Rais Magufuli timiza ahadi yako ya kumpatia ajira Joshua Nassari

Rais Magufuli timiza ahadi yako ya kumpatia ajira Joshua Nassari

Hii National Park imeanza lini?
Wewe uko nchi gani? Tulishasomba wanyama wengi toka mbuga mbalimbali na kuwapeleka kule Chato kwenye pori maalum lililotengwa na JIWE. Bila mbuga za wanyama Chato haiwezekani! Nasema haiwezekani.
 
Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli wakati wa kipindi cha kampeni ulitoa ahadi ya kumpatia kazi kijana wetu mpendwa Joshua Nassari.

Muda unakwenda kasi sana tangu kampeni zimalizike na wewe kuibuka na ushindi wa kishindo.Kijana wetu wetu ana mtoto ambae anahitaji matunzo ya kiwango cha nafasi za juu za kiserekali kama Regional Commissioner au High Commissioner au Mkuu wa shirika lolote zuri la umma kama NSSF, PSPF, TANAPA, NCAA, CRDB, KADCO, TANESCO, TANROAD, UWASSA,TBC, na NK.

Kijana wetu Nassari alishiriki kikamilifu kampeni hadi ukapata ushindi wa kishindo,hata kama yule jamaa wa ubelgiji anasema kulikuwa na kosoro nyingi lakini wewe sasa ni Rais wa JMT.Kwa nafasi yako una nafasi kibao kuanzia serekali kuu,serekali za mitaa,mawizara kibao,nafasi za ubunge 10 jimbo la Ikulu.Najua una shughuli nyingi kiasi unaweza kusahau ebu tupia jicho kama ikishindikana basi mpatie nafasi ya RAS kijana asiteseke na kusahaulika.

Wasalamu Ngongo safarini Chato National Park.

Hi Nassari. Kwanini usjiajiri.

Ulipata muda wa kutosha kukusanya mtaji.
 
Muda unakwenda kasi sana tangu kampeni zimalizike na wewe kuibuka na ushindi wa kishindo.Kijana wetu wetu ana mtoto ambae anahitaji matunzo ya kiwango cha nafasi za juu za kiserekali kama Regional Commissioner au High Commissioner au Mkuu wa shirika lolote zuri la umma kama NSSF, PSPF, TANAPA, NCAA, CRDB, KADCO, TANESCO, TANROAD, UWASSA,TBC, na NK.
sio kila kazi ya serikali ni ya kutangazwa
 
Ni juzi tu Waziri Mkuu kahimiza Watu kujiajiri, mwambieni ajiajiri aache uzembe.
 
Utakuta wewe ndo Nasari mwenyewe 😂😂
 
Hii haina uhusiano na ahadi ya Mheshimiwa Rais.
Kwa hiyo unakiri ya kuwa Wanasiasa wanajua tu kuhikiza wengine Wajiajiri lakini wao wanasubiri ajira....maana hata kama kuna ahadi hazuiliwi kujiajiri incase ahadi itayeyuka.
 
Wewe uko nchi gani? Tulishasomba wanyama wengi toka mbuga mbalimbali na kuwapeleka kule Chato kwenye pori maalum lililotengwa na JIWE. Bila mbuga za wanyama Chato haiwezekani! Nasema haiwezekani.
Na tunafanya tafiti namna ya kuhamisha mlima
 
Nassari acha njaa tushajua ID yako ni Ngongo naona umesugua benchi umefulia hadi umekuja kujianzishia thread yako. Jiajiri kiazi wewe, nyie si ndio mnaoshinda bungeni mkisema vijana wajiajiri.

Kukee isembo kabisa.(najua utanielewa)

Hii hapa link ya ule uzi wako uliokuwa ukipima upepo kuhamia kijanini.

Da umemchana makavu, cha kufanya mods waverify ID yake tu
 
Nassari ameapa kuwa kama hadi March mosi hajapewa kazi atahama nchi na akifika mbele ndiyo ataiumbua CCM na ataeleza yote yaliyo nyuma ya pazia kuanzia biashara ya kununua wabunge wa upinzani hadi hawa covid 19, na kwa jinsi anavyozungumza kwa hisia kali atafanya kweli.
Kwa hiyo na yeye alinunuliwa? Kama ni hivyo haoni kama atajidhalilisha yeye mwenyewe?
 
Back
Top Bottom