Wanawake ni viumbe wa ajabu sana,naamini Mungu aliwapa wanawake moyo wa kipekee sana,moyo wa uvumilivu na upendo.Wakati jamii inashangazwa na baadhi ya mienendo ya wanaume,mienendo ya ubabe na kutojali,wanaume hao wanaoonekana wa ajabu huku mitaani hutoka katika familia zao.
Pamoja na mitazamo hasi juu ya wababe hawa,nyuma yao kuna wanawake wavumilivu,waliowapenda jinsi walivyo na waliotayari hata kuhatarisha Maisha yao kwa kuwatetea.Laiti wanadamu wote wangeumbiwa moyo wa kike,naamini dunia ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.Hongereni Mama zetu,kwani wababe wote tunaowashangaa katika dunia hii,pamoja na ubabe wao bado mnamudu kuishi nao!!Kama haya ndiyo tunayashuhudia sisi tulio nje ya nyumba,Mama aliye ndani anashuhudia na kuona mangapi?Asanteni akina mama.