Hakika hizi mbinu zao za kupeleka miswada ya hati za dharura ya sheria za ukandamizaji zitafeli tuu.......Hakuna atakayejificha
Mbona nyinyi kila kukicha mnajitahidi kupeleka kwa hati za dharura, miswada ya sheria za hovyo hovyo za ukandamizaji hapa nchini?T14 Ambast: 35873858 said:Sina neno zaidi ya kusema huyu rais kakurupuka vibaya mno. Huwezi kuja mbiombio ndani ya masaa 24 unafumua mfumo kwa ghafla hivyo, hiyo ni nchi wala sio kama chama cha mpira. Nchi ina systems na hazibadiliki ghafla bali zinabadilika taratibu kuachana na mazoea mabovu yaliyokuwepo.
China alipoingia Deng Xiaoping alikuwa anapinga ujinga uliofanywa na kina Mao Zedong lakini hakufanya haraka hivyo, USSR alipoingia Nikita Kruschev alijipanga kabla ya kuanza kumpinga Stalin ambaye alikuwa ashakufa.
Ni kama vile ana kisirani na kisasi, kama vile kaja kukomoa mtu. Mabadiliko hayaji kama mapinduzi yanatakiwa kuja hatua kwa hatua.
Tumepokea taarifa kutoka Malawi, kuwa kiongozi mpya aliyechaguliwa kwa kura nyingi katika kura za marejeo, Lazarus Chakwera, katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, ndani ya saa 24, tokea aapishwe, ameondoa kinga ya kutoshtakiwa, aliyokuwa amejiwekea, kiongozi anayeondoka madarakani, Peter Mutharika.
Tunajifunza nini kwa hatua hiyo iliyochukuliwa na kiongozi huyo mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera?
Kama Taifa tunachopaswa kujifunza, ni kuona uongozi ni kama dhamana ambayo tumepewa na wananchi, ambapo tunapaswa tujinyenyekeze kwa wananchi wote na tuwatumikie kwa usawa, hao wananchi waliotupa dhamana hiyo tuliyo nayo na tunapaswa tutekeleze majukumu yetu, kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, bila kuwaonea raia kwa kutumia vyombo vya dola, ambavyo tunaamini kuwa sisi ndiyo tunaovimiliki.
Viongozi wetu pia wanapaswa waache mara moja tabia wanayoiendekeza ya kila kukicha, kupeleka Bungeni miswada mipya ya sheria za ukandamizaji na kujiwekea kinga ya kutoshtakiwa, kama vile wao ndiyo watakaodumu milele madarakani!
Wanapaswa pia kufikiri upya, kama hatua yao ya kupeleka muswada kwa hati ya dharura, kwa viongozi kama vile kuwawekea kinga ya kutoshtakiwa, Spika wa Bunge, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu, kama uamuzi huo ulikuwa wa busara.
Ni lazima tujue kuwa ukandamizaji unaozidi kupita kiasi hapa nchini, hautadumu milele, kwa hiyo ni vyema viongozi wetu wakatekeleza majukumu yao kwa haki na kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kwani ndiyo kinga pekee ya kudumu, itakayowaacha salama, hata watakapotoka madarakani.
Hio ni Safi sana mkuu.Masaa mawili yanatosha kutengua hiyo sheria, wala siyo kazi kama vile watu wanavyoaminishwa.
Kutesa kwa zamu.Huyu Raisi mpya anataka kuleta machafuko tu Malawi kipengele cha Raisi anayeondoka madarakani kutoshitakiwa kiko kwenye katiba ya nchi kukibadilisha inatakiwa katiba ibadilishwe kwanza na uwezo huo kama Raisi hana ni bunge na kura za maoni za wananchi ndio zaweza kakosea kukifuta hana huo ubavu wa kuvunja katiba wazi wazi!!!
kifungu hicho cha katiba ya malawi namba 91 hiki hapa nanukuu
91. Immunity
1. No person holding the office of President or performing the functions of
President may be sued in any civil proceedings but the office of President shall
not be immune to orders of the courts concerning rights and duties under this
Constitution.
