Rais Mwinyi, tengua Amri haramu ya kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime Zanzibar. Inahatarisha Muungano!

Acha kutuchafua, nchi hii hatuna 'mkristo' mjinga wa kushindwa kutambua kuwa, kanzu pia ni vazi la watu wa pwani/ Waislamu huku Tanganyika. unataka kutuambia akina Kikwete, january makamba, Kassim majaliwa na wengine walikuja kutoka zanzibar?
Dada angu hii mada huiwezi wewe kaa pembeni
 
Mi ni mchagga na kwa nchi hii tuko kila mahali wengine tuna vibarua wengine hatuna tupo tu kuhangaika angalau kipatikane chochote kitu. Kusema wamasai wanazagaa ndio ubaguz wenyewe mkuu. Watu wengi wamezagaa kila mahali sema wewe unawaona wamasai zaid kwasababu ya mavaz yao nothing more bro. Wazanzibar kwa asili ni wabaguz pasee. Unaongea utafikir wamasai wamefika nchi hii jana. By the way unafikir kwanini wanazagaa. Ulishawah kujiuliza hilo swali? Nani mwenye jukumu la kuhakikisha raia wake wanaajiriwa au kusoma. Mmewatoa kwao kwa nguvu mmewatupa hapo tanga mazingira mapya hawajui chochote. wafugaji hawa life imekuwa ngumu wameamua kuja mjin kujitafuta halafu mwanaume mzima unasimama hapa unabana pua eti wamasai wamezagaa seriously. Halafu huyu mtu utamkuta msikitin anaswali. We unafikir kumtoa mtu ilipo kwa kwa asili ni Jambo jepes sio. Bro kama huna msaada kwa atleast nyamaza usiwaumize kwa kejeli zako.
kwanza kabisa mimi ni Msukuma, na pili hakina masaid alie lazimishwa kwenda ZNZ, wameenda kwa uamuzi wao. Na kama umefika ZNZ ndio utaelewa kuwa hawa MAsai ni kero. Sasa kama imekuuma sansa basi wapeke huko kwenu Moshi ukawape kazi
 
Ukimsikiliza ni chuki tu za kibaguzi. Eti kama wanataka kufanya biashara wafungue maduka na wasibebe sime wala marungu. Hiv nchi hii wamasai wamewakosea nini. Maana porin kwao wamefukuzwa na huku mjin wanakojitafuta hawatakiwi. Mnataka wafanye nini waende wapi.

Wakiendaga Europe hawatembei na rungu wala sime
 
Nina laani kwa nguvu zote kitendo cha vurugu za mgambo na watu wa jamii ya kimasai kwakupigana hadharani, Nina laani Masai kushambulia Mgambo, Nina laani kwa nguvu kubwa Mgambo wa Zanzibar kushanbulia watu wa jamii ya kimasai! Jambo hili halikubaliki kwa mjibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazokataza kupigana hadharani au kificho.

Lakini naomba nitofautiane na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Zanzibar, Amri kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime/visu vyao, Ni Kauli Haramu na ya kibaguzi inayohatarisha muungano wa Tangabyika na Zanzibar.

Ifahamike kuwa Fimbo na Sime kwa Jamii za kimasai ni sehemu ya “vazi lao la asili”, ni Sehemu ya utamaduni wao, Ni Identity yao, na hivyo kujaribu kwa aina yoyote kuondoa kimoja wapo katika hivyo vinavyokuwa ndani ya mwili wa Masai ni kutangaza kuwafukuza Wamasi Zanzibar, Hili ni tangazo la kijinga limekurupukwa na mamlaka za Zanzibar!

Kwamiaka yote tangu kabla ya uhuru hadi leo, Jamii za Wamasai wapo Zanzibar na utamaduni wao wa visu/Sime na Fimbo, hakujawahi kuwa hatari kwa raia yoyote, Kwanini iwe leo baada ya Masai kujihami waliposhambuliwa na mgambo wa mji? Serikali ya Rais @dr.hmwinyi itafute jawabu la kumaliza mzozo huu sio kufunika kwakuwafukuza Wamasai, Tatizo liko kwa mamlaka za jiji, Tatizo liko kwa Wakuu wa Mikoa, na mamlaka zingine za jiji.

