa atakufa siku si zake
 
Serikali haijatoa chochote hadi sasa kwa sababu haina pesa yan imefulia...basi sawa,wawape hizo pesa za misaada hakuna haja ya kuwasimanga wahanga.....yani mtu ukiwa huna pela na ukijua utaombwa pesa haya ndo huwaga mujibu yake
 
Nchi hii tulizoea kauli za kinafiki zisizotekelezeka, sasa tumepata Raisi anayenyoosha maneno hata kwenye wakati mgumu ni kuongea ukweli tu kwa kwenda mbele.
Kwa wapinzani ni haki yao kikatiba kubeza ukweli ambao umesemwa na Mh raisi, wao walitaka Raisi atoe ahadi zisizotekelezeka ili ije kuwa mtaji wa kisiasa huko mbeleni.
Hizi ni zama za kunyoosha maneno, mh raisi ameanza na sisi huku kitaa tuige mfano wako maana tumekuwa jamii ya kinafiki kupindukia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…