Rais Magufuli: Wasiotutakia mema wanatumia Asasi za Kiraia na NGO kutuhujumu ili kufifisha jitihada zetu kujikomboa kiuchumi kwa maslahi yao binafsi

Rais Magufuli: Wasiotutakia mema wanatumia Asasi za Kiraia na NGO kutuhujumu ili kufifisha jitihada zetu kujikomboa kiuchumi kwa maslahi yao binafsi

Hii kitu inaitwa democracy ni mdudu mbaya kama virus wa ukimwi, Democracy ni dhana ambayo ukitumia ubongo vizuri kutafakari utagundua hakuna ukweli kwenye demokrasia. Hawezi kutekelezeka, na hakuna nchi imeweza kutekeleza... Ni imperialist manuva... Katika kuendeleza ukoloni Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini kila azungumzapo yeye ni kulialia tunahujumiwa, hatupendwi, mabeberu wanatuonea nk nk?
Hivi tuna nini sisi hapa duniani kilicho cha kipekee hadi tushambuliwe kiasi hicho?
Tumeharibu biashara wenyewe, tumeua kilimo cha biashara chenye kuweza kubadili maisha ya watu wetu wenyewe na tumevunja mahusiano ya kijamii na kikanda kwa ubaguzi tulio anzisha wenyewe halafu tunatupia lawama za kilaghai kwa wengine?
CCM mtaacha lini usanii?

Sent using Jamii Forums mobile app

I dont is is ahout CCM..Well we can make right all all wrong we hage done.
 
Kuna hujuma dhidi ya jitihada za Serikali zinazofanywa na baadhi ya wasioitakia mema Tanzania zikilenga kufifisha jitihada zetu za kujikomboa, kiuchumi kwa maslahi yao binafsi, kamwe hawataki kuona tunadhibiti rasilimali walizokuwa wakivuna na kusafirisha bila kuulizwa.

Wanaotuhujumu hawatakubali tutekeleze miradi ya kimapinduzi itakayoharakisha maendeleo, ikiwemo Bwawa la Nyerere, SGR au Kufufua Shirika la ATCL, wasingependa tutoe elimu bure n.k, wangependa tuendelee kuwategemea wao, ilihali wao wanaishi kwa kutegemea rasilimali zetu.

Wanatumia kila njia kufifisha jitihada zetu na kupenyeza ajenda zao,muda mwingine wanatumia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kujifanya wanatufundisha Demokrasia na Haki za Binadamu, ilihali wenyewe wanavunja misingi hiyo kwa kujenga mifumo ya kinyonyaji.

Wanajifanya wanatufundisha Demokrasia ilihali wenyewe wanachochea machafuko na kuingilia uhuru wa Mataifa mengine, wanajenga hadi mazingira ya taharuki na kusema EBOLA imeingia Tanzania ili ionekane Nchi haiko salama, tusiposimama imara na kujenga uzalendo hatuwezi kushinda.

View attachment 1290479
Jamani naomba mnaojua mnisaidie na mimi kuelewa jambo hili ,hivi hizi figure pointing za Magufuli zimeshamsaidia yeye na nchi yetu kwa kiwango gani hadi sasa?
 
nchi inaliwa na wahindi. wafadhili wa kuu wa ccm.

anawasingizia wazungu.
 
Walituzushia Ebola ili watu wao wapate ajira. Na tungekubali upo wangeleta virusi vingi zaidi ili wagonjwa wawe wengi zaidi.mwisho wa siku wataleta dawa, wataleta vaccine, wataleta watu wao nawataomba Ela za tafiti. Janja ya beberu Ni kutumia majanga ya wengine kujinufaisha
 
Tuandamane au tufanyeje!! Mabeberu yanawajambisha Wachina,warusi, waajemi,wahindi sembuse sisi afrika akili ndogo ,,mkuu unajidanganya mchana kweupe tukubali hii dunia ni yao hivyo tushirikiane nao
Mzalendo ni shujaa ktk nchi yake
Mzalendo wakweli hakati tamaa
Ipo siku Africa itasimama pamoja pale mtazamo kama wako utakapo toweka ktk vichwa vya watu
Bora kumwaga damu ktk nchi yako kuliko kula pamoja na makafiri wa kibeberu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni miradi tunajenga kwa pesa zetu 'kwa mujibu ya maelezo ya JPM) sasa hujuma zinatoka wapi? Kuna mtu anataka kwenda kubomoa hiyo miradi? Tusisingizie hujuma kuwakandamiza watanzania wanaokosoa mwenendo wa serikali.
“Kuna hujuma dhidi ya jitihada za Serikali zinazofanywa na baadhi ya wasioitakia mema Tanzania zikilenga kufifisha jitihada zetu za kujikomboa, kiuchumi kwa maslahi yao binafsi, kamwe hawataki kuona tunadhibiti rasilimali walizokuwa wakivuna na kusafirisha bila kuulizwa-JPM
_
“Wanaotuhujumu hawatakubali tutekeleze miradi ya kimapinduzi itakayoharakisha maendeleo, ikiwemo Bwawa la Nyerere, SGR au Kufufua Shirika la ATCL, wasingependa tutoe elimu bure n.k, wangependa tuendelee kuwategemea wao, ilihali wao wanaishi kwa kutegemea rasilimali zetu”-JPM
_
“Wanatumia kila njia kufifisha jitihada zetu na kupenyeza ajenda zao,muda mwingine wanatumia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kujifanya wanatufundisha Demokrasia na Haki za Binadamu, ilihali wenyewe wanavunja misingi hiyo kwa kujenga mifumo ya kinyonyaji”-JPM
_
“Wanajifanya wanatufundisha Demokrasia ilihali wenyewe wanachochea machafuko na kuingilia uhuru wa Mataifa mengine, wanajenga hadi mazingira ya taharuki na kusema EBOLA imeingia Tanzania ili ionekane Nchi haiko salama, tusiposimama imara na kujenga uzalendo hatuwezi kushinda”-JPM
#JPMMwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waingereza walimshawishi Iddi Amin ampindue Obote hatimaye tuliona yaliyotokea, na wakamshawishi Nyerere aivamie Uganda, wakatutelekeza peke yetu, hadi uchumi wetu ukaharibika.

