Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Huku bara wanatimuliwa maeneo yao ya asili, na kule Zenji wanakatazwa kuvaa vitu vyao vya asili.
Huku bara wanasemekana wanaharibu ikolojia ya viumbe hai, na kule Zenji wanasemekana wanahatarisha amani ya wazanzibari.
😅
Kuna ka muunganiko flani ambako kanaonesha kweli huu muungano umeungana Kuwatokomeza wamasai
 
Ule ni utamaduni wa watu, mbona nyie mnakuja na kanzu zenu huku kwetu na wakati sisi ni wakristo?
Kanzu ni vazi takatifu,Yesu pia amevaa.Mapadiri,maaskofu,
Huku bara wanatimuliwa maeneo yao ya asili, na kule Zenji wanakatazwa kuvaa vitu vyao vya asili.
Huku bara wanasemekana wanaharibu ikolojia ya viumbe hai, na kule Zenji wanasemekana wanahatarisha amani ya wazanzinari.
😅
Hawa wamasai sio wabantu,ni wakutoka pembe ya Afrika.Na hao wenye asili ya pembe ya Afrika kama wasomali,waarabu,wa Ethiopia,wameacha mila za kutembea na silaha kama sime,visu,majambia,bakora na fimbo.Mila za kutembea na silaha ni hatarishi na zimepitwa na wakati.
 
Tatizo la wanaharakati wanadakia kila kitu, imradi waonekane na kusisikika
 
Upo sahihi kwa upande wako chief, ila utamaduni wa mtu ni jambo pana. Kuna watu leo hii wanasema mapenzi ya jinsia mbili yamepitwa na wakati 😅, zuio la ghafla kwa utamaduni wa mtu ni ukosefu wa adabu. Wapewe elimu taratibu watabadilika. Mfano mzuri ni kwenye ukeketaji
 
Mi ni mchagga na kwa nchi hii tuko kila mahali wengine tuna vibarua wengine hatuna tupo tu kuhangaika angalau kipatikane chochote kitu. Kusema wamasai wanazagaa ndio ubaguz wenyewe mkuu. Watu wengi wamezagaa kila mahali sema wewe unawaona wamasai zaid kwasababu ya mavaz yao nothing more bro. Wazanzibar kwa asili ni wabaguz pasee. Unaongea utafikir wamasai wamefika nchi hii jana. By the way unafikir kwanini wanazagaa. Ulishawah kujiuliza hilo swali? Nani mwenye jukumu la kuhakikisha raia wake wanaajiriwa au kusoma. Mmewatoa kwao kwa nguvu mmewatupa hapo tanga mazingira mapya hawajui chochote. wafugaji hawa life imekuwa ngumu wameamua kuja mjin kujitafuta halafu mwanaume mzima unasimama hapa unabana pua eti wamasai wamezagaa seriously. Halafu huyu mtu utamkuta msikitin anaswali. We unafikir kumtoa mtu ilipo kwa kwa asili ni Jambo jepes sio. Bro kama huna msaada kwa atleast nyamaza usiwaumize kwa kejeli zako.
 
Unataka Wazanzibar nao waanze kutembea wamebeba Majambia kama wa Oman wa kipindi kile?
Kwani wazanzibar ni waoman?? Wale ni wanyamwez..mwarabu alitia mimba tu kule wakatokea hao halfcasts, lkn wale ni watanganyika waliyoingia pale na mwingereza na mwarabu waliwakuta pale
 
Wamasai waondokane na ujinga wa miaka mingi na wakubali kubadilika kuendana na hulka za visiwani. Wabadilike wao sio serikali ya SMZ ibadilike kisa kulinda mila za wamasai, kama wao hawawezi kulinda mila na desturi zao hakuna wa kuwalindia hizo mila zao.

Unapokwenda kuishi kwa mtu jifunze zile hulka zake za kila siku ili uwe sehemu ya hapo nyumbani sio kwenda na tabia zako halafu ukikosolewa zinaanza kusikika kelele za muungano. Wapuuzi sana hao wamasai.
 
