Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana
Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?
Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Inategemea "status" ya afanyaye utani..
Aidha;
å Kuna wakati wa kufanya utani.
å Kuna mahali pa kufanyia utani
å Chagua aina ya utani
å Angalia na aina ya watu unaowafanyia utani.
Bwana Magufuli ni mgombea Urais na wakati huohuo bado ni Rais wa JMT..
Kwa hadhi (status) yake ya cheo na mamlaka ya Urais hakupaswa kutoa kauli hiyo in public bila kujali ni utani au kweli..
Ili ujue kuwa alikosea na amechemka kweli, tazama ilivyopokelewa na umma. Imepokelewa hivyo hivyo. Hawahitaji uwaambie ilikuwa ni UTANI tu...
Najua tatizo lako unaweza kusema, "...ooh, mapokeo mabaya ya kauli hiyo ni kwa wapinzani tu..."
Siyo kweli hata kidogo na utakuwa unajidanganya wewe mwenyewe na nafsi yako..
Amini usiamini, wana CCM na serikalini huko hawajapendezwa na wanakiri, mgombea wao anakosea na anawapa wakati mgumu kuzuia "damage" ya kauli zake zinazomponyoka bila breki...!!
Kumbuka hawa ndiyo wanapambana kufa na kupona usiku na mchana kumwokoa abaki madarakani...
Lakini, wao wanapojitahidi kupambana kumsafishia njia ya kumshindisha iwe "Mungu anataka au hataki" lakini wakitoka tu huku nyuma wanayemsafishia anamwaga kinyesi paliposafishwa..!!!
Na kwa taarifa yako unapofanya kampeni katikati ya siasa za ushindani wa vyama vingi, tena ukiwa na mtu na mgombea mpinzani wako aina ya Tundu Lissu upande huu, basi chunga sana mdomo wako..
Kauli ndogo unayodhani unaitoa kiutani lakini bila HEKIMA na BUSARA inaweza kukugharimu kuliko maelezo..
Unaweza kuthibitisha hili kwa jinsi timu kampeni yake wanavyopata shida kuitetea (ukiwemo wewe) huku wapinzani wake wakiitumia kama silaha kumpiga nayo...!!
Ona tu. Wapinzani wake hadharani kwenye mikutano yao wanasema huyu mgombea awatumie madaktari wake anaotembea kuchunguza afya ya akili yake maana inawezekana haiko sawa..!
Unaona hii?
Kubali kuwa, Mzee amekosea na anafanya Makosa haya several times..