Unawazuia Wamasai wasibebe fimbo unataka Wabebe Vikapu vya Nazi na vigemeo vya Litembo? Unataka wabebe Usinga? Unataka wabebe karafuu? Noooo nooo tukatae unyanyasaji huu kwa jamii ya kimasai! Ukamilifu wa Masai ni fimbo na sime. Sasa unaka awe na shuka tu kama dera?

Kesho yataibuka Bara Wapemba watashambuliwa, Je serikali iweke amri wapemba wasizaliane kwa Wingi Bara ambao ni sehemu ya utamaduni wao? Nooo Nooo! Tukatae ubaguzi huu.

Mh Rais @dr.hmwinyi ili kunusuri maafa zaidi na kuoondoa hii taswira mbaya ya ubaguzi iliyotengenezwa na mamlaka za mji hapo Unguja, Ninakuomba na kukusihi Mh Rais, tengua hii kauli ya kibaguzi, Haifai kutolewa na kiongozi wa serikali katika ulimwengu wa leo! Madhara yake ni makubwa zaidi mbeleni.

Serikali ijifunze kutatua migogo kwa hekima na busara, Majibu ya hasira ya kiserikali yanaweza kuleta maafa zaidi kuliko kutatua, Nimeisikiliza kauli ikitolewa na yule kiongozi wa mjinibZanzibar (Unguja) ni wazi alitawaliwa na ghadhabu zaidi kuliko hekima ya kiuongozi, Amewahukumu Wamasai bila kujaribu kujua undani na kutafuta jawabu, Badala yake ametafuta jibu ambalo ni la hovyo zaidi!,

Nimesikitika sana kwa kauli hii ya serikali ya Zanzibar katika zama hizi za utandawazi na utandaridhi! Utengamano wa taifa letu ni muhimu kuliko hizi chuki zinazokolezwa na namlaka za nchi!

Na Yericko Nyerere
View attachment 2890368
Hawatakiwi Ngorongoro hawatakiwi Znz baghosha!
 
Wamasai wanatembea na vifimbo zao kwa sababu ya kuchunga ngombe zao. Jee zanzibar huwa wanachunga ngombe? Acheni hoja za kitoto. Mambo yanabadilika.
senior-omani-man-wearing-the-traditional-khanjar-in-the-town-ibra-oman-2F8TCAF.jpg
portait-omani-man-nizwa-oman-may-traditional-outfit-wearing-khanjar-traditional-dagger-belt-73...jpg

Na hawa ma Bwana zako wanawinda nini?

Acheni kuwasimanga Wamasai wakati huohuo wakivaa wengine mnasema ni Suna takatifu ya Mtume.

Sime na Rungu la Mmasai ni Ceremonial.
 
Kila mtu ana haki ya kikatiba ya kujilinda (right to bear/ carry arms). Iwe rungu, panga au bunduki. Wamasai wanatumia haki yao kikatiba. Wasiguswe.
Screenshot_20240201-145504.jpg
 
Tippu-Tip-Autobiography-Early-and-Later-Life (1).jpg

Tippu Tip amevaa Jambiya kiunoni kwanini hamkumkataza wakati anawaleta kutoka Kindu na Ujiji?
 
Ukimsikiliza ni chuki tu za kibaguzi. Eti kama wanataka kufanya biashara wafungue maduka na wasibebe sime wala marungu. Hiv nchi hii wamasai wamewakosea nini. Maana porin kwao wamefukuzwa na huku mjin wanakojitafuta hawatakiwi. Mnataka wafanye nini waende wapi.
Naunga mkono hoja
 
Hii nchi hakuna mwenye kwao wewe unaruhusiwa kuish popote kwa utamaduni wako. Nyie ndio wale waafrica mnaoamini ukivaa kizungu umeendelea.
Heshimu mamlaka huwezi kuwa juu ya mamlaka na ukajiendea tu kipuuzi, wapo ndani wamasai tisa mpaka muda huu kwa ujinga huo wa kudhani sime ndio kila kitu.
 