Hawezi fanya hivyo.

Ana muunnga mkono dada yake kuwatokomeza wamasai.
 
Mmeuza makazi yao ya asili Loliondo na Ngorongoro mkawafukuza , sasa wameamua kuhamia kizimkazi for good WAACHENI vinginevyo iacheni ngorongoro na loliondo yao
 
Hii nchi hakuna mwenye kwao wewe unaruhusiwa kuish popote kwa utamaduni wako. Nyie ndio wale waafrica mnaoamini ukivaa kizungu umeendelea.
 
Turuhusu watu watembee na sime eti ni utamaduni wao? Upuuzi gani huu?

Wamasai sio watu special kwenye nchi hii, waishi kwa mujibu wa taratibu kama watanzania wengine.

Kila siku wamasai ni tamaduni zao na blah blah kibao, kila mtu anatamaduni zake ila haziko juu ya sheria.
 
Ulishajiuliza kwanini wahadzabe wanawinda wanyama Pori na serikali haiwakamati Lakin ukiwinda wewe ni miaka 10.
 
Msitutoe nje ya reli,

Serikali ya Mwinyi Zanzibar inapitia Hali Tete.

Tueleze chanzo Cha mtikisiko kwenye baraza la mawaziri.
 
Ulishajiuliza kwanini wahadzabe wanawinda wanyama Pori na serikali haiwakamati Lakin ukiwinda wewe ni miaka 10.
Huu wote ni upumbavu tu, wote hao wanapaswa wachukuliwe hatua kama watanzania wengine.

Hatuwezi kuwa na sheria ambazo zinawabeba group la watu na zinakandamiza wengine.

Wasukuma ambalo ndilo kabila lenye watu wengi ufugaji ni sehemu ya utamaduni wao, ila wananyanyaswa kila kukicha na ng'ombe zao na wanaambiwa wauze mifugo yao Kwasababu hakuna sehemu za malisho. Ila kuna kabila limeachiwa hifadhi wanafuga bila kusumbuliwa na mamlaka.

Ifike mahali huu ujinga ufike kikomo na watanzania wote wawe na haki sawa
 
Ifike hatua huu ujinga tuuweke kando, tuishi wote kwa usawa kwa mujibu wa taratibu za nchi.

Kwa kisingizio cha utamaduni Leo hii kuna watu wanafanya uwindaji haramu, wanaua mamia ya wanyama kadri wanavyojisikia.

Ila kuna mtu anafungwa zaidi ya miaka 10 kwa kukutwa na nyamapori kilo moja.

Kwa kisingizio cha tamaduni watu wanatembea na siraha kali kama sime, ila wengine wakifanya hivyo wanakuwa wamekiuka taratibu za nchi.

Kwa kisingizio cha utamaduni watu wameachiwa hifadhi wafuge mifugo yao, ila wengine wanakosa malisho na mifugo yao inataifishwa na kupigwa mnada.

Kama mnaheshimu tamaduni za watu mbona hampigi kelele wakurya kukatazwa kukeketa? Ila mnapiga kelele wahadzabe wakinyooshewa kidole kwa uwindaji haramu? Ila mnapiga kelele wamasai wakikatazwa kutembea na siraha.
 
Wazanzibar ni wabaguzi sana, nimekuwa na routes kadhaa ila hawa jamaa hawatupendi kabisa watu wa Bara,hata ukiwa Zanzibar hujioni kama upo Tz, wakati huku kwetu wanazurula kama kuku wa kienyeji tu,kuna hatua tutaifikia kila mtu ataenda kwao
 
Ila bana, tuache utani, hizo sime kwa karne hii waachane nazo tu,
Kesho kutwa mm nikiwa natembe na AK47 mtaniruhusu kwa kuwa sipigi nayo mtu?
 
Tubadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…