View attachment 1425361
Cha ajabu kuna Watu wamefikiri huu ujumbe ameuelekeza Tanzania
View attachment 1425369
Mh. Rais yuko sahihi, kwamba Mungu hashughuliki na wajinga, ila hayuko sahihi kwa kusema Mungu yuko busy unless Mungu ana akili yenye upeo sawa na wa mwanadamu.
Sifa pekee za Mungu zinazomtofautisha na kiumbe kingine chochte kile ni hizi hapa:
1. Ni wa milele-hana mwanzo, hana mwisho.
2. Ni muumbaji- hakuna kiumbe kingine chenye uwezo huo.
3. Yupo kila mahali- hakipo kiumbe kingine ambacho kina uwezo wa kuwa kila mahali. Shetani amekuwa akiigiza tabia hiyo lakini yeye kama kiumbe ambaye ni "individual personality", hayupo kila mahali isipokuwa malaika zake tu ndiyo wametapaka kila mahali.
Shetani alikuwa malaika mbinguni na anaendelea kuwa malika hadi leo, ila aliyeasi, na hivyo malaika hana uwezo wa kuwa kila mahali. Tuchukulie kwa mfano siku Malaika Gabriel alivyotumwa na Mungu kwenda kwa Bikra Maria kumweleza kuwa atamzaa mtoto Yesu, wakati Malaika Gabriel akiwa anaongea na Mariam nyumbani kwake, malaika huyu hakuwepo mahali pengine popote duniani au mbinguni, except nyumbani kwa Mariam
4. Anajua yote
5. Anaweza yote
Na kwa post hii sasa, nashauri wale wote ambao wamekuwa wakisema kuwa Mungu hayupo, na kama yupo basi awaue, natoa wito sasa watu hao wajitokeze humu jukwaani, halafu wakiri tena maneno hayo sasa hivi,
Kiranga akiwa ni kiongozi wao. Wakikaa kimya nitashangaa sana. Wajitokeze sasa, huu ndiyo muda ambao wanaweza kuhakiksha vizuri sana tena very precisely!