Rais na Taasisi saidizi zirudi Dar es Salaam, Makamu wa Rais abaki Dodoma

nchi zipi? nitajie..... nami nikutajie nchi za first world ambazo biashara na makao makuu vipo sehemu moja.
Wanachofanya ni kudiversify viwanda according to location of raw materials and other infrastructure to feed the planned factory/industry
South Africa...
USA
 
nchi zipi? nitajie..... nami nikutajie nchi za first world ambazo biashara na makao makuu vipo sehemu moja.
Wanachofanya ni kudiversify viwanda according to location of raw materials and other infrastructure to feed the planned factory/industry
Kila nchi ina sababu zake kwa nini makao yake makuu yako sehemu fulani.

Mfano, Brazil wakati wa ukoloni Makao makuu yaliwekwa Rio Di Janeiro kwa sababu kulikuwa na migodi ya dhahabu kule. Hivyo taasisi za kibiashara na kiserikali zikawa pale (lengo mkoloni kunyonya nchi, sio kuhudumia wananchi). Baadae mji wa kibiashara ukahamia Sao Paul kufuata mashamba kule, lakini serikali haikuhama. Kwa sababu mbili, moja haikuwa na sababu ya kuufuata mji wa kibiashara, pili urahisi wa ufikaji maeneo ya nchi yao na tatu ni sababu za kiusalama. Sababu hizi na Nigeria walikuwa nazo baadhi.

Sisi sababu za umbali bado zipo ( sababu bado watu ni lazima wasafiri kwenda makao makuu, ingawa inazidi kupotea), pili sababu kuu ambazo bado zipo, ni za kiusalama na kiuchumi.

Dar iliwekwa kuwa makao makuu ya nchi na wakoloni kwa sababu za kiographia. I.e bandari, reli. Hivyo eneo hili limeendelea sana, na mikoa ya jirani yake kama Morogoro na Pwani inaendelezea kwa mchango mkubwa kutokea Dar. Hata mikoa ya nyanda za juu kusini kibiashara bado inaitegemea dar. Hivyo Makao ya serikali yakihamia Dodoma, itaboost uchumi wa Kanda ya kati na maeneo jirani. Mfano sekta ya Hospitality itakuwa sana maana yake wakulima, wavuvi na wafugi kuna faida nyingi zitawakuta. Pili mji wa dar na Dodoma vitafungamanishwa sana kiuchumi. Mikoa kama singida, iringa na maeneo kama Igunga yatapata manufaa ya uwepo wa makao makuu. Kwa picha kubwa unatanua uchumi. Tusisahau diversification is healthy. Kiusalama bado si busara mji wa serikali na kibiashara kuwa sehemu moja. Tusiwaze kama wamarekani wakati sisi ni Watanzania. Bado teknolojia ni ndogo hivyo bado mbinu nyingi za kiusalama na ulinzi ziko mechanical zaidi. Ikimaanisha kujilinda pamoja na uokoaji. Mwaka jana kuna ajali ilitaka kutokea Dar kwenye matank ya Lake Oil, i can tell you ile issue ingekuwa ni disaster. Bado Dodoma kuna manufaa makubwa kuwa makao makuu ya nchi.
 

Mradi wa kuhamia makao makuu Dodoma ulikuwa na madhumuni ya kuwadhibiti wakubwa wote, ilikuwa ni aina ya sanaa kuwatia mbaroni kiakili wakubwa wote wasifurukute.

Mradi huu Dodoma ambao ingawa haujaisha majengo yake lakini hauna tofauti na simulizi ya ule mradi maarufu wa King Louis XIV mwaka 1682 nchini France makao makao makuu mapya mfalme ya Versailles : Versailles was a golden prison Versailles - King Louis XIV: Age of Absolutism
Ambapo mfalme alihakikisha kila shughuli amezungukwa na viongozi wa mihimili yote na kuoneshwa live.

Baada ya mwendazake kuondoka ndiyo wamestuka kuwa kumbe kuna majengo yaliyokamilika Dar es Salaam na pia uhuru wa kuburuzwa kuwepo ktk kila shughuli hupunguza tija, ufanisi wa kazi zao hivyo bora kurejea Dar es Salaam kulikokamilika 'kazi iendelee ' ya kuwatumikia waTanzania.
 
Ujinga mwingine Huu

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Hahaaa naunga mkono hoja maana mwendazake alijitia kuhamishia watu kule lakini yeye akaja kufia Dar tena Mzena , mambo yanakwenda kasi sana usije kumwamini mwana siasa hata siku moja
 
Kama hutaki kuendelea na utumishi wa umma Dodoma acha rudi Dar es salaam hujalazimishwa. Usichoshe watu humu na pumba zako. Inaonyesha baadhi ya watz wanavyojitoa akili kwa maslahi ya matumbo yao. Wewe sema umewekeza Dar es Salaam au unamaslahi yako binafsi huko Dar es Salaam siyo kuleta porojo zisizo na na tija.
 
Kwani kuhamia Dodoma kuna tatizo gani? Au ndiyo nyie ambao hamtaki kubadilika mnaishi kwa mazoea tu. Miafrika inawazia matumbo yao tu kila dakika!
 
Japo umeita mawazo yangu ni pumba ila inasikitisha umeishia kuni critisize bila kuweka mawazo yako yasiyo pumba.

Weka ushabiki pembeni alafu jifikirie tena

Utumishi siwezi kuacha
 
Nikajua unasema miundombinu ambayo inapelea kwa Dom iharakishwe kumbe unashauri kugeuka nyuma,acha upuuzi mkuu
 
Dah!!..mkuu hizi serikali kuamia uko dodoma washatutesa vya kutosha,
Hasa sekretariet ya ajira aisee Bora warudi t mjini imetosha.
 
Mmenunua viwanja Dodoma Bei kubwa,,,Sasa mmepigwa Sasa mnalialia Kama yule Dada Fulani,aliyelipwa bilioni mbili kwa kumuuguza mama yake ikulu akaenda kujenga hotel chato
 
Kwani kuhamia Dodoma kuna tatizo gani? Au ndiyo nyie ambao hamtaki kubadilika mnaishi kwa mazoea tu. Miafrika inawazia matumbo yao tu kila dakika!
Wewe ni Mgogo au Mrangi?
 
Wewe ni Mgogo au Mrangi?
Miafrika mingine bwana hufukiria mwisho wa matumbo yao. Kwa hiyo wanaotaka makao makuu ya nchi yabaki Dodoma ni Wagogo na Warangi tu. Am afraid that am engaging a person with psychiatric case into this conversation. Fortunately enough Dodoma is also equipped with Milembe Hospital.
 
Mzee mgaya yeye anashauri nini
 
ila watu wengine bhanaaaaa, wakihamia Dodoma au wakirudi Dar ww inakusaidia nini. Humo ofisini ni wewe unakaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…