Watanganyika tuna upole uliochanganya mpaka kufikia kilele cha ukilaza.

mfano:kwa ilo tukio la masai na polisi wa Zanzibar raia wa tz wangekua ndio raia wa South,Nigeria n,k wazanzibari wangechezea kichapo huku bara mpaka huo muungano ungejuta.
Tusingeweza! ikiwa sisi wenyewe tunashindwa hata kutofautisha nani 'mtanganyika' nani 'mzanzibari' tungeweza kweli bila ya kusababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe?

Baada ya miaka zaidi ya 60 ya uhuru hadi leo wapo wanaomini waisilamu wote, watu weupe wote, watu wa pwani wote waliopo Tanganyika ni Wazanzibari na kuna mtoa maoni mwenzetu mmoja humu anaeharibu majina ya watu anajiita 'Benjamin Neyanyahu' amekwenda mbali zaidi kwa kusema hata wanaokula 'supu ya pweza' wote ni wazanzibari, hivi kweli tunaweza kuwa na 'united Tanganyika' dhidi ya wazanzibari?
 
View attachment 2890769View attachment 2890770
Na hawa ma Bwana zako wanawinda nini?

Acheni kuwasimanga Wamasai wakati huohuo wakivaa wengine mnasema ni Suna takatifu ya Mtume.

Sime na Rungu la Mmasai ni Ceremonial.
' Utumwa kweli kitu kibaya' hawa si ndio walikuwa wanatesa ndugu zetu kule zenji hadi mwalimu akapeleka jeshi kusaidia mapinduzi na hatimae muungano? mtu ameenda kuchukua picha zao katuletea tena humu?
 
Tena John Okello ni Nilote kama hao Wamasai wanaosimangwa.
 
Watanganyika tuna upole uliochanganya mpaka kufikia kilele cha ukilaza.

mfano:kwa ilo tukio la masai na polisi wa Zanzibar raia wa tz wangekua ndio raia wa South,Nigeria n,k wazanzibari wangechezea kichapo huku bara mpaka huo muungano ungejuta.

wa TZ ni watu wa ovyo sana wewe ukiwa mmoja wao, sasa wamasai wamepigana na security ambao ni watanganyika wenzao ndio mwanzo wa hii kesi, sasa muwapige wazanzibari kwa misingi ipi?
 
ujuaji mwingi kumbe zero.,🚮
Security wamepewa amri na nani?
 
Ukimsikiliza ni chuki tu za kibaguzi. Eti kama wanataka kufanya biashara wafungue maduka na wasibebe sime wala marungu. Hiv nchi hii wamasai wamewakosea nini. Maana porin kwao wamefukuzwa na huku mjin wanakojitafuta hawatakiwi. Mnataka wafanye nini waende wapi.
Kuna Jambo limejificha Mimi na wewe hatulijui Ila kuna Jambo kuhusu ndugu zetu Wamasai na wa kina fulani
 
CHADEMA FROM GROUNDS OF THEIR HEART SIELEWI KWANINI WANAPENDA MUUNGANO UVUNJIKE NI HILI LITAWA COST SANA CHADEMA, IPO HAJA YA KUREFORM HATA AINA YA DEMOKRASIA YETU, RAIS AKAWA NI WA CCM KWA MIAKA YOTE, LAKINI NGAZI YA WAZIRI MKUU NDIYO IKAWA INACHEZESHEWA MCHEZO WA DEMOKRASIA, INFACTS CHADEMA HAWAAMINIKI KAMWE, YANAWEZA KUTOKANA NA ULEVI WAO WAKAJA KUTUVUNJIA MUUNGANO WETU ADHIMU.
 
Nina laani kwa nguvu zote kitendo cha vurugu za mgambo na watu wa jamii ya kimasai kwakupigana hadharani, Nina laani Masai kushambulia Mgambo, Nina laani kwa nguvu kubwa Mgambo wa Zanzibar kushanbulia watu wa jamii ya kimasai! Jambo hili halikubaliki kwa mjibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazokataza kupigana hadharani au kificho.

Lakini naomba nitofautiane na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Zanzibar, Amri kwamba Wamasai hawaruhusiwi kutembea na fimbo na Sime/visu vyao, Ni Kauli Haramu na ya kibaguzi inayohatarisha muungano wa Tangabyika na Zanzibar.