Leo hii wanatumia NGO na WHO kutudhibiti kwa kutumia chanjo za Polia na maradhi mengineyo, huku wachanganya dawa za kufunga uzazi, tuzizaane.

Kuna mengi yanafanywa tusiendele na wazidi kutudhibiti.


Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa muongo sana.
 
Mkirindi, Sasa ni vema kujiuliza, kwa nini ni Tanzania tuu mabeberu wanaiandama kama usemavyo? Na kwa nini muandamo huo umekuja baada ya Magufuli kuingia madarakani? Hakika Tanzania ya sasa ni kama peponi kiasi cha kuonewa wivu namna hii na wazungu.

Lakini wazungu hao hao ndio bado wanawaponya watu wetu wakiwapo viongozi kwa msaada wa ARV wanazokunywa kwa siri. Deni la taifa ndio limekuwa kwa kasi sana miaka hii minne ikimaanisha ndio tumekopeshwa sana na hao wanaoyuchukia?

Zipo dalili kuwa MALALAMIKO haya ya kila siku na namna ya kutafuta mahali pa kutupia lawama mambo tunayoshindwa kutekeleza au tunayoharibu.

Na usanii mkubwa sana unaofanywa hapa ni pale Rais awapo na watu wa WB, IMF, WHO na mashirika au mabalozi wa kimataifa kutumia lugha ya kuwashukuru sana kwa misaada na mahusiano mazuri lakini wakiondoka na akizungumza na sisi kwa kiswahili ni kuwaponda na kuwalaumu sana kuwa wanatukwamisha.

Mbona ndimi zinakuwa mbili? Hatari ni kuwa hata tukizungumza kiswahili hao "mabeberu" wanakuja kupata tafsiri yumeongea nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi huwa hatuli Utawala Bora au Demokrasia bali tunaitaji Maendeleo kwa uhalisia,Elimu,Afya,Miundombinu,Masoko kwa wakulima wetu,ajira kwa vijana ,Usimamizi mzuri wa rasilimali zetu na mengineyo mengi tu ambayo Mh Rais Magufuli ametekeleza kwa 100% na bado anaendeleza guludumu la Maendeleo Nchini. Viva Rais JPM!Viva Tanzania!Viva wale wote wenye dhamira njema na Taifa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alex Fredrick,

Naunga mkono hoja,
hakuna namna yeyote mabeberu watataka mtu mweusi awe na maendeleo bila wao kufaidi kwa kumnyonya,marekani inainyonya Japan kwa miaka nenda rudi,marekani inanyonya nchi za kiarabu miaka nenda rudi,nakadhalika.

Kubwa la kufanya watanzania ni kuendelea kumuunga mkono Raisi wetu na kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidiii na kuwaombea viongozi wetu.
 
Huku kunyooshea kidole watu wa nje kila wakati ni sawa na mtu anayeamini ulozi.
Kuna watu wanaogopa hata kununua baiskeli au kujenga kajumba ka kisasa kwa kusingizia wachawi.
Suala hapa ni kupambana na kuzingatia misingi ya haki, demokrasia na utawala wa sheria.
Nchi zilizopitia ujamaa zina shida sana kila wakati wana hofu ya mabeberu huku wenyewe ni mabeberu kwa watu wao.
Mabibi na mababu husingiziwa sana uchawi japo wana mchango mkubwa kwetu. Tuchape kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
On the contrary kauli za namna hii si za kizalendo bali ni kibaguzi na kugawa watu, ionekane kuna kundi fulani ndiyo linaipenda nchi na lingine linahujumu nchi. Hii si kweli, when i read between lines anataka kuwafanyia ubaya kundi fulani la watu kwa kisingizio cha uzalendo.

Hakuna mtanzania asiyeipenda nchi yake, wanaokosoa wanakosoa ili taifa lisonge mbele na hii ni kawaida kwa mtu yeyote aliyepitia development studies misuguano ni jambo la kawaida. Na kwa waliosoma physics they know that there is no movement without friction. We unataka kuongoza nchi ambayo watu wametulia kama maji ya mtungi we ni nani? hakuna nchi ya hivyo, ajifunze kupanua kifua cha kupokea anayoyataka na asiyoyataka. That is what leadership entails.
Pia ikiwezekana weka na vifungu vya biblia kuanzia mwanzo hadi kitabu cha samwel wa kwanza. Nchi ya Israel iliongozwa na Mungu mwenyewe lakini yaliyotokea bado tunashangaa waliwezaje kwenda kinyume?
 
Magufuli anaongoza kutuuwa kwa kimawazo kila nisikiapo ahadi zake za miradi ya maendeleo unaweza usifikiri kabisa... Check maisha ya watu wangapi yatabadilika kupitia utekelezaji wa Hotuba hii ya JPM hakika itauwa maisha duni ya watu wengi Sana..

 
Magufuli anaongoza kutuuwa kwa kimawazo kila nisikiapo ahadi zake za miradi ya maendeleo unaweza usifikiri kabisa... Check maisha ya watu wangapi yatabadilika kupitia utekelezaji wa Hotuba hii ya JPM hakika itauwa maisha duni ya watu wengi Sana..

 
Back
Top Bottom