Kila nchi ina sababu zake kwa nini makao yake makuu yako sehemu fulani.
Mfano, Brazil wakati wa ukoloni Makao makuu yaliwekwa Rio Di Janeiro kwa sababu kulikuwa na migodi ya dhahabu kule. Hivyo taasisi za kibiashara na kiserikali zikawa pale (lengo mkoloni kunyonya nchi, sio kuhudumia wananchi). Baadae mji wa kibiashara ukahamia Sao Paul kufuata mashamba kule, lakini serikali haikuhama. Kwa sababu mbili, moja haikuwa na sababu ya kuufuata mji wa kibiashara, pili urahisi wa ufikaji maeneo ya nchi yao na tatu ni sababu za kiusalama. Sababu hizi na Nigeria walikuwa nazo baadhi.
Sisi sababu za umbali bado zipo ( sababu bado watu ni lazima wasafiri kwenda makao makuu, ingawa inazidi kupotea), pili sababu kuu ambazo bado zipo, ni za kiusalama na kiuchumi.
Dar iliwekwa kuwa makao makuu ya nchi na wakoloni kwa sababu za kiographia. I.e bandari, reli. Hivyo eneo hili limeendelea sana, na mikoa ya jirani yake kama Morogoro na Pwani inaendelezea kwa mchango mkubwa kutokea Dar. Hata mikoa ya nyanda za juu kusini kibiashara bado inaitegemea dar. Hivyo Makao ya serikali yakihamia Dodoma, itaboost uchumi wa Kanda ya kati na maeneo jirani. Mfano sekta ya Hospitality itakuwa sana maana yake wakulima, wavuvi na wafugi kuna faida nyingi zitawakuta. Pili mji wa dar na Dodoma vitafungamanishwa sana kiuchumi. Mikoa kama singida, iringa na maeneo kama Igunga yatapata manufaa ya uwepo wa makao makuu. Kwa picha kubwa unatanua uchumi. Tusisahau diversification is healthy. Kiusalama bado si busara mji wa serikali na kibiashara kuwa sehemu moja. Tusiwaze kama wamarekani wakati sisi ni Watanzania. Bado teknolojia ni ndogo hivyo bado mbinu nyingi za kiusalama na ulinzi ziko mechanical zaidi. Ikimaanisha kujilinda pamoja na uokoaji. Mwaka jana kuna ajali ilitaka kutokea Dar kwenye matank ya Lake Oil, i can tell you ile issue ingekuwa ni disaster. Bado Dodoma kuna manufaa makubwa kuwa makao makuu ya nchi.