Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Hivi hayo madeni, mimi kama mwananchi yananidhuruje? Naomba kufahamishwa!! Binafsi nadhani hayana "IMPACT" kwa ustawi wa familia yangu!! hata usingizi sijawahi kukosa eti nawaza deni la taifa
 
Lakini mikopo ni hatari. Serikali inayosisitiza kukopa sio serikali ya kuishabikia hata kidogo. Sera zako za kiuchumi zitavurigika sana kama utategemea uchumi. Itafika mahali sera za kiuchumi utapangiwa ili uwezw kuserve debt.
Mbona unaongea na kujijibu mwenyewe??
 
Mikopo ikifanyia hizi shughuli nakuwa sina tatizo nayo! Ila kuniambia mikopo inajenga madarasa halafu tozo nazo pia zinajenga madarasa ni wizi wa mchana kweupe!

Hamnaga kitu kama hicho...Ufisadi utakuwa wa kutisha sana
 
Lakini mikopo ni hatari. Serikali inayosisitiza kukopa sio serikali ya kuishabikia hata kidogo. Sera zako za kiuchumi zitavurigika sana kama utategemea uchumi. Itafika mahali sera za kiuchumi utapangiwa ili uwezw kuserve debt.
Kwani taifa hili lini liliacha kukopa?hadi awamu hii ndio isemwe?kuna awamu iliyokopa zaidi ya awamu ya 5? Huku tuliaminishwa kuwa ni pesa zetu!!alikuwa wapi , na mala ngapi mbungeni ukuaji wa deni la taifa ulijojiwa sana na wapinzani, lakini walikuwa wanapewa tu majibu ya ki MIPASHO?!!hayo ma miradi aliyoyaacha meko unafikiria yataendeleaje wakati yeye alikopa kuyaanza?!!si bora hata huyu ana sema ukweli kuwa ana kopa?na yule aliyekuwa ana kopa hadi kwenye ma bank ya biashara?
 
Unapendekeza afavywaje spika? Huo ni mhimili pamoja na kwamba yuko chini ya chama kinachoongozwa na rais!!! Hawezi kumtoa

Mhimili wa pili umeshatoa dukuduku lao, bado mhimili mahakama nao wana mambo yanayowaudhi kisheria kulazimishwa kuyatenda; kisha funga kazi jeshi ndio litakalo mwacha hoi mkuu wa nchi kwamba akifanyacho kitamgharimu.

Rais hamfanyi chochote spika na jaji mkuu pamoja na mkuwa majeshi.

Aache kujibizana na watu wanaotumia haki yao ya kutoa maoni kama anavyyeye, majibizano kama taarabu kwenye masuala ya msingi hayana afya kwa taifa anatakiwa kukubali udhaifu wake wa kutokuwa na uwezo kutafuta vyanzo vya ndani maana tuna rasilimali za kutosha

Hii kauli ya kusema "tutaendelea kukopa..........", Mungu amsamehe mhajui alitendalo; hakuna Mtanzania anayempenda kwa sasa labda wansiasa wezi
 
Tutengeneze vitu vya maana kama electric plants hio ya Nyerere ili treni ianze kazi viwanda vya magari electric cars tuvianzishe nchini uchumi uende kasi tuachane na biashara ya kuagiza mafuta kwa wingi kupoteza pesa!
 
Ndugai anaweza kuzisukuma kete?....hao Msoga Inc wanasukuma kete balaa, muulize EL na ulipo tupo....Ndugai kaa mkao wa kula hao jamaa watalaam wa fitina, jifunze kwa Mzee Six na uwaziri mkuu....
Bila kujua watu wanaanza kujichekecha...Mara team wazalendo na team ma deal wataanza mpambano...The author is watching from a far...
 
Mh. Ndugai pia anao Uhuru wa maoni na ni vemauhuru huo uheshimiwe.
Tuzoee na tukubaliutamaduni mzuri wa kidemokradia wa kutofautiana hoja bila kugombana.

Hili litawezekana tu kama tukipata Katiba Mpya!

Tuungane kuidai!!
 
Soma katiba uone spika anatokaje, mchakato wa kumtoa madarakani Rais ndio mgumu na pengine ni impossible
 
Hata Mzee Samwel Six aliikosoa sana serikali ya Kikwete. Ndugai anatumia haki yake ya kutoa maoni kama ambavyo kina Bulembo wanatumia.
Kwani mzee Ulimwengu alitumia haki yake ya nini akamtisha tisha
 
Acha uongo!
 
Hahahaha kumekuchaaaaa
 
Tutengeneze vitu vya maana kama electric plants hio ya Nyerere ili treni ianze kazi viwanda vya magari electric cars tuvianzishe nchini uchumi uende kasi tuachane na biashara ya kuagiza mafuta kwa wingi kupoteza pesa!
Miradi yote ya nchi hii niyaupigaji wala usifikiri Kama mwananchi unapendwa sana, hiyo stiglars gorge au standard gauge ingekuwa imekamilika kila siku kughaili tarehe, tumeshapigwa sana
 
Dharau tu naona enzi za jiwe kila mtu aliufyata kuanzia kina Mbowe walikuwa kimya over sudden wote wameota mapembe, ndugai yeye alikuwa anasifia tu kila kitu Hadi vya kijinga
Ukisema Mbowe alikuwa kimya wakati wa Magufuli unamaanisha nini exactly? Manake uhalisia ni kwamba alikuwa anaongea hadharani Magufuli akiwepo hai,kumpinga alipokosea hasa kuhusiana na madudu ya uchaguzi mkuu
 
Manyang'au sasa yanatafutana ndani; Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi mkishaifanya haitawaacha salama...mtagundua kumbe nyinyi siyo wamoja, siyo ccm, kuna ccm wenye mikia na waliokatwa mikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…