Rais na Makamu wasipokuwepo nchini Nani Anakaimu?

Rais na Makamu wasipokuwepo nchini Nani Anakaimu?

Kwa kuchota Mabilioni na Kuweka ngumu Makamu kushika hatamu mara tu baada ya Shujaa kung'ata shuka
Kuna mengi kumhusu mwendazake hatukuambiwa, Dr. Bashiru hakuchota hata senti 5, ila ni Blaza ndie hakuwa na imani na mwanamke, akamkabidhi mamlaka yote Dr. Bashiru, hizo fedha zilichotwa katika kumhangaikia huku na kule kujaribu kuokoa maisha mara Nairobi Hospital, mara India alimradi watu walihangaika sana for 5 good days bila mafanikio ndipo mwisho wakakubali matokeo na kututangazia after 5 days!. Niliuliza humu Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5? hili mimi nimeliongea sana Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025 na hapa http://85.217.170.64/sw/ubunge-wa-bashiru-ali-wachambuzi-wanasemaje/av-57074092
P
 
Hivi yule nani alisema Mimi nimepuyanga aje hapa nikuone tena Foxhound au na hii utabisha? CDF si ndio Chief of Defence Forces au nakosea Mkuu wa Majeshi?
Hivi ni wapi nimesema umepuyanga, au unatafuta tu la kuongea, nioneshe hapo niliposema!
 
Mkuu Foxhound , kuna mambo mengi tunafanya shaghalabaghala.
Kanuni ya kukaimu inahusu kitu kinachoitwa hierarchy. Kufuatia Tanzania kuwa ni nchi ya Muungano, tuna hierarchy mbili.
1. Hierarchy kwa mujibu wa Katiba
2. Hierarchy ya protocol

Kwenye hierarchy ya Katiba ya JMT
No. 1 ni Rais wa JMT
No. 2 ni VP
No. 3 ni Spika
No. 4 ni CJ
No. 5 ni PM
Kwenye set up ya Muungano, rais wa Zanzibar is nobody na katiba yetu haiwatambui wale makamo wawili wa Zanzibar.

Kwenye hierarchy ya protocol
No. 1 ni Rais wa JMT
No. 2 ni VP
No. 3 ni Rais wa Zanzibar
No. 4 ni PM
No. 5 ni VP-I Zanzibar
No. 6 ni VP -II
No. 7 ni Spika
No. 8 ni CJ
No. 9 ni PM
No. 10 ni CDF

P
Namba 4 na 9 ni MTU huyo hiyo au ni Waziri Kiongozi wa Zanzibar
 
Kama maelezo hayapo kwenye katiba basi anaeongoza nchi ni katibu mkuu kiongozi.

Kwa siasa za kijijini kwetu mkuu wa nchi akitoka tu japokuwa ana naibu wake, mwenye maamuzi ni katibu mkuu kiongozi.

Nafasi ya katibu mkuu kiongozi sio ya mzaha kabisa kwenye nchi zilizokopi katiba ya nchi mama za madola unitary constitution. Katibu mkuu kiongozi technically ndio anaongoza nchi kama uingereza bila ya mandate (yaani sio mtu wa mzaha kabisa).
 
Waziri Mkuu
Asipokuepo yeye pia Naibu wake asipokuepo na yeye anaebakia kusimamia ni Spika wa Bunge akiwa hayupo na yeye Naibu wake akiwa hayupo na yeye Mkuu wa Majeshi ndio anachukua nafasi km yeye hayupo pia anachukua anaemfuatia mwenye nyota 3 km na yeye hayupo anachukua anaemfuatia mwenye nyota 2 km na yeye hayupo anachukua anaemfuatia mwenye nyota 1

Uliza swali lingine
Unatupiga fix balaa...
 
