Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Binafsi sijaona tatizo na maneno yaliyotamkwa na raisi, labda kama kuna video nyingine zaidi ya hiyo hapo juu. Kweli mtu ukuta umebomoka unasubili msaada wakati una uwezo wa kuurekebisha? Kuna watu wanahitaji msaada kweli na hao ndiyo wapewe kipaumbele.
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] si mlitaka aseme..ndo kasema sasa...poleni wana kagera.MUNGU mwenyewe awatokee.Awasaidie.na kuwafariji wakati huu mgumu na wafiwa wote MUNGU awape faraja.
 
Rais wakati akipokea report ya waziri mkuu kawambia wana Kagera wasibweteke kungojea misaada wafanye kazi wasingoje misaada serikali itafanya inapoweza tu
Maneno ya faraja kweli kweli
 
Waliomchagua watajuta kwa nini anatoa kauli kama hizi wakati wananchi wa Kagera wanahitaji misaada?
 
Rais yupo sahihi kabisa, hakuna haja ya unafiki. Wananchi waanze ujenzi wa nyumba zao sio kusubiri Serikali. Serikali na wahisani watasaidia si kwa asilimia 100 kiasi cha kuwafanya wabweteke kusubiri serikali.
 
...sasa naamini hata hizo zinaweza zisiwafikie walengwa...naona wanajenga precedent ya kuepa kupeleka pesa za wahanga....wazee wa kupindisha priority...hukawii kukuta pesa inapelekwa Dodoma...kusaidia kuhamia....lol
 
Siku za kwanza watu mitaani walikuwa wanasema limeletwa na yeye sasasijui ulikuwa ni utani au chuki binafsi, alipokaa kimyaa zaidi hayo maneno yakazidi kukolea,ila watu waache imani za ajabu hakuna binadamu awezaye kuleta tetemeko, Naamin mh.rais ni mtu makini na anafuatilia haya majanga.
Hilo ni tukio la kiphysical lakini chanzo chake ni cha rohoni. Kumbuka Paulo na Sila waliomba na kumsifu Mungu likatokea tetemeko na milango ya gereza ikafunguka. Tukio la kimwili lenye chanzo cha rohoni. Hizo ni kanuni za rohoni, shetani aweza kuleta tetemeko kwa kutumia mawakala wake hapa duniani.
 
Tatizo letu tunapenda kupewa ahadi hewa pasi utekelezaji!,, nahisi zama za ahadi zimekwishwa sasa ni ukweli mtupu unaambiwa kilichopo unakaa kimya, (jitahidini misaada itawajengea miundo mbinu yenu)
 
Bibi yule aliyefiwa na mtoto wake wa kike na kuachiwa wajuu watatu pia ajenge kwanza harafu ndo wamuone?..
kazi ipo kweli kweli, yaani majeruhi wajipeleke wenyenye ama wajipe wenyewe huduma ya kwanza kisha serikali inayo wajari sana hawa wapiga kura wake masikini ndo iwasaidie.

Hapakuwa na lugha nyingine kwa leo then hayo maelezo yakatolewa tu wanaoshugulikia suara hilo.... Wataanzania waombe upendeleo maalumu kwa Mora ili haya yasijitokeze tena maana , serikali yetu inahitaji miaka 100 kujipanga na majanga ya asili ama jamga lolote lile.

Mv.Bukoba.
ajari ya Trein.
Mafuliko na mengine mengi bado hatupo tyari kujipanga?
 
Yuko sawa ... Kujengea wananchi nyumba sio kazi ya serekali ... Kama ungekuwa hivo tusingejenga miaka yote tungesubiria tujengewe... Kazi ya serekali Ni kutengeneza miundo mbinu ya public kama barabara shule madaraja hospital maji UMEME tutimize wajibu wetu kama watanzania bana khaaaaa... Namkubali magufuli ...# raiskeshasema#
Tofautisha kujengewa na maafa
Duniani kote wahanga wa maafa husaidiwa na serikali zao au wahisani.
Ni nani alijiandaa na maafa?
Kwanini serikali ina mfuko wa maafa?
Hii ndio kazi ya mfuko wa maafa
 
michango itasaidia kuboresha miundo mbinu na kuwapa mahema ya kujisitiri ila wafanye kazi wanaanze wao serikali itawapa taff watakapo shindwa
Ni kweli mkuu, ifike mahali tuwe wasema kweli hamna haja ya kufichaficha. Sio jukumu la Serikali kuwajengea watu nyumba za kuishi. Serikali itarejesha miundombinu yote ya kijamii iliyoathirika na kutoa misaada ya awali ya kibinaadam na kusaidia kurejesha hali kwa waathirika.
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
hii ni kweli ajali haikusababishwa na serikali ya CCM,je
ile balaa iliyo sababishwa kwa wakazi wa Mbagala na Gongo la Mboto walilipwa nini?Mbona wanaendelea na maisha....na hata wengine wamekwishisha sahau..
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.

Sidhani kama fedha na misaada mingine imetolewa na serikali peke yake, michango mingi zaidi imetolewa na watu binafsi na mashirika mbalimbali, kwa hiyo nashauri kwamba wote waliochangia wasitumie fursa hiyo kuwasimanga wahanga wa tetemeko, misaada wanayopewa ni kidogo sana ukilinganisha na hasara waliopata, ya upotevu wa mali na hata maisha.
 
Bwana heee,hivi unajua kwa Tanzania kumiliki nyumba ni shughuli pevu sana,kwa halii ya kiuchumi watu washapatwa na majanga alafu ndo waanze pandisha nyumba inawezekana ila co kirahisi hvy,maana wengine ndo wachangishane ukoo mzima.
Kwa hiyo unataka Serikali iwajengee nyumba??
 
Huko sumbawanga kuna kaya 24 nyumba zao paa zimechukuliwa na upepo. nao tena wanasubiri serikali ikawajengee mbona kazi ipo
 
Huyu jamaa ni mkatili sana. Hana huruma aisee. Bado mijitu itakuja kujipendekeza kusifia na kuitetea hiyo kauli. Mungu atalipa kisasi!
 
Kwani kasema uongo? Mbona ni kweli tupu? Nimesikia mpaka viongozi wa makanisa wanataka wajengewe makqnisa yao. Hii ni aibu. Wekeni bima nyumba zenu japo hata bima hazihusiki na majanga ya asili. Serikali haijengi nyumba ya mtu kwa majanga asili. Utapata turubali na hema kwa muda wakati unahangaika ku settle na si kujengewa nyuma. Amkeni!
Watanzania wamezoea kupata faraja hewa na hawataki kuambiwa ukweli. Rais kaongea kweli tupu mm namuunga mkono.
 
Back
Top Bottom