Rais na Makamu wasipokuwepo nchini Nani Anakaimu?

Rais na Makamu wasipokuwepo nchini Nani Anakaimu?

1. Naomba kujuzwa utaratibu wa kikatiba unasemaje endapo Rais na Makamu wa Rais wanapokua nje ya nchi Kwa wakati mmoja. Ni Nani Anakaimu nafasi ya Rais Kwa Katiba ya Sasa?

3. Jibu Kwa kutaja kifungu cha Katiba iliyopo (toleo), usijibu kama upo vilingeni.
Sasa nini kimekushinda wewe kwenda kuvisoma hivyo vifungu huko kwenye Katiba? Mbona mnapenda kuchosha wenzenu aisee!
 
Hapana, ikiwa Rais na Makamu hawapo nchi itaongozwa na spika wa bunge na kama HAYUPO nchi itaongozwa na judge mkuu.,... Waziri mkuu hajatajwa kwenye katiba...hiyo nilisomaga zamani kwenye SoMo la siasa darasa la nne ama la tatu
Soma katiba ibara ya 37(3) nakuwekekea hapa[emoji116][emoji116]
Screenshot_20240818-113545.jpg
 
Ni kweli mbaya zaidi baadhi ya Taasisi za umma zimeweka kwenye tovuti zao Katiba toleo la 1995 badala ya latest edition ya 2010.
Mfano wa Taasisi zilizoweka katiba toleo la zamani.
1. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Baadhi ya Tovuti hazina kabisa katiba kwenye machapisho yake.
Duh! Hao akina Shositi (Cyst) Nyahoza na akina Mtungi, wao wamepiga usingizi wa pono. Wataamka kukemea au kupiga vita mikutano ya Chadema. Na kuratibu ushindi wa CCM.
 
Taasisi zetu nyingi ni haziweki taarifa sahihi kwenye Tovuti zake.

Baadhi ya Taasisi taarifa latest ni za miaka mitatu iliyopita.
Kwa uzembe huu na kutokujali, maendeleo tutaendelea kuyasikilizia Kwa wenzetu walio serious sisi tuendeleze uchawa, ukunguni na uviluwiluwi wa chura kiziwi.
 
Waziri Mkuu
Asipokuepo yeye pia Naibu wake asipokuepo na yeye anaebakia kusimamia ni Spika wa Bunge akiwa hayupo na yeye Naibu wake akiwa hayupo na yeye Mkuu wa Majeshi ndio anachukua nafasi km yeye hayupo pia anachukua anaemfuatia mwenye nyota 3 km na yeye hayupo anachukua anaemfuatia mwenye nyota 2 km na yeye hayupo anachukua anaemfuatia mwenye nyota 1

Uliza swali lingine
Na wasipokuwepo wote nikabaki mwenyewe 🤣 kumbe kila mtu anaweza kuwa Rais
 
Back
Top Bottom