Rais na Waziri wa Kilimo kuhusu chakula nchini mnapotosha Taifa

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Wandugu,

Kuna lugha za kujirudiarudia kutoka kwa hawa viongozi wakisisitiza kwamba mkulima lima jiwekee cha kwako na familia yako chakula kingine nenda kauze nje mipaka ya nchi mipaka imefunguliwa.

Najiuliza ina maana wananchi wengine kama Dar es Salaam wanaotegemea vyakula hivyo havitawafikia kwa sababu mkulima ataangalia wapi atapata bei kubwa ya mazao na ukweli ni kwamba chakula kingi kinachukuliwa na Wakenya kwa kigezo cha bei nzuri na watu Dar es Salaam wanakosa chakula ndio maana kuna mfumuko wa bei mkubwa.

Kuna kitu kinaitwa food security, kwa Tanzania hakuna.
 
Maghala ya taifa na binafsi yana chakula cha kutosha.. wafanyabiashara wa ndani na nje wote wanakutana kwa mkulima bei ile ile.
 
Wandugu
kuna lugha za kujirudirudia kutoka kwa hawa viongozi wakisisitiza kwamba mkulima Lima jiwekee cha kwako na familia yako chakula kingine nenda kauze nje mipaka ya nchi mipaka imefunguliwa.
Najiuliza ina maana wananchi wengine kama Dar es salaam wanaotegemea vyakula hivyo havitawafikia kwa sababu mkulima ataangalia wapi atapata bei kubwa ya mazao na ukweli ni kwamba chakula kingi kinachukuliwa na wakenya kwa kigezo cha bei nzuri na watu Dar es salaam wanakosa chakula ndio maana kuna mfumuko wa bei mkubwa.
Kuna kitu kinaitwa food security kwa Tanzania hakuna.

Serikali ilishakuwa inanunua Chakula (mahindi) mikoa inayozalisha sana mahindi yoote kuanzia Mbeya,Songwe,Ruvuma,Rukwa Katavi Na kwingine Na kisha kuweka kwenye maghala isitoshe wafanyabiashara nao wana maghala yao wameshanunua mahindinya kutosha wameweka kwenye godown zao

Kwa hiyo haipo shida hiyo
 
Hebu zungumza kiuhalisia ww kuhusu upungufu wa chakula unaopelekea mfumuko wa bei. Kuruhusu uuzwaji holela wa chakula nje ya nchi kutatuletea shida mbeleni, Kama una familia utakuwa unajua
 
Hebu zungumza kiuhalisia ww kuhusu upungufu wa chakula unaopelekea mfumuko wa bei. Kuruhidu uuzwaji holela wa chakula nje ya nchi kutatuletea shida mbeleni, Kama una familia utakuwa unajua

Msipende kuwa mnadandia migongo ya wakulima mwaka jana bei zilikuwa mbovu sana za mahindi mkawa kimya

Haya mkulima pia ananunua mbolea bei Mara tatu ya kabla ya korona ila hamjaona kama kupanda bei mbolea kunaweza sababisha ukosefu wa chakula nchini
 
Mkulima ukishalima uza panapokupa faida ili mwakani ulime tena,kama kuna mtu anahitaji aje kununulia shambani kwa bei ya soko.

Kuna mwaka hapa wakulima motisha ya kulima kibiashara ilishuka, Vijana wengi sana waliamia kwenye bodaboda maana boda inalipa kuliko shamba.

Serikali ifunge mipaka iwapo kuna vita au njaa ya level 1.
 
Hebu zungumza kiuhalisia ww kuhusu upungufu wa chakula unaopelekea mfumuko wa bei. Kuruhusu uuzwaji holela wa chakula nje ya nchi kutatuletea shida mbeleni, Kama una familia utakuwa unajua
Kwani mikate ile ngano tunayokula ni ya Tanzania? Juan maghala ya taifa ya chakula na yameshawekwa hifadhi ya chakula

Tanzania hii wakulima wa mahindi ndio wengi kuliko Mazao mengine Na we we Lima kama tunavyolima wenzio msitake huruma wakati hamuwachangii hao wakulima wanapolima mahindi yao
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Mkulima ukishalima uza panapokupa faida ili mwakani ulime tena,kama kuna mtu anahitaji aje kununulia shambani kwa bei ya soko.

