Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Ok, point yangu ni kuwa mipaka sio sababu pekee ya bei kuwa juu, Bei kuwa juu hutokana na mwaka husika uzalishaji ulikuwa kiasi gani. Na uzalishaji kushuka pia Kuna sababu ambazo kubwa huwa ni hali ya hewa.Embu elezea hapa? Mkuu Una hakika ww ni mfanya biashara na muwekezaji mkubwa wa mazao? Mbona hili ni suala jepesi sana kwa wafanyabiashara maana pia huwa kunatabia ya kuzuia mzigo iwe michache sokoni ili bei ipande baada ya demand kuongezeka.
Unapofunga mipaka unaingilia market forces za demand and supply. Ukisema mahindi yasiuzwe nje tafsiri yake ni kuwa umesema mahindi yauzwe kwa wateja wa ndani tu ambao si wengi kama wakiwepo wa ndani na wa nje, kama watu wamevuna inamaana wateja ni wa ndani tu wanagawana mazao ambayo ni ya kutosha hapo bei lazima ishuke tofauti na ukiacha mipaka wazi wateja wa kenya na nchi nyingine wakaruhusiwa kununua unaruhusu demand kuwa juu na bei inakua juu.
Turudi miaka mitatu nyuma, Mwaka 2019 mipaka ilikuwa wazi na bei ilikuwa kubwa sana kuliko mwaka huu.gunia la mahindi lilifika 120k
Mwaka 2020 mipaka ilikuwa wazi ila gunia liliporomoka hadi kwa 30k.
Hapa tafsiri yake ni kuwa mipaka kuwa wazi sio sababu pekee ya Bei kuwa juu.
Kuhuu kuhifadhi na kuuza bei ikipanda ndio haswa nachofanya tena kwa kiwango kikubwa. Nilihifadhi 2019 na ilipofika November niliuza kwa bei kubwa Sana.
2020 nikahifadhi, Ila ilipofika November nikauza kwa bei ya hasara sana.
Mwaka Jana 2021 pia haukua mzuri sana.
Mwaka huu 2022 pia sio mzuri kwa kuwa uzalishaji umeshuka sana, wakulima wamepata mazao kidogo hivyo wanauza kwa bei ya juu sana. Hapa ndio wengi mnachanganya na kusema wakulima wanafaidika,
kwa mfano mkulima wa mpunga aliyekadiria kupata gunia 200, Kapata gunia 80. Huyu tayari ana hasara hapo, japo gunia ataliuza 100k.
Wenye faida ni wale waliokuwa na stock kubwa ya mwaka jana, kwa kuwa mwaka huu bei tu ya kununulia ili kusubiri November ni kubwa hivyo hakuna faida utapata. Ununue Leo gunia la mpunga 90k, alafu usubiri November au December uliuze kwa 110k au 120k huwezi sema umepata faida hapo.