Kwa mujibu wa kifungu cha 37 (5) cha Katiba ya nchi iliyotungwa mwaka 1977, nafasi ya urais inapokuwa wazi kwa sababu yoyote ikiwemo kifo, viongozi watatu wameorodheshwa na ni Makamu wa Rais, na endapo hatakuwepo atachukua Spika wa Bunge na kama hayupo atachukua Jaji Mkuu.

La roche
Sio kweli.
 
Mkuu Foxhound , kuna mambo mengi tunafanya shaghalabaghala.
Kanuni ya kukaimu inahusu kitu kinachoitwa hierarchy. Kufuatia Tanzania kuwa ni nchi ya Muungano, tuna hierarchy mbili.
1. Hierarchy kwa mujibu wa Katiba
2. Hierarchy ya protocol

Kwenye hierarchy ya Katiba ya JMT
No. 1 ni Rais wa JMT
No. 2 ni VP
No. 3 ni Spika
No. 4 ni CJ
No. 5 ni PM
Kwenye set up ya Muungano, rais wa Zanzibar is nobody na katiba yetu haiwatambui wale makamo wawili wa Zanzibar.

Kwenye hierarchy ya protocol
No. 1 ni Rais wa JMT
No. 2 ni VP
No. 3 ni Rais wa Zanzibar
No. 4 ni PM
No. 5 ni VP-I Zanzibar
No. 6 ni VP -II Zanzibar
No. 7 ni Spika
No. 8 ni CJ
No. 9 ni CDF
No. 10 ni DGIS

Kuna kutokuwepo Rais na Makamo kwa aina mbili, kuna kutokuwepo kwa sababu ya safari nje ya nchi, rais anaweza kumteua yeyote kuwa kaimu rais, enzi za JK kuna siku Spika Sitta alikaimu urais, enzi hii ya Samia, kuna siku Dr. Mwinyi alikaimu urais. Kwa vile kwa mujibu wa Katiba ya JMT, rais wa Zanzibar is nobody, ni kinyume cha Katiba kumkaimisha urais wa JMT someone who is nobody!. Prof Kabudi atamsaidia Rais Samia kwenye hili.
Na kuna kutokuwepo kwa rais kwa ama kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kwa maradhi au ile safari ya kimoja kama ilivyotokea kwa JPM, then hierarchy ya Katiba inafuatwa.

Kwa kawaida No. 2, VP ana pokea amri kwa mtu mmoja tuu, No. 1. Lile tukio tulilo tangaziwa Machi 17, lilitokea Machi 12!, (Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?) swali ni nani alitoa amri kumtuma VC safari ya Tanga ili waweze kufanya mambo huku bara CDF ndie akaingilia kati?.

Kiukweli tuna mambo ya ajabu!. JPM naye kuna kipindi alipelekewa majina matatu ya kumchagua mmoja kuwa CJ baada ya Jaji Chande, JPM akawakataa wote na kumkaimisha Prof. Ibrahim Juma u CJ. Kaimu CJ anaweza kuteuliwa in an event of sudden death of the current CJ, na sio CJ amestaafu kwa mujibu wa sheria halafu unateua kaimu!.

Mama nae kaja na mpya, the current CJ amemaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba, ameongezewa muda kinyume cha Katiba! washauri wa rais sheria wote wapo kimya, isipokuwa shujaa mmoja mwanamke Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.

Mkuu wa mkoa asipokuwepo mkoani kwake, Mkuu wa mkoa wa jirani ndie ana kaimu, sii mara moja wala mbili nimehudhuria matukio Mkuu wa wilaya mmoja ana kaimu Mkuu wa mkoa na mfano hai ni huu
View: https://youtu.be/KvvschTpEh0?si=57P-820uIazhzpj_

Kuna baadhi ya mambo tunayaendesha kwa auto pilot!.

P

Hakika umeeleza vizuri sana mkuu nimekupata katiba haifatwi ipasavyo ni kujitwangia tu. Kwa kuwa una nguvu na mamlaka na wote ni wateule wako hakuna anayeweza kukujibu against

Cc. Michiwen
 
Back
Top Bottom