Rais Magufuli: Wasiotutakia mema wanatumia Asasi za Kiraia na NGO kutuhujumu ili kufifisha jitihada zetu kujikomboa kiuchumi kwa maslahi yao binafsi

Hii kitu inaitwa democracy ni mdudu mbaya kama virus wa ukimwi, Democracy ni dhana ambayo ukitumia ubongo vizuri kutafakari utagundua hakuna ukweli kwenye demokrasia. Hawezi kutekelezeka, na hakuna nchi imeweza kutekeleza... Ni imperialist manuva... Katika kuendeleza ukoloni Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

I dont is is ahout CCM..Well we can make right all all wrong we hage done.
 
Jamani naomba mnaojua mnisaidie na mimi kuelewa jambo hili ,hivi hizi figure pointing za Magufuli zimeshamsaidia yeye na nchi yetu kwa kiwango gani hadi sasa?
 
nchi inaliwa na wahindi. wafadhili wa kuu wa ccm.

anawasingizia wazungu.
 
Walituzushia Ebola ili watu wao wapate ajira. Na tungekubali upo wangeleta virusi vingi zaidi ili wagonjwa wawe wengi zaidi.mwisho wa siku wataleta dawa, wataleta vaccine, wataleta watu wao nawataomba Ela za tafiti. Janja ya beberu Ni kutumia majanga ya wengine kujinufaisha
 
Tuandamane au tufanyeje!! Mabeberu yanawajambisha Wachina,warusi, waajemi,wahindi sembuse sisi afrika akili ndogo ,,mkuu unajidanganya mchana kweupe tukubali hii dunia ni yao hivyo tushirikiane nao
Mzalendo ni shujaa ktk nchi yake
Mzalendo wakweli hakati tamaa
Ipo siku Africa itasimama pamoja pale mtazamo kama wako utakapo toweka ktk vichwa vya watu
Bora kumwaga damu ktk nchi yako kuliko kula pamoja na makafiri wa kibeberu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni miradi tunajenga kwa pesa zetu 'kwa mujibu ya maelezo ya JPM) sasa hujuma zinatoka wapi? Kuna mtu anataka kwenda kubomoa hiyo miradi? Tusisingizie hujuma kuwakandamiza watanzania wanaokosoa mwenendo wa serikali.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa muongo sana.
 
Mkirindi, Sasa ni vema kujiuliza, kwa nini ni Tanzania tuu mabeberu wanaiandama kama usemavyo? Na kwa nini muandamo huo umekuja baada ya Magufuli kuingia madarakani? Hakika Tanzania ya sasa ni kama peponi kiasi cha kuonewa wivu namna hii na wazungu.

Lakini wazungu hao hao ndio bado wanawaponya watu wetu wakiwapo viongozi kwa msaada wa ARV wanazokunywa kwa siri. Deni la taifa ndio limekuwa kwa kasi sana miaka hii minne ikimaanisha ndio tumekopeshwa sana na hao wanaoyuchukia?

Zipo dalili kuwa MALALAMIKO haya ya kila siku na namna ya kutafuta mahali pa kutupia lawama mambo tunayoshindwa kutekeleza au tunayoharibu.

Na usanii mkubwa sana unaofanywa hapa ni pale Rais awapo na watu wa WB, IMF, WHO na mashirika au mabalozi wa kimataifa kutumia lugha ya kuwashukuru sana kwa misaada na mahusiano mazuri lakini wakiondoka na akizungumza na sisi kwa kiswahili ni kuwaponda na kuwalaumu sana kuwa wanatukwamisha.

Mbona ndimi zinakuwa mbili? Hatari ni kuwa hata tukizungumza kiswahili hao "mabeberu" wanakuja kupata tafsiri yumeongea nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi huwa hatuli Utawala Bora au Demokrasia bali tunaitaji Maendeleo kwa uhalisia,Elimu,Afya,Miundombinu,Masoko kwa wakulima wetu,ajira kwa vijana ,Usimamizi mzuri wa rasilimali zetu na mengineyo mengi tu ambayo Mh Rais Magufuli ametekeleza kwa 100% na bado anaendeleza guludumu la Maendeleo Nchini. Viva Rais JPM!Viva Tanzania!Viva wale wote wenye dhamira njema na Taifa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alex Fredrick,

Naunga mkono hoja,
hakuna namna yeyote mabeberu watataka mtu mweusi awe na maendeleo bila wao kufaidi kwa kumnyonya,marekani inainyonya Japan kwa miaka nenda rudi,marekani inanyonya nchi za kiarabu miaka nenda rudi,nakadhalika.

Kubwa la kufanya watanzania ni kuendelea kumuunga mkono Raisi wetu na kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidiii na kuwaombea viongozi wetu.
 
Huku kunyooshea kidole watu wa nje kila wakati ni sawa na mtu anayeamini ulozi.
Kuna watu wanaogopa hata kununua baiskeli au kujenga kajumba ka kisasa kwa kusingizia wachawi.
Suala hapa ni kupambana na kuzingatia misingi ya haki, demokrasia na utawala wa sheria.
Nchi zilizopitia ujamaa zina shida sana kila wakati wana hofu ya mabeberu huku wenyewe ni mabeberu kwa watu wao.
Mabibi na mababu husingiziwa sana uchawi japo wana mchango mkubwa kwetu. Tuchape kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia ikiwezekana weka na vifungu vya biblia kuanzia mwanzo hadi kitabu cha samwel wa kwanza. Nchi ya Israel iliongozwa na Mungu mwenyewe lakini yaliyotokea bado tunashangaa waliwezaje kwenda kinyume?
 
Magufuli anaongoza kutuuwa kwa kimawazo kila nisikiapo ahadi zake za miradi ya maendeleo unaweza usifikiri kabisa... Check maisha ya watu wangapi yatabadilika kupitia utekelezaji wa Hotuba hii ya JPM hakika itauwa maisha duni ya watu wengi Sana..

 
Magufuli anaongoza kutuuwa kwa kimawazo kila nisikiapo ahadi zake za miradi ya maendeleo unaweza usifikiri kabisa... Check maisha ya watu wangapi yatabadilika kupitia utekelezaji wa Hotuba hii ya JPM hakika itauwa maisha duni ya watu wengi Sana..

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…