Ifahamike kuwa Fimbo na Sime kwa Jamii za kimasai ni sehemu ya “vazi lao la asili”, ni Sehemu ya utamaduni wao, Ni Identity yao, na hivyo kujaribu kwa aina yoyote kuondoa kimoja wapo katika hivyo vinavyokuwa ndani ya mwili wa Masai ni kutangaza kuwafukuza Wamasi Zanzibar, Hili ni tangazo la kijinga limekurupukwa na mamlaka za Zanzibar!

Kwamiaka yote tangu kabla ya uhuru hadi leo, Jamii za Wamasai wapo Zanzibar na utamaduni wao wa visu/Sime na Fimbo, hakujawahi kuwa hatari kwa raia yoyote, Kwanini iwe leo baada ya Masai kujihami waliposhambuliwa na mgambo wa mji? Serikali ya Rais @dr.hmwinyi itafute jawabu la kumaliza mzozo huu sio kufunika kwakuwafukuza Wamasai, Tatizo liko kwa mamlaka za jiji, Tatizo liko kwa Wakuu wa Mikoa, na mamlaka zingine za jiji.

Unawazuia Wamasai wasibebe fimbo unataka Wabebe Vikapu vya Nazi na vigemeo vya Litembo? Unataka wabebe Usinga? Unataka wabebe karafuu? Noooo nooo tukatae unyanyasaji huu kwa jamii ya kimasai! Ukamilifu wa Masai ni fimbo na sime. Sasa unaka awe na shuka tu kama dera?

Kesho yataibuka Bara Wapemba watashambuliwa, Je serikali iweke amri wapemba wasizaliane kwa Wingi Bara ambao ni sehemu ya utamaduni wao? Nooo Nooo! Tukatae ubaguzi huu.

Mh Rais @dr.hmwinyi ili kunusuri maafa zaidi na kuoondoa hii taswira mbaya ya ubaguzi iliyotengenezwa na mamlaka za mji hapo Unguja, Ninakuomba na kukusihi Mh Rais, tengua hii kauli ya kibaguzi, Haifai kutolewa na kiongozi wa serikali katika ulimwengu wa leo! Madhara yake ni makubwa zaidi mbeleni.

Serikali ijifunze kutatua migogo kwa hekima na busara, Majibu ya hasira ya kiserikali yanaweza kuleta maafa zaidi kuliko kutatua, Nimeisikiliza kauli ikitolewa na yule kiongozi wa mjinibZanzibar (Unguja) ni wazi alitawaliwa na ghadhabu zaidi kuliko hekima ya kiuongozi, Amewahukumu Wamasai bila kujaribu kujua undani na kutafuta jawabu, Badala yake ametafuta jibu ambalo ni la hovyo zaidi!,

Nimesikitika sana kwa kauli hii ya serikali ya Zanzibar katika zama hizi za utandawazi na utandaridhi! Utengamano wa taifa letu ni muhimu kuliko hizi chuki zinazokolezwa na namlaka za nchi!

Na Yericko Nyerere
View attachment 2890368
Fimbo na Sime ni kwa ajili ya kujilinda na wanyama wakali wakiwa huko mapolini kwao. Sasa Beach uende na Sime na Fimbo kweli?
 
Viongozi wa nchi na walio wengi ni wajinga sana. Unalikubali shaka la.ke unakataa sime yake. Kisha unadanganya utalii kuongezeka
Huo sindo utambulisho wao???
 
Heshimu mamlaka huwezi kuwa juu ya mamlaka na ukajiendea tu kipuuzi, wapo ndani wamasai tisa mpaka muda huu kwa ujinga huo wa kudhani sime ndio kila kitu.
Vip wale wanaouza mapanga njian au wanaotumia hizo sime kukwangulia samaki kule ferry. Tumia akili acheni chuki za kimasikin
 
Viongozi wa nchi na walio wengi ni wajinga sana. Unalikubali shaka la.ke unakataa sime yake. Kisha unadanganya utalii kuongezeka
Huo sindo utambulisho wao???
Utambulisho ni kitu kimoja, kujua kuwa ni silaha inayoweza kuua ni suala jingine tofauti kabisa.

Hao wamasai waliokamatwa na kuwekwa ndani wanalo kosa la kuvuruga amani, mada za Yericko zinawajaza ujinga badala ya kuwasaidia wakajitambua.
 
Back
Top Bottom