Rais Mama Samia Suluhu asipokuwa makini 2025 CCM itaondolewa madarakani

Tuko makini sana mkuu na hawa wanasaccos mitandaoni hawana kitu hawa! Sisi tunajua sehemu ya watz ni mitaani walioko wapiga kura.
Yaani sijawahi kuona majitu mazuzu kama haya ya upinzani.

Ni mamtu rahisi sana kuyadhibiti.

Yaani sasa hivi Mama Samia ayaue tu kwa kindness na kuongea kwa upole.

Akifanya hivyo yatasahau hadi habari za katiba mpya na tume huru.

Kikwete aliziitaga kelele zao upepo. Unavuma na kupita fyuuuu.

🤣🤣🤣
 
Kauli mbiu ya kila mwenyekiti wa sisiemu ni CHAMA HAKINIFII MIMI...
 

Mkuuu kiukweli tutakuwa hatuna Jinsi,Mungu keshamchukua Jembe letu hawa jamaa wanamshangilia mama kila uchwao, kigogo na Mange kimambi wanamuunga mkono,wanamshangilia wapo upande wake na wanamtumia mimemsg ya kumpongeza kila mara.....
Mama anatakiwa kuwa makini sana mana anaweza kuandika historia mbili katika maisha ya kesho
1:kwanza kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Taifa kama mwanamke
2: Rais wa kwanza chama kufia Mikononi make.
Kwakweli inauma sana
 
Wapinzani huwa wanasifia jambo lenye manufaa kwa taifa... nadhani hata wewe ukiamua kutumia akili yako utaona hilo.
 
Naona watu sasa hivi wqnashindana tu kutabiri.
 
Ccm na chadema wote walikuwa hawaipendi ccm. Ss utawala umebadilika wote wana furahia.

Ccm wanafurahi kurudi kwa ccm na chadema wanafurahi kurudi kwa uhafadhali wa uhuru wa kupigana na ccm.
 
Mimi siipendi CCM ila mama akiwa mtenda haki nampa kura yangu nikiwa hai
 
Ww ndo huujui upinzani wa TZ. Kwa Asilimia kubwa hawataki kuchukua nchi sababu hawako tayari kupigania hilo.

Wanachotaka ni ushindani wa kisiasa na wawakilishi bungeni jambo ambalo walinyimwa awamu iliyopita. Utawala umebadilika lazima wafurahi sababu wana matumaini kuwa watapata nafasi tena.
 
Ww ndo huujui upinzani wa TZ. Kwa Asilimia kubwa hawataki kuchukua nchi sababu hawako tayari kupigania hilo.
“Hawataki kuchukua nchi sababu hawako tayari”.

That sums it all up.
 
Hii kitu ikanifanya nitenge muda kutafakari why?,.Tangu lini mtu wa CHADEMA akasifia utendaji kazi wa kiongozi wa CCM
Chadema ni watu wasiojielewa
Hata Magufuli alipoingia madarakani,walimpongeza na kusema kaiba Sera zao
Huyu Samia watamtukana sana,subiri tu
 
Katiba haina kipengele kinasema CCM itaongoza milele,Uimara wa viongozi unafanya CCM iendelee kuwa madarakani.So mama akikosa msimamo na kucheza ngoma ya Upinzani makwisha
Upinzani ndio huimba ngoma ya ccm
 
Magufuli atarudi tena madarakani muda utaongea
 
Ni sawa na mende kuangusha kabati ulisikia wapi hiyo.
Hata ccm iwe nyepesi kama unyoya hakuna upinzani wa kuitoa madarakani, labida ccm isambaratike vipande vipande.
Kwa hiyo kwa kufanya hivyo anapata faida nani na anakomolewa nani?
 
Safi mkuu, nafurahi sasa umeacha kushabikia kina belgiji na kuiona ccm iliyosalama zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…