2. No person holding the office of President shall be charged with any criminal
offence in any court during his term of office.
3. After a person has vacated the office of President, he or she shall not be
personally liable for acts done in an official capacity during his or her term of
office but shall not otherwise be immune.
Hiyo sheria aliiweka yeye au ilitungwa na bunge?
Yeye kama yeye anawezaje kubadili katiba ambayo imetungwa na bunge, kwa hiyo yeye yupo juu ya katiba?
Cha kujifunza ni kuwa ama ana papara ama kuna 'kundi' lenye nguvu lililomuweka hapo na linataka afanye linavyotaka bila yeye kufikiria madhara yatakayompata na wananchi kwa ujumla. Kama na mihemuko aache...na kutulizana kwanza asubiri kimbunga kipite.
Wasio na akili ni pamoja na wewe unayetaka tujifunze mambo ya nchi nyingine wakati sisi ni sisi.
Mbona nyinyi kila kukicha mnajitahidi kupeleka kwa hati za dharura, miswada ya sheria za hovyo hovyo za ukandamizaji hapa nchini?
Hivi kwa mfano mlipopeleka sheria ya kuongeza list ya wale ambao hamtaki washitakiwe, wakiwemo Spika wa Bunge, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu, kwenu nyinyi mliona mmefanya sawa?
Hivi ameondoa kinga ya APM kutokushitakiwa au ameondoa ya rais kutokushitakiwa?Cha kujifunza hapa ni kwamba viongozi wetu wa kiafrica wamejaa chuki na visasi... Angepeleka muswada bungeni iwe sheria kwa rais yeyote atakàeingia madarakani siyo kumtarget mpinzan wako tu
Kama wewe ni wewe na hujifunzi hata Yale mazuri au mabaya yanayomtokea jirani yako Basi wewe utawa maitiWasio na akili ni pamoja na wewe unayetaka tujifunze mambo ya nchi nyingine wakati sisi ni sisi.
Sina neno zaidi ya kusema huyu rais kakurupuka vibaya mno. Huwezi kuja mbiombio ndani ya masaa 24 unafumua mfumo kwa ghafla hivyo, hiyo ni nchi wala sio kama chama cha mpira. Nchi ina systems na hazibadiliki ghafla bali zinabadilika taratibu kuachana na mazoea mabovu yaliyokuwepo.
China alipoingia Deng Xiaoping alikuwa anapinga ujinga uliofanywa na kina Mao Zedong lakini hakufanya haraka hivyo, USSR alipoingia Nikita Kruschev alijipanga kabla ya kuanza kumpinga Stalin ambaye alikuwa ashakufa.
Ni kama vile ana kisirani na kisasi, kama vile kaja kukomoa mtu. Mabadiliko hayaji kama mapinduzi yanatakiwa kuja hatua kwa hatua.
Wasio na akili ni pamoja na wewe unayetaka tujifunze mambo ya nchi nyingine wakati sisi ni sisi.
Katiba yao inamruhusu kufanya hivo hata hapa ni hivyohivyo mambo ya bunge yanakuja baadae.Hiyo sheria aliiweka yeye au ilitungwa na bunge?
Yeye kama yeye anawezaje kubadili katiba ambayo imetungwa na bunge, kwa hiyo yeye yupo juu ya katiba?
Hiyo sheria aliiweka yeye au ilitungwa na bunge?
Yeye kama yeye anawezaje kubadili katiba ambayo imetungwa na bunge, kwa hiyo yeye yupo juu ya katiba?
Cha kujifunza hapa ni kwamba viongozi wetu wa kiafrica wamejaa chuki na visasi... Angepeleka muswada bungeni iwe sheria kwa rais yeyote atakàeingia madarakani siyo kumtarget mpinzan wako tu