Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Mama ana malengo ya kuitangaza Zanzibar zaid
Zanzibar (visiwa vya marashi ya karafuu) inajitangaza yenyewe haihitaji mtu kuitangaza. Zanzibar sio geita au katavi iliyozaliwa juzi.

Zanzibar ina historia kubwa sana ambayo Tanganyika haiwezi ifikia.

Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
 
Huyu maza kazi tunayo 🤔,
Kazi inaendelea Ila miaka kadhaa tutalia nakusaga meno.
 
Nafkiri ieleweke kwanza Mh. Rais ana haki ya kumchagua yeyote kumuwakilisha katika ziara za nje, Dr Mwinyi ni Rais wa SMZ ila pia ni mjumbe wa baraza la mawaziri na katika masuala ya mambo ya nje ni yakimuungano so sio kosa yeye kwenda kama mwakilishi wa rais wa SMT ila tu znz haiwezi ikajiwakilisha yenyewe kwenye mambo ya nje.

Pia yawezekana kwakuwa viongozi wakuu wa SMT kwa sasa Rais,VP na PM wapo busy na kuunda serikali yao ya awamu ya sita, pia waziri nje tunaona yupo busy kurejesha mahusiano ya kidiplomasia (tunaona ugeni mwingi) yawezekana ndio maana mh SSH anaona ni busara wawepo halafu kuwe na uwakilishi.

Nawasilisha
 
Acheni Wivu
Ni Zamu Wa Zenj.
Mbona Mwendazake alikuwa anamtuma Bashite
Ni wivu, husda, chuki, vijicho na roho mbaya ndio vinasumbua watu.

Mama tangu ameingia madarakani neema mbali mbali zimepatikana. Huko Arusha St. Jude nimeambiwa watoto wanaenda kurudi shule na mambo yanakwenda vyema tu.
 
Paul Makonda alikuwa anatumwa na Hayati Rais Dkt. Magufuli ' Kumuwakilisha ' katika Safari zake za Kimataifa ili Kuiwakilisha nchi pia? Kuna Watu huwa mnanilazimisha niwe nawadharau kwa Upumbavu wenu wa Kurithishwa.
kwaani Mwinyi anatumwa kuuwakilisha mkoa...?
 
Zanzibar (visiwa vya marashi ya karafuu) inajitangaza yenyewe haihitaji mtu kuitangaza. Zanzibar sio geita au katavi iliyozaliwa juzi.

Zanzibar ina historia kubwa sana ambayo Tanganyika haiwezi ifikia.

Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
Mama 'anakulipa' nini 'Kumpigania' hivi?
 
Rais Mwinyi ndiye Rais Mtarajiwa wa JMT mwaka 2025 kimsingi mama anakamilisha tu kipindi cha mpito kuja kumkabidhi kijiti mwinyi 2025 hili litasimamiwa kwa ukaribu sana na vyombo vya dola kuhakikisha the chosen anakuwa Rais wa JMT hili liko wazi
Sasa tunaanza kuelewana....hizi overt actions zinadhihirisha hili....
 
Katiba ya nchi haimzuii kumtuma RAIS WA ZANZIBAR kumuwakilisha nje......
Na Mama anafanya kazi kwa akili kubwa sana.

Ukiwa babala huwezi muelewa mama kamwe.

Watanzania, tuwaacheni wapiga domo waendelee kupiga domo mitandaoni. Sisi tumuunge mkono Mama na kazi iendelee
 
Ni wivu, husda, chuki, vijicho na roho mbaya ndio vinasumbua watu.

Mama tangu ameingia madarakani neema mbali mbali zimepatikana. Huko Arusha St. Jude nimeambiwa watoto wanaenda kurudi shule na mambo yanakwenda vyema tu.
Jadili Kihoja na siyo Kishabiki unatuboa.
 
Hapo maza anaharibu wasijisahaulishe wao wako milioni moja na nusu tu, wanapotaka fursa sawa wajue wengi ndio tunaoamua hatma ya Muungano feki unaowanufaisha Zanzibar kuliko Tanganyika Mbona magufuli alimwagiza sana Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuliko mwingine yoyote,
Usimpangie mama cha kufanya.

Sisi Watanzania tumemuamini na tunajua nchi ipo katika mikono sahihi.

Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Back
Top Bottom