Kuna mwaka hapa wakulima motisha ya kulima kibiashara ilishuka, Vijana wengi sana waliamia kwenye bodaboda maana boda inalipa kuliko shamba.

Serikali ifunge mipaka iwapo kuna vita au njaa ya level 1.

We hata njaa ya level one wasifunge maana tunaweza nunua nchi nyingine hata Afrika kusini nako huwa sana mahindi mengi
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Msipende kuwa mnadandia migongo ya wakulima mwaka jana bei zilikuwa mbovu sana za mahindi mkawa kimya

Haya mkulima pia ananunua mbolea bei Mara tatu ya kabla ya korona ila hamjaona kama kupanda bei mbolea kunaweza sababisha ukosefu wa chakula nchini
Na uwa tunawaletea nada za kulalamika kuhusu mbolea kupanda bei
Hatuoni hata wakichangia saa hizi wanajifanya kutoa ushauri.
Waje walime mapori yaoo kibao huku
 
Kwani mikate ile ngano tunayokula ni ya Tanzania? Juan maghala ya taifa ya chakula na yameshawekwa hifadhi ya chakula

Tanzania hii wakulima wa mahindi ndio wengi kuliko Mazao mengine Na we we Lima kama tunavyolima wenzio msitake huruma wakati hamuwachangii hao wakulima wanapolima mahindi yao
Kabisa. Hivi inakuaje mtu anataka kazi ya mikono ya mwingine iminywe ili yeye ashibe? Mbona hatusemi serikali ihakikishe gesti house, usafiri, pembejeo kwa mkulima iwe bure ili akija kuuza kwa bei ya chini asiumie?
 
We hata njaa ya level one wasifunge maana tunaweza nunua nchi nyingine hata Afrika kusini nako huwa sana mahindi mengi
Njaa level 1 hata huko mashambani kunakuwa hakuna hivyo hata ukifungua hakuna mwenye chakula cha kupeleka nje, kila mtu kajihifadhia tumagunia twake akiomba njaa iishe mvua zije, serikali nayo ni reserve ndo inalisha sisi wa mjini tukiombea wakulima mvua zinyeshe walime tushibe.
 
Serikali inanunua chakula cha kutosha sana chini ya NMC. Na kila mkoa unaozalisha mahindi kuna maghala makubwa tu ya chakula. Waacheni wakulima wadogo nao wanufaike.

Food security unayosemea wewe ndio aliyoifanya magufuli na mahindi yaliyo kwenye maghala mfano ghala la Songea liliopo Ruhuwiko mahindi mengi yalioza na yakatupwa kwa sababu mtaani mahindi yalikuwepo sababu mipaka mingi ilifungwa, hiyo hali ilipelekea wakulima wengi kupata midororo ya kiuchumi miongoni mwao na kuacha kilimo.

Mipaka ikifunguliwa hivi itaongeza uzalishaji sababu ya uhakika wa soko na wakulima wengi wataludi kwenye kilimo.

Cha kufanya hapa ni kuongeza thamani mazao kama mahindi kwa kuyachakata kabisa na kuuza unga na product nyingine nje ya nchi na sio kuuza mahindi kama yalivyo. Kwahiyo ufunguaji wa mipaka watanzania tuchukulie kama fursa ambayo italeta chachu ya maendeleo kwa kuongeza uzalishaji zaidi na kufungua viwanda vya uongezaji thamani mazao ya kilimo.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kama tunataka mkulima auze kwa bei ndogo basi ianzishwe kodi ya watu wasiolima kwa ajili ya wakulima ili wakulima wawezeshwe. Tutakubali?
 
