Akili au hisia hivi vyote vina nafasi katika mtu.
Ni vigumu hisia kupambanua akili. Suala la uchumi linategemea kwanza mfumo.
Kimsingi mfumo una chaonzo chake katika familia.
Suala la kujiuliza:mfumo wa familia zetu ukoje?
Kwa mfumo wa familia zetu, suala la uchumi linawezekana?
Ni vigumu Tanzania kupata maendeleo kwa mfumo huu tulionao kuanzia kwenye familia, vyama vya siasa mpaka kwenye serikali.
Kinachofanyika ukiacha akili ukatumia hisia utaona ni maendeleo.
Kuhusu viongozi na raia: viongozi wanaongoza nchi zetu ama hawajui jamii yao, mifumo yake na ya dunia. Au wanajua mifumo ya jamii yao na ya dunia, lakini wanatekeleza dhamira zao.
Raia vivyo hivyo, kwa kutokuwa na uelewa na elimu ya mambo hawawezi kujua yapi ni maendeleo na yapi sio maendeleo!
Kwa sababu raia hawana uelewa na elimu ya mambo, wanadanganywa kuwa kufikia au kupata maendeleo lazima muumie wengine wanufaike. Mawazo potofu kabisa!