Mkuu
Foxhound , kuna mambo mengi tunafanya shaghalabaghala.
Kanuni ya kukaimu inahusu kitu kinachoitwa hierarchy. Kufuatia Tanzania kuwa ni nchi ya Muungano, tuna hierarchy mbili.
1. Hierarchy kwa mujibu wa Katiba
2. Hierarchy ya protocol
Kwenye hierarchy ya Katiba ya JMT
No. 1 ni Rais wa JMT
No. 2 ni VP
No. 3 ni Spika
No. 4 ni CJ
No. 5 ni PM
Kwenye set up ya Muungano, rais wa Zanzibar is nobody na katiba yetu haiwatambui wale makamo wawili wa Zanzibar.
Kwenye hierarchy ya protocol
No. 1 ni Rais wa JMT
No. 2 ni VP
No. 3 ni Rais wa Zanzibar
No. 4 ni PM
No. 5 ni VP-I Zanzibar
No. 6 ni VP -II Zanzibar
No. 7 ni Spika
No. 8 ni CJ
No. 9 ni CDF
No. 10 ni DGIS
Kuna kutokuwepo Rais na Makamo kwa aina mbili, kuna kutokuwepo kwa sababu ya safari nje ya nchi, rais anaweza kumteua yeyote kuwa kaimu rais, enzi za JK kuna siku Spika Sitta alikaimu urais, enzi hii ya Samia, kuna siku Dr. Mwinyi alikaimu urais. Kwa vile kwa mujibu wa Katiba ya JMT, rais wa Zanzibar is nobody, ni kinyume cha Katiba kumkaimisha urais wa JMT someone who is nobody!. Prof Kabudi atamsaidia Rais Samia kwenye hili.
Na kuna kutokuwepo kwa rais kwa ama kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kwa maradhi au ile safari ya kimoja kama ilivyotokea kwa JPM, then hierarchy ya Katiba inafuatwa.
Kwa kawaida No. 2, VP ana pokea amri kwa mtu mmoja tuu, No. 1. Lile tukio tulilo tangaziwa Machi 17, lilitokea Machi 12!, (
Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?) swali ni nani alitoa amri kumtuma VC safari ya Tanga ili waweze kufanya mambo huku bara CDF ndie akaingilia kati?.
Kiukweli tuna mambo ya ajabu!. JPM naye kuna kipindi alipelekewa majina matatu ya kumchagua mmoja kuwa CJ baada ya Jaji Chande, JPM akawakataa wote na kumkaimisha Prof. Ibrahim Juma u CJ. Kaimu CJ anaweza kuteuliwa in an event of sudden death of the current CJ, na sio CJ amestaafu kwa mujibu wa sheria halafu unateua kaimu!.
Mama nae kaja na mpya, the current CJ amemaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba, ameongezewa muda kinyume cha Katiba! washauri wa rais sheria wote wapo kimya, isipokuwa shujaa mmoja mwanamke
Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.
Mkuu wa mkoa asipokuwepo mkoani kwake, Mkuu wa mkoa wa jirani ndie ana kaimu, sii mara moja wala mbili nimehudhuria matukio Mkuu wa wilaya mmoja ana kaimu Mkuu wa mkoa na mfano hai ni huu
View: https://youtu.be/KvvschTpEh0?si=57P-820uIazhzpj_
Kuna baadhi ya mambo tunayaendesha kwa auto pilot!.
P