Kuna hujuma dhidi ya jitihada za Serikali zinazofanywa na baadhi ya wasioitakia mema Tanzania zikilenga kufifisha jitihada zetu za kujikomboa, kiuchumi kwa maslahi yao binafsi, kamwe hawataki kuona tunadhibiti rasilimali walizokuwa wakivuna na kusafirisha bila kuulizwa.
Wanaotuhujumu hawatakubali tutekeleze miradi ya kimapinduzi itakayoharakisha maendeleo, ikiwemo Bwawa la Nyerere, SGR au Kufufua Shirika la ATCL, wasingependa tutoe elimu bure n.k, wangependa tuendelee kuwategemea wao, ilihali wao wanaishi kwa kutegemea rasilimali zetu.
Wanatumia kila njia kufifisha jitihada zetu na kupenyeza ajenda zao,muda mwingine wanatumia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kujifanya wanatufundisha Demokrasia na Haki za Binadamu, ilihali wenyewe wanavunja misingi hiyo kwa kujenga mifumo ya kinyonyaji.
Wanajifanya wanatufundisha Demokrasia ilihali wenyewe wanachochea machafuko na kuingilia uhuru wa Mataifa mengine, wanajenga hadi mazingira ya taharuki na kusema EBOLA imeingia Tanzania ili ionekane Nchi haiko salama, tusiposimama imara na kujenga uzalendo hatuwezi kushinda.
View attachment 1290479