Rais na Taasisi saidizi zirudi Dar es Salaam, Makamu wa Rais abaki Dodoma

Rais na Taasisi saidizi zirudi Dar es Salaam, Makamu wa Rais abaki Dodoma

tuliwaambia issue sio kuhamia dodoma, malalamiko yalikuwa kwenye uharaka na gharama itakayotumika......naona mnatema ndoano taratibu....
 
Dodoma wabaki Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Spika aende chato bunge ataliongoza kwa WhatsApp video call
 
Mimi ningeomba kwanza kufahamishwa nisababu zipi kwa wakati wa nyerere zilipelekea dodoma kupendekezwa kuwa makao makuu ya nchi?
 
Hakuna kitu kitaniuma katika maisha yangu kama kuua habari ya Dodoma, tumeenda Dodoma, tumefika Dodoma, Dodoma imeanza kushamiri, watu wananunua viwanja. Hakika wanasiasaa ndio miungu wa dunia hii.
 
Kama tulipanga kuhamia dodoma na kulikuwa na umuhimu na priority hiyo basi tungetengeneza time frame na phases kuanzia one mpaka sita....kwa kutenga budget kila mwaka na kufanya kitu..sio ghafla bin vuu tu...
 
Huu upuuzi ndo jpm alikuwa hataki.yaan wanaloliona gumu kumbe jepesi tu.

Ukiona mtu anaeogopa kufanya maamuzi jua kichwa maji tu.

Kama sio jpm sidhani kama ikulu ingehamiaga dodoma.

Rip jpm
Hata kurudi Dar es salaam ni maamuzi pia bwashee!
 
Safari ya Dodoma hatua iliyofikia inaitwa "point of no return", fedha iliyotumika kwenye majengo + hela za kuhamisha wafanyakazi, hakuna namna wanaweza kufanya reverse.
 
Ni maoni tu kwamba ni vema Rais wa JMT na taasisi saidizi zikarudi Dar es salaam na Makamu wa Rais, Waziri mkuu na Spika wa bunge wakaendelea kubaki Dodoma pamoja na wizara zote.

Uhamiaji wa Dodoma ulifanywa kwa haraka haraka na mambo mengi ya muhimu na msingi bado yako Dar es salaam ikiwemo Ikulu ya kihistoria ya Magogoni.

Dodoma itakapokamilika kwa miundombinu na kitaasisi basi Rais wa JMT arejee kwenye Ikulu ya Chamwino kama patakuwepo na ulazima huo wakati husika.

Mungu wa mbinguni awabariki.

Kazi Iendelee!
Ivi BOT na Gavana waliwahi kuhamia Dodoma pia?

Hii hoja ya kuwa Dodoma wamehamia haraka nashindwa ielewa. Huu uhamaji wa Taratibu na hadi CDA ikaanzishwa zaidi ya miaka 40 wameshindwa kuhamia. Kwa njia hii inayoitwa ya 'haraka', miaka minne wizara zote zimehama na wanaendelea kuimarisha mji wa serikali na Ikulu imejengwa?. Kwa akili ya kawaida tu, uhamaji wa taratibu kwa mwanadamu kamwe hauwezekanj, dar watu walishakuwa wamejiestablish huwezi wahamisha taratibu, inahitabu force. It was a matter of 'Do it now or Never'!.
Siyo lazima kuhamia Dodoma!
 
uendeshaji wa ofis ni ghali mno wabaki Dodoma foleni hapa dar zipungue
 
Kamwulize ambaye ameanza kusihi kwenye hilo jumba jeupe magogoni amekutana na kitu gani halafu urejee kutetea mawazo mfu. Makao makuu ya nchi ni sharti yabaki DODOMA. Mtwara na Kigoma ni lazima zipewe hadhi ya JIJI kwa kuonesha maendeleo ya akili, watu na vitu

Wabaguzi pekee ndio wanaotetea Ikulu kubaki Dar Es Salaam kwa kuwa ni wavivu na hawako kwa ajili ya kushiriki changamoto za wananchi wa chini.

Nilitegemea wapinzani kama ninyi mngetilia maanani suala la serikali kuwa DODOMA kiukamilifu badala ya kukimbilia raha za Dar huku wananchi maskini wakiendelea kuwa duni bila tumaini la kupata nafuu.
Je kuhamia DDM ndio kujali hali ya wanyonge? sioni mantiki ya kauli hii. Kuhamia DDM kumeligharimu Taifa fedha nyingi bila maandalizi ya kutosha. Maraisi waliotangulia isipokua Magu wailiona ni vema kuhamia kidogokidogo bila kuumiza wananchi. Unafrees ajira, promosion zote na kupeleka budget kiduchu isipokuwa Budget ya ujenzi hii sio sawa. Nchi hujengwa kwa kuendeleza watu na sii vitu. Kwa sasa na technolojia hii unadhani kuna haja ya kuwa DDM kwa sasa?
 
Nimekuelewa sana bwashee!
 
Back
Top Bottom