Kupenda au kutopenda kitu au mtu fulani ni personal feelings ambazo haziwezi ingia katika kipengele cha uzalilisha, labda kiwe ni sera ya nchi kuwatenga watu kutokana na maumbile yao ya kiasili.
Ni haki yako kutaja sifa za wanawake unaowapenda, hivi angesema "huyu kwanza ni mweusi kwahiyo ninapenda wanawake weusi kuliko weupe", ungemlaumu?.
Mtu binafsi kuonyesha mapenzi kwa aina fulani ya watu, haiwezi kuwa ni udhalilishaji, hasa hayo mapenzi yasihusishwe katika utoaji haki za msingi za binadamu.
Kama kuna wanawake watajaojisikia vibaya, huo ni udhahifu wao kutokana na kutojiamini kwako. Kuhusu wanawake kujichubua kwasababu ya kuwaridhisha wanaume wanaopenda wanawake weupe, hilo ni jambo la kijamii, mbona kuna wanawake wanaovaa nguo fupi sana ili kuwaridhisha wanaume lakini wanawake wengi wamekataa kuiga hicho kitendo. kwanini waige kubadilisha rangi ya ngozi?