Rais Mwinyi: Tukatae uzushi kuwa Mtu akipata chanjo ya corona atakufa

Rais Mwinyi: Tukatae uzushi kuwa Mtu akipata chanjo ya corona atakufa

Nimekuuliza Tz kutokuchukua tahadhari dhidi ya corona kuna maana gani?
Kuunda kamati ni hatua ya kwanza..... Chanjo kuletwa hatua ya pili.... Tunamuona Rais anaongoza kampeni ya barakoa n.k sasa unataka hatua gani? Waweke lockdown ili mpate cha kuongea?
 
"Chanjo ya ugonjwa wa Corona ni hiari, hatolazimishwa mtu kuchanja chanjo hiyo. Tukatae uzushi kuwa mtu akichanjwa atakufa, sio kweli"

Ndugu @DrHmwinyi
Rais wa Zanzibar na M/kiti wa BLM
Mjumbe wa Kamati Kuu ya H/Kuu ya Taifa.

Mahonda, Kaskazini Unguja.
Mei 29, 2021.

View attachment 1802084

Ile mijamaa sasa na isubirie tu sasa dawa iyaingie.
 
Natumaini viongozi wetu nao watachoma chanjo na picha zitaonekana kwenye vyombo vya habari kama nchi zingine walivyofanya. Kiongozi ni mfano!!!
 
Nikuulize swali sasa hivi corona ipo au haipo? nakuuliza hivyo ili nipate kuelewa huku kutochukua tahadhari kuna maana gani kwa sasa na huko kutaka chanjo kuna maana gani.
Nchi ya Tanzania ni kama mchwa waliopo pangoni.hatuna data "taarifa" ya nini kinachoendelea duniani. Hatupimi Corona, hatuna ugonjwa wa Corona. Kwakifupi tupo gizani hatuna tunachoelewa kuhusu huu ugonjwa.
 
Natumaini viongozi wetu nao watachoma chanjo na picha zitaonekana kwenye vyombo vya habari kama nchi zingine walivyofanya. Kiongozi ni mfano!!!
Siyo lazima chanjo ni hiari.tusifuate mkumbo wa viongozi kuchanja tukafuata .tumia akili yako binafsi kuchanja au kuacha. Kama huna akili azima kwa jirani au ndugu yako ili uweze kuamua!
 
Kuunda kamati ni hatua ya kwanza..... Chanjo kuletwa hatua ya pili.... Tunamuona Rais anaongoza kampeni ya barakoa n.k sasa unataka hatua gani? Waweke lockdown ili mpate cha kuongea?
Hivi kweli hata wewe nae unafikiria barakoa ni kama hirizi ukiwa nayo tu kila kitu kinaenda sawa? kila mtu anaimba barakoa barakoa.
Hivi barakoa bila social distance ni nani huyo aliyeshaur hivyo? halafu hiyo kampeni yenyewe ndio hiyo ya kuvaa barakoa anapokuwepo rais tu ila nje ya hapo watu hawavai?
 
Kusema chanjo hizo ni hiari kuzikubali au kuzikataa ni ulagai mtupu.

Kitakacho tokea baada ya chanjo hizo kuingia nchini ni vikwazo vingi katika taasisi za kijamii na maeneo mbalimbali ya kutolea huduma hususani Bank, Hospital, Usafiri nk.

Kwamba ili uweze kuingia katika sehemu hizo na kuhudumiwa ni lazima uwe tayari umeshachanjwa! Kwa vyovyote wote mtachanjwa tu, uwe unataka au hutaki!
Chanjo hiyari hutaki acha kwa hiyo hata huko Bank wakisema lazima ule sindano ndiyo upate huduma sawa tu ni hiyari yako uchanjwe au ukose huduma.
 
Mbona hakuyasema hayo JPM akiwepo!!!
Sasa si arudi kama yeye mbabe 😡 acheni kusumbua watu kila siku Shujaa Shujaaa 😏😏😏😏, watu walipambana na Hitler sembuse huyo msukuma wenu.
 
Siyo lazima chanjo ni hiari.tusifuate mkumbo wa viongozi kuchanja tukafuata .tumia akili yako binafsi kuchanja au kuacha. Kama huna akili azima kwa jirani au ndugu yako ili uweze kuamua!
😁
 
Nchi ya Tanzania ni kama mchwa waliopo pangoni.hatuna data "taarifa" ya nini kinachoendelea duniani. Hatupimi Corona, hatuna ugonjwa wa Corona. Kwakifupi tupo gizani hatuna tunachoelewa kuhusu huu ugonjwa.
Ulichojibu sichonilichouliza, mimi nauliza kwanini hatuchukui tahadhari hilo la takwimu ni lengine au unataka kuniambia kwamba hatuchukui tahadhari kwa sababu hatuna takwimu?
 
Ulichojibu sichonilichouliza, mimi nauliza kwanini hatuchukui tahadhari hilo la takwimu ni lengine au unataka kuniambia kwamba hatuchukui tahadhari kwa sababu hatuna takwimu?
Hilo swali siwezi kulijibu ni la kijinga sana
 
Hilo swali siwezi kulijibu ni la kijinga sana
Kwanini la kijinga? Rais aliyetoka alikuwa na msimamo wa kwamba hakuna corona na ndio maana alikuwa hachukui tahadhari watu walijiachia kwa sababu huku wakiamini Corona imeondoka kwa maombi, sasa rais wa sasa msimamo wake ni kwamba corona ipo na ana mpango hadi wa kuagiza chanjo sasa inakuaje kwamba anatambua kuwa kuna ugonjwa hatari corona ila kaachia watu waishi kama hakuna corona? mwaka jana mwanzoni kabla ya kufanya maombi walifunga mashule,walizuia mikusanyiko ya masherehe michezo n.k na waliweka utaratibu wa level seat kwenye daladala. Yote hayo yalifanyika ili kuzuia maambukizi na wenzetu bado wanayafanya na sisi sio kisiwa inakuaje hatuchukui tahadhari kama hizo?

Tofauti ninayoiona sasa hivi ni Rais Samia kuvaa barakoa tu huku raia wakiwa wanaendelea na mambo yao kama kawaida.
 
Corona imeondoka na mwendazake, na huo ndo ukweli wenyewe.
 
Corona imeondoka na mwendazake, na huo ndo ukweli wenyewe.
Ukweli huwa na ushahidi, hebu fikiria kuna watu nao walisema kuwa Mwendazake alichanjwa kisirisiri chanjo ya corona sasa hapo nani anasema kweli? ndio maana nakwambia ukweli huwa na ushahidi ili wengine ndio tuweze kujua la sivyo kila jambo litalozungumzwa litakuwa kweli hata kama kuna contradiction.
 
Back
Top Bottom