Rais mteule wa Kenya William Ruto ni mtu wa aina gani? Tanzania itegemee nini kutoka kwake?

Rais mteule wa Kenya William Ruto ni mtu wa aina gani? Tanzania itegemee nini kutoka kwake?

Mtegemee jino kwa jino. Uhamasa utaongezeka kwasababu si mtu wa kupenda Amani na hekima. Issues zikitokea usitegemee atakuja kuwapigia magoti au kumaliza Mambo kwa hekima, project nyingi zinazokuja ukanda huu na utalii pia mtegemee fitina. Ni mtu wa maneno matamu lakini nyuma yake ni mtu wa fitina Sana. Kenyatta alijitahidi Sana kuwa na hekima na mkweli. Tunza hii message iko siku utakuja kuelewa nachoandika.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ruto ni mtu hatari sana. Halafu ni fisadi mno ana utajiri mwingi wa ghafla. Pia msaidizi wake Gachagua ni hatari na fisadi mno.

Hebu jiulize pesa za kukiendesha chama cha UDA kwenye kampeni na gharama zote. Hiyo pesa kaitoa wapi? Chanzo cha mapato cha utajiri mwingi wake ni upi? Au familia ya Moi ndio imempa hela? Jamaa pesa hiyo aliyotumia kwenye siasa atairudishaje?

Msijidanganye na tabia yake ya kuomba. Watu wengi wanaojifanya ni watakatifu na watu wa maombi huwa ni watu hatari sana.

Muda utazungumza.
 
Kauli ya kijasiri sana hii. Uhalisia TZ masikini ni wengi sana

kuwa tajiri haina maana una nguvu.

ndio maana tunahubiriwa aiasa za kujitegemea africa,kaka bara hatuma kabisa sera hizo.tunaahinda tukiomba omba na kukopa kopa kushindwa kulipa kila siku.
 
Tanzania haihitaji kutegemea hisani ya raisi yoyote wa nchi jirani.

Infact Tz ni nchi pekee inayoweza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Congo DR, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Comoro, Malawi, Zambia na Sudani ya kusini zote kwa pamoja na isiathirike pakubwa.

Tz ni nchi kubwa. Hakuna nchi nyingine yeyote kusini mwa jangwa la Sahara yenye uwezo huu.

Tz is the United State of Sub Sahara - Africa.
Jinsi ulivyoiongelea,natamani sana ingekuwa kubwa kiasi hiko.
 
Mtegemee jino kwa jino. Uhamasa utaongezeka kwasababu si mtu wa kupenda Amani na hekima. Issues zikitokea usitegemee atakuja kuwapigia magoti au kumaliza Mambo kwa hekima, project nyingi zinazokuja ukanda huu na utalii pia mtegemee fitina. Ni mtu wa maneno matamu lakini nyuma yake ni mtu wa fitina Sana. Kenyatta alijitahidi Sana kuwa na hekima na mkweli. Tunza hii message iko siku utakuja kuelewa nachoandika.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Umejitahidi kuzungumzia personalities zake.

Lakini yanapokuja mahusiano baina ya nchi na nchi it is very rare matakwa ya mtu binafsi yaka prevail.
 
Sijajua chini yake ushirikiano kwenye Jumuia ya Afrika mashariki itakuwaje, maana huyu jama ajiwa ana hasira huwa achagui maneno, aliwahi kuongea vibaya kuhusu DRC mpaka balozi wa Drc akaitisha wanahabari kumlaani kwa kutoa maneno yanayotdhihaki sovereignty ya nchi njingine
 
Ila jamaa atatawala nchi kwa mbinde sana,maana hiyo njaa waliyonayo Wakenya na yeye alisema atashusha Bei ya unga.
Alafu Baba naye akiamua kumchezesha sijui itakuaje?mwenzake Uhuru alikuwa na akili alijitahidi kumteka Baba na akamaliza ngwe yake salama,sasa ndugu Ruto anaomekana kwanza haelewani na Uhuru,rafiki wa karibu wa Baba na alafu Baba anaonekana hamkubali sana Ruto.
Ruto ana kazi kubwa sana,alafu Malofa wa Kenya Wana Imani naye kubwa sana,yeye anajiita "Hustler"!
 
Chicken seller
 
Kampein zake aliwaponda sana wawekezaji wa kichina. Kenya kwanza. Ujue Ruto kura nyingi kazipata kwa mama ntilie, boda boda na wafanyabiashara ndogondogo.
Maneno ya siasa usiwekwe kwa moyo utaumia, weka kwa mapafu ukitoa hewa inaenda nayo....ile hustler na wheelbarrow ilikuwa ni mbinu tu hakuna kitu atafanya....
 
kwa kifupi, vizuizi vingi Tz ilikuwa inapata katika bado zake na Ke, ni kutokana na yeye kwa sehemu kubwa!

sasa yeye ni Rais! sijajua ile issue ya Rostam itaishia vipi kule Mombasa ama atamtoaje!

Ngoja tuone! huenda focus ikabadilika pia!
 
Kwangu mimi naona hali mwanzo haitakuwa smooth kama ilivyokuwa kwa Kenyata kwani Kenyata alitumia sana soft power unlike huyu Roto ambae ni type ya solid man ila fisadi sana. I am sure siasa zake za kenya kwanza akizitekeleza inaweza kuwa ngumu kwa watanzania kufanya biashara Kenya. The bottom line is he can never ignore TZ, especially food, we are their food basket and now raw material for some of their factories.
 
Back
Top Bottom