Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Serikali ya mapinduzi inapotoshwa kwa hili la wamasai. Kuna chuki kubwa za kidini dhidi ya jamii Za watanganyika
Ila kwa ajili ya siasa watakanusha , wafute tangazo lao kimyakimya dhidi ya wamasai.
hakuna Chuki Ya Kidini Hapo Wametumia Vibaya Uhuru Walopewa Wangekatazwa Kabla Ya Kupiga Polisi Hapo Sawa
 
Bro mmasai mwenyewe ni kivutio cha kitalii. The way alivyovyaa tu tembea nchi za watu ndio utajua nachokuambia. Wazungu wanataka kitu unique mzee sio aje aone sawa na kwao
Sawa ila sime ile siku ikitokea kutoelewan huoni mauaji yanawez kutokea? Zile ni silaha halisi.
 
Eti wapemba na wao waache kuzaliana, cha msingi mmasai bila fimbo na sime yaani hajakamilika watafute njia nzuri ya kutatua swala hili ule ni utamafuni wao!!!
 
Kweli kabisa ndugu tunazunguka mitaani huko tunakutana nao wengine ni rafiki zetu mpaka ahatarishe usalama kama jinsi wanavyosema wenyewe wapemba ujue ulianzisha shari!!!
 
Nitajie faida 10 za Huu muungano adimu?

Ikiwezekana taja foida za muungano Kwa upande wa Bara!
Hayo mambo yanafundishwa shuleni kwenye somo la uraia, kama wewe unaona muungano hauna faida wache wenzako wanaojua faida zake, Ndugu zetu wa pwani, wamakonde na wasukuma wanakuwa hadi viongozi huko! sote tungerundikana huku ingekuwaje? wewe wa Ngara huwezi kuona faida kwa vile familia haina miaka mingi hapa nchini!
 
Wanawalazimisha wawe magaidi sasa
 
Na Zanzibar kama nini?

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Wawaelimishe kuacha utamaduni wao? We mzima? Kwani utamaduni wao ni sababu ya kukosa elimu? Kuna machizi mengi sana Tanzania.
Kuna mambo lazima yatabaki kama historia tu na kumbukumbu hayawezi kuendelea kwa muda mrefu. Ni suala la mfumo.

Kwani Suala la Tohara kimila kwa wamasai limeishia wapi? Walikuwa wakishakatwa wanatembea kwa makundi na fimbo na huruhusiwi kuwatazama usoni, ukiwatazama unachapwa. Umeshasikia hii tamaduni ikiwa maarufu tena kwenye miji mikubwa? Inajifia.

Kama wanajichanganya na dunia hii inayokwenda kwa kasi watu wanahamia kwenye AI, ni suala la muda tu wataadupt na kuna mambo yatabaki historia kuwa ilikuwa hivi. Kama huko USA tu red indian walivyobaki historia, walikuwa wanatembea na mishale.

Njia sahihi ni kuishi katika maeneo ambayo yanaruhusu mfumo wa tamaduni zao kama nje ya miji mikubwa, vijijini na maporini.
 
Acha kutetea ujinga. Unaruhusu vipi watu watembee na silaha katika nchi iliyostaarabika kama Zanzibar? Visu na marungu vya nini Zanzibar? Kama wanataka kutembea na visu na marungu yao warudi huku Bara ambako wamezoeleka na siyo kwenye nchi za watu.
 
Sawa ila sime ile siku ikitokea kutoelewan huoni mauaji yanawez kutokea? Zile ni silaha halisi.
Kwan mmasai ameaza kukaa na sime leo mzee. Hakuna watu poa kama wamasai hawana shida na mtu. Kingine mnatakiwa mzingatie hawa watu walikuwa wanaish porin huko bila shida mkaja kuwalazimisha kuhamia maeneo tofauti so hizo ndio athari zake. Na watajaa mijin balaa maana mmewatoa kwenye uhalisia jiandaein na gharama zake
 
Kwamiaka yote tangu kabla ya uhuru hadi leo, Jamii za Wamasai wapo Zanzibar na utamaduni wao wa visu/Sime na Fimbo,
siyo kweli kuwa wamasai walikuwepo zanzibar kabla ya uhuru , wameanza kufika zenj kwa kuanza kuuza madawa yaho kwenye miaka ya tisini.
 
siyo kweli kuwa wamasai walikuwepo zanzibar kabla ya uhuru , wameanza kufika zenj kwa kuanza kuuza madawa yaho kwenye miaka ya tisini.
So kwa muda wote huo wameua wangapi kwa hizo sime na marungu yao. Chuki ni ushetan kabisa
 
Rais anatakiwa kujua kua matumizi yoyote ya silaha yanakuja baada ya mtu kuonewa au kunyang'anywa haki yake na uvumiiivu ukafika mwisho.Hao masai wametumia nyenzo walizonazo kwasababu mojawapo kati ya hayo mawili kuna ambayo wamefanyiwa.Mimi sitembei na silaha yoyote zaidi ya akili yangu ila siwezi kukubali kua mnyonge kwa yoyote atakayetaka kunionea au kuninyima kile ninachoamini ni haki yangu lazima nijitete.Kwahiyo inawezekana hao masai nao wametumia kanuni hiyo hiyo.chakurekebisha ni jamii nzima iishi kwa haki badala ya kuwanyanyasa alafu muwanyang'anye wanachobeba kwasababu hiyo wala haisaidii endapo uonevu utaendelea, kwasababu mtu uonevu ukizidi silaha inaweza kua kitu chochote.
 
STOP THE GENOCIDE

Hivi watajisikiaje wakiambiwa waache kuvaa makobazi na Kanzu....tena utamaduni wa kuletwa, watajisikiaje?

Wanzanibari wanaweza kuacha kucheza mduara?

Wazanzibari wanaweza kuacha kula rojo?

Wanaweza kuacha supu la pweza?
Nyinyi waporipori msiojuwa historia ya nchi yetu mtatusumbua sana, tamaduni za kuvaa kanzu, makobadhi barakashia, kula ulojo na hata supu ya pweza zinahusisha pia tamaduni za watu wa pwani/waislamu huku kwetu ama 'MDUARA' sawa!
 
Acha kukuza mambo yaonekane makubwa.

Jambo la wamasai ni dogo sana na linatatulika.

Unataka ku score points za bure!

Serekali ipo kazini kitambo
 
Ule ni utamaduni wa watu, mbona nyie mnakuja na kanzu zenu huku kwetu na wakati sisi ni wakristo?
Acha kutuchafua, nchi hii hatuna 'mkristo' mjinga wa kushindwa kutambua kuwa, kanzu pia ni vazi la watu wa pwani/ Waislamu huku Tanganyika. unataka kutuambia akina Kikwete, january makamba, Kassim majaliwa na wengine walikuja kutoka zanzibar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…