Rais Magufuli, umewadhalilisha sana wanawake weusi nchini

Rais Magufuli, umewadhalilisha sana wanawake weusi nchini

Wewe ni cheusi kweli? Hebu weka picha yako tuuone weusi wako mataga wewe
Mimi hapa mweusi na sijaumia chochote
Labda Kama wee mtoa mada umeumia pole Sana mwanamke mwenzangu

Tena mwisho akasema i mnajua Tena wasukuma!!!!
Alimaanisha wasukuma wanapenda wanawake weupe na aalitania
 
Au huyu ndugu ana duka la mikorogo labda atuambie ili Tujue moja
 
Mzee baba anatania hivyo mbele ya halaiki ya watu wazima na watoto, vipi huyo cheupe akiingia ofisini kwake halafu wakae wawili tu hata mfanya kweli?

Eeeeeh Mungu walinde wake za watu dhidi ya mbwa mwitu wabaya
 
Watu tuko tofauti, tunatakiwa kuishi kwa kutumia standard code of conduct. Nimezaliwa porini, tunajisaidia vichakani, nikifika mjini nikianza kutafuta vichaka nitajinyea au kuloanisha nguo kwa mkojo.
Mtu wa miaka 61 huwezi kumbadilisha. Cha muhimu ni kumfahamu namna anavyobadilika kimaongezi.

Hakuna mkamilifu chini ya jua.
 
Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Yeye atutanie sisi tusimtanie!
 
View attachment 1595438


Kauli yako uliyoitoa leo hii, eti huyo mgombea wako cheupe akija Ofisini mwako utamuhudumia haraka kuliko hata wanawake weusi.

Ni Udhalilishaji na Unyanyasaji wa kijinsia, umeonyesha wazi kuwa wewe ni mbaguzi wa rangi.

Kumbe ndo maana wanawake weupe weupe wanakula Mema ya nchi huku wachache weusi ukiwateua sababu ya Elimu zao?

Umewaumiza Kihisia, umewaumiza kiakili wanawake Weusi.

Hivi Leo mwalimu wa shule ya msingi atakuonaje?
Kwahiyo tulia hawezi kusikilizwa mana sura yake anafanana na meko
 
Wewe ni msemaji wa wanawake weusi?

Kutokana na chuki zenu zilizokithiri dhidi ya Rais wetu daima mmekalia kutafuta makosa! JPM naye ni binadamu kuna wakati anatania, anacheka. Hata kama anapenda wanawake weupe bado sio kosa kwa sababu kuwa na hisia sio jinai.

Hata mueneze vipi chuki dhidi ya JPM bado tupo watanzania kwa mamilioni tunaompenda sana JPM na tutaendelea kumpenda.

Rsis amefanya mengi mno mazuri (classic) kwa watanzania na hata dunia na kazi zake daima zitabakia kuwa rejea hata baada ya yeye kuondoka madarakani, mataifa mengi wanamjua wanamadmire wanamuiga staili yake ya kutatua changamoto na kusukuma maendeleo. Mfano ugonjwa wa COVID 19 dunia nzima yeye ndio kiongozi pekee wa mfano aliyefanikiwa kuutokomeza.

Endelea kujidanganya kuwa unaweza kumpandikizia chuki kwa wananchi, labda kwa majizi na mafisadi wa fedha za umma na waliokuwa wananufaika nazo.

Subiri tarehe 28/10 mnanyolewa mapema bila maji kwa ushindi wake wa kishindo .
Weka mpaka, sema kakufanyia mambo mengi mazuri. Wengi wananchi hakuna ambaye hajaguswa na rungu la Magufuli. Tumbuatumbua, timua wenye vyeti fake(akiwaacha majeshi, wabunge na wateuli kama kina Makonda), teuzi za ukabila, vunja nyumba za watu bila fidia, vurugu za korosho na tumbaku, pombe za viroba, kuingilia Sheria ya vileo (muda wa kufungua bar), kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na mahakama, wasiojulikana kufanya yao, polisi kuruhusiwa kuchukua hela ya kiwi nk mk.
 
Tundu Lissu aanze kufunga mabegi arudi kweny Green card yake.Tuko Dar kesho na kesho kutwa tunachukua majimbo yetu.Tnawaacha mkiwa mrenda mrenda.Mlishindwa kutangaza sera kwa wana Dar es salaam mkabaki mkitukana TBC.Leo sera zimeuzwa na kiboko yenu JPM na jiji limepokea kupatiwa flyovers 6.kudadadadeki, Lissu alibaki kuuza matundu ya risasi 16.Hopeless presidential Candidate
Wana DSM wanakula sementi,kokoto na nondo? Wana DSM si wana Kongwa.
 
Yaaani watu mna shida nyie. Hivi Rais pale aliongea kwa utani tu tayari mmelibeba. Binadamu bhana ni shida sana

Au mnafikiri kwa vile ni Rais basi haruhusiwi kufanya utani?

Acheni ushamba kila kitu mnakishikia bango
Utakuwa mwanamke mweupe wewe si bure....[emoji41]
 
Huyu mpaka 2025 atakuwa anakosolewa na hao wakosoaji hakuna watakachoweza kubadilisha.

Hatuwezi kuwa na tabia zinazofanana na haitatokea tukaja kufanana. Ukishauelewa huo ukweli itakuwa rahisi maishani mwako kuishi na watu wasiofanana na wewe kitabia.
Kwa kuwa kila mtu ana tabia yake basi ndio uishi na mwizi mtaani kisa tu watu hatufanani?
Uishi na mbakaji kisa tu kila mtu na tabia zake?
Uishi na mchawi kisa tu ni kila mtu na maisha yake?
Uishi na muuaji jirani kisa tu kila mtu kaumbwa na hulka zake?
Ikifikia hatua hiyo,wewe si mtu hai tena,bali ni maiti inayoishi.
 
Back
Top Bottom