Kabisa. Hivi inakuaje mtu anataka kazi ya mikono ya mwingine iminywe ili yeye ashibe? Mbona hatusemi serikali ihakikishe gesti house, usafiri, pembejeo kwa mkulima iwe bure ili akija kuuza kwa bei ya chini asiumie?
Mkuu ubinafsi tumeumbiwa binadamu na kilimo kwa Tanzania ni kazi inayoumiza siku zote uyu jamaa anataka wakulima wasiuze eti yeye awe na chakula cha kutosha sasa ngoja wakulima wauze chote mpk debe lifike 40 elfu ndio tutaelewana.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Serikali inanunua chakula cha kutosha sana chini ya NMC. Na kila mkoa unaozalisha mahindi kuna maghala makubwa tu ya chakula. Waacheni wakulima wadogo nao wanufaike.

Food security unayosemea wewe ndio aliyoifanya magufuli na mahindi yaliyo kwenye maghala mfano ghala la Songea liliopo Ruhuwiko mahindi mengi yalioza na yakatupwa kwa sababu mtaani mahindi yalikuwepo sababu mipaka mingi ilifungwa, hiyo hali ilipelekea wakulima wengi kupata midororo ya kiuchumi miongoni mwao na kuacha kilimo.

Mipaka ikifunguliwa hivi itaongeza uzalishaji sababu ya uhakika wa soko na wakulima wengi wataludi kwenye kilimo.

Cha kufanya hapa ni kuongeza thamani mazao kama mahindi kwa kuyachakata kabisa na kuuza unga na product nyingine nje ya nchi na sio kuuza mahindi kama yalivyo. Kwahiyo ufunguaji wa mipaka watanzania tuchukulie kama fursa ambayo italeta chachu ya maendeleo kwa kuongeza uzalishaji zaidi na kufungua viwanda vya uongezaji thamani mazao ya kilimo.
Umeongea point sana. Watu wa mijini hatukujua tu kuwa serikali ilipofunga mipaka tukafurahia bei ya kutupa ya mahindi side effect ilikuwa nn kwenye kilimo. Gunia liliuzwa shambani mpaka elf 28,000/= unajiuliza huyu mkulima alipewa kila kitu bure au?

Na ingeachwa misimu mitatu mbele wakulima wengi wangeamia mijini sijui nani angelima.
 
Mkuu ubinafsi tumeumbiwa binadamu na kilimo kwa Tanzania ni kazi inayoumiza siku zote uyu jamaa anataka wakulima wasiuze eti yeye awe na chakula cha kutosha sasa ngoja wakulima wauze chote mpk debe lifike 40 elfu ndio tutaelewana.
Kuna hoja yako umeitoa nimeikubali sana. Umetumia akili. Sijajua kwann baadhi yetu tunapenda kutafuniwa wengine waumie sisi tufurahi.
 
Najiuliza ina maana wananchi wengine kama Dar es salaam wanaotegemea vyakula hivyo havitawafikia kwa sababu mkulima ataangalia wapi atapata bei kubwa ya mazao na ukweli ni kwamba chakula kingi kinachukuliwa na wakenya kwa kigezo cha bei nzuri na watu Dar es salaam wanakosa chakula ndio maana kuna mfumuko wa bei mkubwa.
Mkulima anapopata shida unamsaidia? Mfano akipata hasara hakuna hata mmoja anaejitahidi kumsaidia huwa anapambana mwenyewe. Iweje leo apangiwe bei na kuamriwa pa kuuza?

Na nyinyi Dar es Salaam mulime vya kwenu au mupambane na bei watakazoweka wao sio kuwa mufaidike nyinyi wakulima wapate hasara.
 
Halafu DSM Tz tunaiangalia sana ndo maana tumejazana huko. Mapato ya utalii yanaenda kujenga huko, madini yanaenda kujenga huko, Kilimo inatakiwa nchi ifungwe matumbo yasingurume.
 
Back
Top Bottom